Kizito Mihigo
Kizito Mihigo (amezaliwa Kibeho, wilaya ya Nyaruguru, 25 Julai 1981) ni mwimbaji, mtunzi na muimbaji wa nyimbo za kanisa, mpiga kinanda na mtangazaji wa televisheni raia wa Rwanda. Mhanga wa mauaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994, mwanaharakati wa amani na maridhiano, kasomea nchini Ufaransa kwenye shule ya Conservatoire de Paris, mwaka wa 2010 alianzisha taasisi ya Kizito Mihigo Peace Foundation. Mwaka 2014, baada ya kutunga nyimbo iliyopinga mwelekeo wa serikali ya Rwanda, alitiwa mbaroni akishitakiwa kwa kosa la kutaka kuangusha serikali ya rais Paul Kagame.
Kizito Mihigo | |
---|---|
Amezaliwa | 1981 |
Asili yake | Kibeho, Rwanda |
Katika mwezi wa Februari 2015 baada ya kusomewa mashitaka alipewa kifungo cha miaka kumi.
Wasifu
haririKizito Mihigo alizaiwa katika uliokuwa mkoa wa Gikongoro, kusini mwa Rwanda. Ni mtoto wa tatu katika watoto sita ya familia ya Augustin Buguzi na Placidie Ilibagiza. [1]
Mwanzo wa muziki
haririWakati akiwa na miaka 9, alianza utunzi wa nyimbo za kanisa. Baada ya miaka mitano wakati alipokuwa ameanza kusoma shule ya secondary kwenye seminari ndogo ya Butare, alikuwa muimbaji bora wa nyimbo za kanisa [2]
Kunusurika mauaji ya kimbari
haririMwaka 1994, Kizito Mihigo alipoteza wazazi wake baada yakuwuliwa kwenye mauaji ya kimbali. Wakati wa vita alikimbilia nchini Burundi ambapo alikutana na baadhi ya watu wa familia yake na kujaribu kujiunga na jeshi ra RPA.[3]
Elimu
haririJulai 1994, alirudi nchini Rwanda akaendelea na masomo yake ya secondary. Wakati huo alijiandikisha kwenye seminari akipendelea kuwa padri, ili katika imani na kupitia muziki wake, aliwasamehe waliowaua wazazi wake katika mauwaji halaiki nchini Rwanda.[3]
Usanii wa muziki
haririMwaka 2001 alikua miongoni mwa wasanii walio tunga nyimbo mpya ya taifa ya Rwanda. Baada ya hapo alidhaminiwa na rais Kagame kama mhisani kwa kwenda kupata elimu zaidi katika fani ya muziki, kwenye shule ya Conservatoire de Paris.[4]
Mjini Paris, Mihigo alijifunza kinanda na utunzi wa nyimbo kwenye hiyo chuo, chini ya mwalimu kiongozi Françoise Levechin- Gangloff. [5]
Baada ya kozi na kurudi nyumbani
haririMnamo mwaka 2011, Kizito Mihigo alikuwa muimbaji bora wa nyimbo mbalimbali za kanisa na za kizalendo, tena msanii munyekweshimi kakatika jamii ya Rwanda.[6]
Mara nyingi, alikuwa akialikwa kutumbuiza kwenye waksha zote za makumbusho ya mauaji ya kimbali nchini Rwanda. Alikuwa akialikwa kwenye sherehe za kitaifa ambazo zilikuwa zikifanyika kwenye ukumbi wa bunge pamoja na kuimba wimbo wa taifa.
Ukosowaji na kujikosowa
haririUkaribiano wake na viongozi wa nchi ulisisimua ukosowaji wa mashabiki wake, ambao waliona tishiyo la kikiuka mwelekeo wa muziki wa kanisa na kuelekea katika siasa. Pamoja na hayo, msanii huyu alijaribu kuwahakikishia mashabiki wake kuhusu msimamo wa imani yake ya kikristo.[7]
Tamasha zake za kidini ziliwavutia watu wengi mjini Kigali na kote nchini. Na mara nyingi kutunukiwa kwa kizuliwa na viongozi wa serikali.[8][9]
Mnamo mwaka huo, tamasha iliotia fora ilifanyika wakati wa Pasaka na Krismasi.[10][11]
Matendo ya Usanii
haririBaada ya mauwaji halaiki ya 1994, mwimbaji huyu raia wa Rwanda alitunga nyimbo 400 katika miaka 20.[12]
Haswa zilizotia fora ni :
• Arc en ciel
• Twanze gutoberwa amateka
• Inuma
• Iteme
• Urugamba rwo kwibohora
• Mon Frere Congolais
• Mwungeri w'intama
• Yohani yarabyanditse
• Turi abana b'u Rwanda
• Igisobanuro cy'urupfu
• Umujinya mwiza
Mwanaharakati kwa amani na maridhiano ya kitaifa
haririKwa muda alipokaa Ulaya kwa mafunzo zaidi ya muziki, alipata fursa ya kufahamiana na chama cha kimataifa cha Mouvement International de la Reconciliatuon - MIR, na kupata upeo zaidi wa mchango wake wa kuwapatanisha Wanyarwanda katika fani ya muziki, kwa kutumbuiza nyimbo nyingi za kidini. [13]
Vile vile aligusia na kuwaalika kumuiya ya waishio nchi za ng'ambo kwa kuwafikishia njumbe wa kudumisha amani na kukuza moya wa maridhiano katika msamaa.
