Radio France Internationale
Radio France Internationale (RFI; Redio ya Dunia ya Ufaransa) imeasisiwa kwa jina hili na serikali ya Ufaransa katika 1975 kama sehemu ya Radio France. Ilikuwa imefanya kazi tangu 1931 kwa majina mbalimbali. Katika 1986 Ubunge wa Ufaransa ulibadilisha sheria ili kuruhusu RFI ifanye kazi bila udhibiti wa Radio France.
| |
Kutoka mji | Paris |
Nchi | Ufaransa |
Eneo la utangazaji | ulimwenguni kote |
Kituo kilianzishwa mwaka | Januari 1975 |
Mwenye kituo | serikali ya Ufaransa |
Programu zinazotolewa | idhaa za redio kwa lugha za dunia |
Tovuti | rfi.fr |
RFI inafanya kazi chini ya himaya ya Waziri wa Ufaransa wa Mambo ya Nchi za Nje na inapata pesa kutoka kwa bajeti yake. Inatangaza kwa Kifaransa hasa lakini kwe Kiingereza, Kiswahili, Kihausa, Kihispania, Kireno, Kiromania, Kirusi, Kiajemi, Kichina, Kivietnam na Kikhmer pia. Inamiliki pia Redio w:Monte Carlo Doualiya inayotayarisha vipindi kwa Kiarabu katika Paris na kuvitangazia hadhira katika Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati kutoka transmita katika Kupro.
Marejeo
Makala hii kuhusu vituo vya redio bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Radio France Internationale kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |