Faheem Rasheed Najm (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama T-Pain; amezaliwa 30 Septemba 1985) ni mwimbaji, mtunzi, rapa, na mtayarishaji wa rekodi kutoka Marekani.

T-Pain

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Faheem Rasheed Najm
Amezaliwa 30 Septemba 1985 (1985-09-30) (umri 39)
Tallahassee, Florida, U.S.
Aina ya muziki R&B, hip hop
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi, rapa, mtayarishaji wa rekodi, dansa
Ala Kinanda
Miaka ya kazi 2004–mpaka sasa
Studio Nappy Boy, Konvict, Jive
Ame/Wameshirikiana na Akon, Chris Brown, Tay Dizm, Young Jeezy, DJ Khaled, Flo Rida, Lil Wayne, Ludacris, Plies, Rick Ross, Kanye West, Twista, Travis McCoy, Lil Mama, The Lonely Island
Tovuti www.t-pain.net

Wasifu

hariri

Najm alizaliwa mjini Tallahassee, Florida.[1] Jina lake la kisanii ni kifupi cha "Tallahassee Pain" ("Tallahassee Mauimivu) na amechagua jina hilo kwa sababu ya ugumu wa maisha aliyoyapata wakati anaishi huko.[2]

Alianza shughuli za urapa akiwa katika kundi la Nappy Headz. Mnamo mwaka wa 2005, akawa mwimbaji na kuweza kutoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa Rappa Ternt Sanga ikiwa na vibao vyake vikali vya "I'm Sprung" na "I'm N Luv (Wit A Stripper)".

Shughuli zake kama mwimbaji, T-Pain ametumia sana kionjo cha sauti cha Auto-Tune. Tangu kutolewa kwa albamu yake ya kwanza, T-Pain ametayarisha vibao kadhaa vikali vyake mwenyewe na vya marapa na waimbaji wengine wa R&B. T-Pain pia amekuwa na single kumi kwenye chati za Billboard Hot 100. Mnamo mwaka wa 2008, ameshinda tuzo ya Grammy na rapa Kanye West kwa ajili ya single ya "Good Life". Mnamo mwaka wa 2010 ameshinda tuzo nyingine ya Grammy na Jamie Foxx kwa ajili ya single ya "Blame It". T-Pain pia ni mwanzilishi wa studio ya kurekodia ya Nappy Boy Entertainment, imeanzishwa mwaka wa 2005.

Diskografia

hariri
Single zake

Marejeo

hariri
  1. T-Pain Gets Some Heat For Turning Gospel Song Into 'Alcoholic Anthem'. Ilihifadhiwa 6 Desemba 2010 kwenye Wayback Machine.. Retrieved 28 Agosti 2008.
  2. Koha, Nui Te. "Escaping Tallahassee", Herald Sun, 2007-06-10. Retrieved on 2008-12-10. Archived from the original on 2012-12-09. 

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: