Kakao
Kakao (pia: kakau[1]; kwa Kiingereza: cocoa) ni zao la mkakao linalotolewa katika mbegu iliyomo ndani ya tunda linaloitwa mkokwa.
Jina hilo hutumiwa kwa ajili ya mbegu za mkakao, kwa unga unaotengenezwa kutoka mbegu hizo na pia kwa kinywaji kinachotengenezwa kwa unga wa mbegu pamoja na maji au maziwa na sukari.
Matumizi ya kakao yalianza huko Amerika ya Kati, hasa Meksiko, ambako walipenda kinywaji lakini walitumia pia mbegu kama pesa.
Mbegu ya kakao huvunjwa, hukaangwa na kusagwa; kuna mafuta mengi ndani ya mbegu, na kwa matumizi ya kinywaji ni lazima kutenganisha mafuta na unga kavu; hivyo sehemu kubwa ya mafuta ya kakao hutolewa; kwa chokoleti yanahitajika tena[2].
Mkakao hulimwa sana nchini Ghana, lakini pia Tanzania katika maeneo kama vile Kyela. Hata hivyo mwanzoni kulikuwa na ugumu wa soko kwa zao hilo mpaka kufikia wakati ambao lilipoanza kupaa na kuhitajika zaidi kibiashara.
Marejeo
hariri- ↑ Kakau ni tahajia inayopendezwa zaidi na kamusi ya KKS
- ↑ Zipperer, Paul (1902). The manufacture of chocolate and other cacao preparations (3rd ed.). Berlin: Verlag von M. Krayn, inapatikana archive.org
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kakao kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |