Konvict Muzik
Konvict Muzik ni studio ya kurekodia muziki inayomilikiwa na mwimbaji wa R&B na hip hop Akon. Mbali na Akon, kuna wanamuziki waliomaarufu kama vile T-Pain, Ray Lavender na Kardinal Offishall ambao wote wamesaini mkataba na studio hiyo. Toka mwanzo nyimbo nyingi za wasanii wa Konvict Muzik huwa zina radha ya muziki wa clank, kufuatia na mwenyewe Akon vile alivyoanza na nyimbo yake ya "Konvict" kuwa na radha ya aina hiyo.
Konvict Muzik | |
---|---|
Shina la studio | Universal Music Group |
Imeanzishwa | 2005 |
Mwanzilishi | Akon |
Ilivyo sasa | Inafanya kazi |
Usambazaji wa studio | Interscope Records, Jive Records/Zomba Label Group/LaFace Records |
Aina za muziki | Mbalimbali |
Nchi | Marekani |
Mahala | Atlanta, Georgia |
Tovuti | KonvictMuzik.com KonvictOnline.com |