Baadhi ya tamasha zake huko Ubelgiji zilihudhuriwa na kumufurahishwa sana Kasisi wa mji wa Bruxelles, Monseigneur Léonard.[14]
Mnamo 2010, Kizito Mihigo aliazisha chama cha ushirika Kizito Mihigo Peace Foundation, shirika la kiraia kisicho cha kiserikali cha Kinyarwanda cha kutetea amani na maridhiano nchini Rwanda.[2]
Chama hiki kiliendeshwa shuguli zake mashuleni na magerezani nchini Rwanda, kwa mchango wa kudumisha amani na kuimarisha maridhiano baina wa wanainchi.[2]
Chama hiki cha ushilika kiliandaa vile vile mijadala ya kidini baina ya makanisa, ikirushwa hewani na runinga ya taifa..[15]
Tuzo
haririMwezi wa Agosti 2011, Kizito Mihigo alipokea tuzo la CYRWA (Cerebrating Young Rwandan Archivers) iliotolewa na mke wa raisi wa Rwanda, mama Jeannette Kagame.[16]
Aprile 2013, shirika la Kizito Mihigo Peace Foundation lilipokea tuzo la 8.000.000 pesa za Rwanda, lililotolewa na bodi ya utawala bora ya Rwanda (Rwanda Gouvernance Board), kwa mchango wa shirika dhizi ya utawala bora na kuamusha moyo wa upendo na uzalendo wa taifa.[17]
Isitoshe, hata Raisi wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame, alimtumiku mwanamuziki huyu, muhanga sa mauwaji halaiki, kama mfano bora bora ya kuigwa na vijana wa Rwanda katika maendeko ya kyamii na ki utamaduni.[12]
Mvunja mbavu katika runinga
haririTokea mwaka 2012, Kizito Mihigo katika kipindi cha vichekesho na mawaidha kwenye runinga ya taifa ya Rwanda, alihusika na kipindi cha Umusanzu w'umuhanzi (Mchango wa msanii). Kipindi hiki kilitayarishwa na kutolewa na shirika Kizito Mihigo Peace Foundation kwa kuwachangamusha wanyarwanda wasahau, katika msamaha na maridhiano, kipindi cha giza na chuki.[15]
Maisha binafsi
haririKizito Mihigo ni Mkristo wa Kanisa Katoliki. Hajaoa wala hana mtoto.
Mwezi Aprili 2013, gazeti la Rwanda The New Times lilimupanga na kumutangaza kuwa mrembo wa kiume wa pili nchini Rwanda.[18]
Mikononi mwa nguvu za dola
haririMwezi wa Aprile 2014, katika maandalizi ya miaka ishirini ya kumbukumba ya mauwaji ya kimbali nchini Rwanda, habari zilivuma kuhusu kutoweka kwake. Ni baada ya kutunga wimbo ya utatanishi ambayo haikufuraishi serikali ya Rwanda. Nyimbo hiyo ilichululiwa kama fikra ya uchochezi ya wapinzani. Wiki umoja baada ya kutoweka kwake, kufuatia shinikizo ya jumua ya kimataifa, polisi ilitangaza kumshikilia msanii huu na kumuonesha mbele ya vyombo vya kimataifa, eti ni mhaini alitaka kipinduwa serikali kwa kushikiana na vyama vya upinzani vilivyo uhamishoni. Kizito Mihigo alikiri na kukubali makosa yote na kuomba msamaa kwa mashitaka yote dhidi yake. [19][20]
Wimbo Wa utata
haririWimbo Igisobanuro cy'urupfu (ufafanuzi ya kifo) chini ya utunzi wake msanii Kizito Mihigo, mnamo mwezi Mach 2014, wiki chache kabla ya sherehe ya kumbukumbu ya miaka 20 ya mauwaji halaiki, ilizuwa utata, hata Serikali ilifikia hatuwa ya kuinyamazisha na kupiga marufuku. [19]
Katika baadhi ya ushahiri ya wimbo huu, yaliimba maneno yafuatayo: "Mimi ni mhanga wa mauwaji halaiki, pamoja na hayo hamizuiyi, kuwa na moyo wa ubinadamu [...] kuwa na utu ni vema zaidi kuliko kusimama katika uzalendo wa Kinyarwanda"[21]
Kesi na matokeo
haririKesi
haririWakati wa kesi ya Kizito Mihigo, mwendesha mashtaka alikuwa ameomba hukumu ya adhabu ya kufungo cha maisha dhidi ya msanii huyu.[12]
Washtakiwa wenzake walieleza mateso walio yapata walipokuwa korokoroni na kulazimishwa kukiri makosa yao.
