Konokono

(Elekezwa kutoka Koa (mnyama))
Konokono
Helix pomatia, spishi ya konokono wa nchi kavu
Helix pomatia, spishi ya konokono wa nchi kavu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Mollusca (Wanyama bila mifupa wenye ulimi kama tupa)
Ngeli: Gastropoda
Cuvier, 1797
Ngazi za chini

Oda 8:

Konokono (pia koa lakini kwa kweli ni kombe la konokono) ni wanyama wa ngeli ya Gastropoda katika faila Mollusca. Neno konokono linatumika kujumuisha wale wa nchi kavu, wa maji baridi na wa bahari. Spishi nyingi zina koa lililojiviringisha na kukua katika hatua. Spishi nyingine zinakosa koa (au zinalo dogo sana) na huitwa konokono uchi.

Konokono hupatikana maeneo mengi kama vile miferejini, jangwani, hata kwenye vina virefu baharini. Ingawa watu wengi wanaufahamu na konokono wanaopatikana nchi kavu tu, hawa wa ardhini ni kidogo mno. Konokono wa majini ndio wengi sana na huchangia kiasi kikubwa cha spishi ya konokono na wana aina nyingi sana na hata maumbo ya kibailojia makubwa zaidi. Konokono wengine wengi kiasi pia hupatikana kwenye maji baridi. Konokono wengi hula majani, japo baadhi yao hula majani na nyama, na wengine huwinda na kula nyama tu.

Konokono wanaopumua kwa kutumia mapafu huwekwa kwenye kundi la Pulmonata, huku wale wenye yavuyavu huuunda kundi la paraphyletic group; kwa maneno mengine konokono wenye yavuyavu wameanishwa kwenye makundi yasiyo husianiana sana. Konokono wenye mapafu na wale wenye yavuyavu kwa nyakati nyingi za mabadiliko wa mfumo wa miamba imepelekea hata baadhi ya konokono wenye mapafu kuishi baharini na hata wale wenye yavuyavu nao kuishi nchi kavu Konokono wana maumbile maelfu yafananayo na meno. Meno haya maelfu madogo yanapatikana kwenye ulimi na hufanya kazi kama tupa na kusaga chakula kwenye vipande vidogo. Ulimi wao huitwa radula.

Aina za konokono kulingana na makazi

hariri

Spishi aina ya gastropod ambao hawana na koa kwa ujumla huitwa slugs badala ya konokono, ingawa, licha ya kutokuwa na makombe au hata kama wanakuwa na makombe madogo, hakuna tofauti kubwa baina ya konokono na slugs zaidi ya tabia na makazi. Kama ilivyo mnyama asiye na kombe anaweza kujongea kwa urahisi, na hivyo hata slugs wakubwa kabisa wanaweza kufanikiwa kuishi katika mazingira tofauti na hata kutosha katika sehemu ndogo sana, ambazo hazitoshi hata konokono wadogo, kama vile kwaenye magamba ya miti yaliyolegea au chini yam awe, magogo au vipande vya mbao vilivyo ardhini.

Kuonesha utamaduni

hariri
 
Konokono aitwaye Moche. (Scutalus sp) 200BK, Larco Museum Collection,, Lima Peru.

Kutokana na kuwa kwake taratibu, konokono amekuwa akionekana kama alama ya uvivu. Katika tamaduni za Kikristo za Yudea, imeonekana mara zote kama uthibitisho wa zambi kubwa ileatayo kifo ya uvivu. Zaburi 58:8 inatumia udanganyifu/ werevu wa konokono kama adhabu ya sitiari.

Konokono mara nyingi wametumika kwenye imani na utakatifu. Mshairi mmoja wa Kigiriki aliandika kuwa konokono hutambulisha msimu wa mavuno kwa kukwea mashina ya mimea, wakati mungu wa mwezi wa Aztec, Tecciztecatl huoneshwa kwa kombe la konokono mgongono mwake. Hii humaanisha kuzaliwa upya; utaratibu wa konokono kuonekana na kutoweka hufananishwa na mwezi. Na hivi karibuni, Carl Jung alitambua uwakilishi wa nafsi kwenye ndoto. Katika saikolojia, sehemu laini za ndani za konokono hufananishwa na mambo tunayoyafanya bila ya fahamu huku kombe likionesha fahamu.

Katika hotuba, msemo “mwendo wa konokono” mara nyingi huonesha mchakato wa taratibu usio makini.

Pia msemo “barua konokono” mara sote humaanisha taratibu za huduma za kawaida za kutuma karatasi zenye ujumbe tofauti na maatumizi ya barua pepe, ambayo kwa hakika ni ya haraka.