Krioli ya Guyani ya Kifaransa

Krioli ya Guyani ya Kifaransa ni lugha ya Krioli inayotumiwa hasa katika Guyani ya Kifaransa na katika nchi jirani za Surinam na Gayana. Kwa Kifaransa inaitwa Créole guyanais, wenyewe wanasema Kriyòl Gwiyannen.

Ni lugha ya Krioli yenye asili ya Kifaransa, pamoja na athira za lugha za Kiafrika, Kiindio, na Kireno. Inafanana na Krioli ya Visiwa vya Karibi: kuna tofauti za msamiati na sarufi lakini kwa jumla wasemaji huelewana.

Lugha hiyo ni tofauti na Krioli ya nchi jirani Guyana (Guyanese Creole) ambayo ni lugha yenye asili ya Kiingereza.

Mifano

hariri
Kikrioli cha Guyani ya Kifaransa
/matamshi/
Kifaransa sanifu Kiswahili
Bonswè /bõswɛ/ Bonsoir Jioni njema! (habar za jioni)
Souplé /suːple/ S'il vous plaît Tafadhali
Grémési /mɛsi/ Merci Asante
Mo /mo/ Moi, me, je Mimi
To /to/ Toi, te, tu Wewe
I, Li /i, li/ Lui, le, la Yeye
Roun /ʁuːn/ Un, une Moja
Èskizé mo /ɛskize mo/ Excusez-moi Unisamehe
Lapli ka tonbé /laˈpliː ka tõbe/ Il pleut mvua inanyesha
Jod-la a roun bèl jou /ʒodˈla a ruːn bel ʒu/ Aujourd'hui, il fait beau Leo ni siku nzuri
A kouman to fika? /a kumã to fika/ (Comment) ça va? habari zako?
Mari a mo manman /maʁi a mo mãˈmã/ Marie est ma mère Maria ni mama yangu
Rodolf a to frè /ʁodolf a to frɛ/ Rodolphe est ton frère Rodolf ni kaka yako
I k'alé laplaj /i kaːle laˈplaʒ/ Il va à la plage Anakwenda mwambaoni
Mo pa mélé /mo pa mele/ Je m'en moque Sijali

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Krioli ya Guyani ya Kifaransa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.