Tarehe 27 Februari 2015, baada ya kusomewa shtaka la kupatikana na hatia ya "uhaini zidi ya serikali" hukumu ilitolewa na Kizito Mihigo kupewa kifungo cha miaka 10.[21]
Matokeo
haririBaada ya kukamatwa kwake na kutolewa hukumu ya kifungo cha miaka10, vyombo vya utangazaji za kimataifa haswa Radio France Internationale, Al Jazeera na kadhalika ziligusia kuhusu wimbo Igisobanuro cy'Urupfu (ufafanuzi ya kifo) na kueleza maneno katika wimbo huu, ambayo haikuwafuraisha viongozi wa nchi, ndio sababu ya kifungo chake.[19]
Inchi za Amerika na Ungereza, wafadhili wakubwa wa serikali hiyo, walionyesha wasiwasi wao dhidi ya kukamatwa kwa msanii Kizito Mihigo.[22]
Mashirika ya kimataifa za kutetea haki za kibinadamu, kama Human Rights Watch, International Federation of Human Rights - FIDH na Amnesty Internationale vile vile zililaumu kesi hiyo.
Marejeo
hariri- ↑ (Kiingereza)Kizito Mihigo Urges Artistes to Promote Peace Through Music|, 10 april 2014 AllAfrica
- ↑ 2.0 2.1 2.2 (Kiingereza)Kizito uses music to promote peace, reconciliation, 20 november 2012 Archived 23 Septemba 2015 at the Wayback Machine. The New Times
- ↑ 3.0 3.1 (Kiingereza)How l overcame desire for revenge – Kizito Mihigo, 25 april 2011 Archived 1 Oktoba 2015 at the Wayback Machine. The New Times
- ↑ (Kifaransa)Kizito Mihigo, chanteur vedette et accusé en aveux, 25 april 2014 Le Soir
- ↑ (Kifaransa)Biographie de l'artiste rwandais Kizito Mihigo, 9 juni 2009 Archived 29 Oktoba 2023 at the Wayback Machine. Rwandaises.com
- ↑ (Kifaransa)Rwanda: Un artiste s'insurge contre les falsificateurs du genocide, 19 april 2011 Pana Press
- ↑ (Kiingereza)Kizito Mihigo churns out Liberation song, 28 Juni 2011 The New Times
- ↑ (Kiingereza)Mihigo planning mega concerts, 4 september 2010
- ↑ (Kiingereza)Kizito Mihigo’s concert was grand, 1 november 2011 The New Times
- ↑ (Kiingereza)Kizito Mihigo excites fans on Xmas , 27 november 2011
- ↑ (Kiingereza)Kizito thrills fans during Easter, 25 april 2011 The New Times
- ↑ 12.0 12.1 12.2 (Kifaransa)Rwanda: la perpétuité requise pour Kizito Mihigo, 30 december 2014 BBC.
- ↑ (Kifaransa)Bulletin du MIR France, 12 decembre 2007 Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- ↑ (Kifaransa)Mgr Léonard: "Je ne peux pas voir en Kizito Mihigo un homme qui serait dangereux pour la société ", 30 juli 2015, Jambo News
- ↑ 15.0 15.1 (Kiingereza)Kizito Mihigo using music to spread Peace un the society , 3 octobre 2012 Archived 18 Mei 2015 at the Wayback Machine. The Independent (Uganda)
- ↑ (Kiingereza)First Lady awards young Rwandan achievers, 20 Augustus 2011 Archived 14 Agosti 2017 at the Wayback Machine. The New Times
- ↑ (Kiingereza)Civil society organs win RGB grants , 21 april 2013 Archived 6 Oktoba 2015 at the Wayback Machine. Great Lakes Voice
- ↑ (Kiingereza)Top 8 hottest male cerebrities in Rwanda , 23 april 2013 Archived 12 Julai 2015 at the Wayback Machine. The New Times
- ↑ 19.0 19.1 19.2 (Kiingereza)Dissident ‘choirboy’: Rwandan gospel star on trial, 11 december 2014 Al Jazeera
- ↑ (Kifaransa)Rwanda: quatre personnes arrêtées, dont le chanteur Kizito Mihigo, 16 april 2014 RFI
- ↑ 21.0 21.1 (Kifaransa)Le célèbre chanteur rwandais Kizito Mihigo condamné à 10 ans de prison, 27 february 2015 France 24
- ↑ (Kifaransa)Rwanda: Washington préoccupé par la vague d'arrestations, 24 april 2014 Radio France Internationale
Viungo vya nje
hariri- Official website
- Kizito Mihigo Peace Foundation Archived 16 Januari 2013 at the Wayback Machine.