Kiuzbeki
Kiuzbeki ni moja ya lugha za Kiturki za mashariki na lugha ya Kiturki yenye wasemaji wengi katika Asia ya Kati.
Kwa lugha yenyewe kuna majina "O‘zbek tili" kwa mwandiko wa Kilatini, "Ўзбек тили" (uzbek tili) kwa mwandiko wa Kisirili; au "ئۇزبېك تىلى" (o'zbek tili) kwa mwandiko wa Kiarabu.
Wasemaji
haririKiuzbeki ni lugha rasmi nchini Uzbekistan ambako kuna wasemaji milioni 21.
Wasemaji wengine wa lugha hii wako Tajikistan (milioni 1.2), Afghanistan (milioni 1), Kyrgyzstan (550,096), Kazakhstan (332,017) na Turkmenistan (317,333).
Mwandiko
haririTangu uenezaji wa Uislamu Kiuzbeki iliandikwa kwa herufi za Kiarabu.
Mapinduzi ya kibolsheviki yalileta mwandiko wa Kilatini kati ya 1929 na 1940 kwa kuiga mfano wa Uturuki. Lakini tangu 1940 siasa ikabadilika tena na lugha ikahamishwa kwa mwandiko wa Kisirili kama Kirusi.
Tangu uhuru wa mwaka 1991 mipango ilijadiliwa kurudi kwa mwandiko wa Kilatini. Azimio lilifanywa 1995 kutumia alfabeti ya Kilatini. Lakini hadi sasa mwandiko wa Kisirili bado unapatikana. Waislamu wengine wameendelea kutumia herufi za Kiarabu.
Shule zinatakiwa kufundisha miandiko yote mitatu ili vijana waweze kuendelea kusoma maandishi ya miaka ya nyuma.
Viungo vya nje
hariri- makala za OLAC kuhusu Kiuzbeki
- lugha ya Kiuzbeki katika Glottolog
- lugha ya Kiuzbeki katika Ethnologue
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiuzbeki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |