Kulipuliwa kwa makazi ya Benjamin Netanyahu, Israeli.

Kulipuliwa kwa makazi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, huko Caesaria Israel, siku ya Jumamosi ya tarehe 18 Oktoba,2024, kunatoa picha mpya ya mwelekeo wa mzozo wa Mashariki ya Kati. [1]

Benjamin Netanyahu

Shambulio hilo lililofanywa na droni ya teknolojia ya kisasa ni sehemu ya madhara ya mashambulizi ya Hezbollah dhidi ya Israeli katika siku moja. Shambulio lao lingine ni la mvua ya maguruneti yaliyorushwa na Hezbollah katika kile kinachoaminika kuwa ndio utekelezaji wa kiapo chao cha kulipiza kisasi walichokitoa kufuatia kuuwawa kwa Yahya Sinwar wa Hamas, tarehe 16 Oktoba,2024. Takwimu zimetaja idadi ya maguruneti hayo kuwa ni 100.[2]

Tamko la Israel

hariri

Kufuatia shambulio hilo, serikali ya Israeli imeishutumu Iran kwa kujaribu kumuua Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Hata hivyo, uchambuzi wa masuala ya kisiasa uliokuwa ukifanywa mbashara na runinga ya Al Jazeera, ulionesha kutoamini hilo na kuongeza kuwa hiyo ni mbinu ya Idara ya Usalama ya Israeli ya kujaribu kuokoa jahazi.[3]

Linapotokea shambulizi baya kama hilo na kudhihirisha wazi kushindwa kwa jeshi kuilinda nchi dhidi ya mashambulizi, propaganda inabidi itumike ili kulinda umoja. Wangesema kuwa wamepigwa na Hezbollah, kungetokea machafuko, hivyo inabidi asingiziwe adui mkubwa zaidi mwenye uwezo wa kijeshi na kimbinu.[4]

Taarifa zaidi

hariri

Taarifa zaidi kuhusu shambulio hilo zinasema kuwa, limeonesha wazi kuvuja Kwa mfumo wa usalama wa Israel kwani droni hiyo iliweza kupenya ndani ya anga la Israeli na kusafiri kilomita 70 (kuanzia Lebanoni) kisha kuranda randa kwa muda mrefu ndani ya Israeli kabla ya ' kujiridhisha ' juu ya pale inapopalenga na kupalipua.[5]

Zipo taarifa pia kuwa ndege za kijeshi ziliibaini katika mida ya mwisho mwisho na kuifuatilia lakini hawakuweza kuichukulia hatua mpaka iliposhambulia.

Mpaka habari hizi zikiwa zimesambaa sana ulimwenguni, si Hamas wala Hezbollah waliothibitisha kuhusika nalo, hali kadhalika, ripoti za kipolisi na kitabibu zimeonesha kuwa shambulio hilo halikuleta madhara kwa binadamu. Jumba la Netanyahu lililoshambuliwa liko kwenye fukwe za Caesarea, kaskazini mwa Israeli.[6] Bwana Netanyahu na familia yake hawakuwepo kwenye jumba hilo wakati wa shambulio.

  1. https://www.aljazeera.com/news/liveblog/2024/10/19/live-israeli-attack-kills-at-least-33-in-north-gazas-jabalia-refugee-camp
  2. https://www.palestinechronicle.com/netanyahus-caesarea-home-hit-by-drone-from-lebanon-unprecedented-attack/
  3. https://www.mirror.co.uk/news/world-news/breaking-israel-blames-iran-drone-33926853
  4. https://www.aljazeera.com/news/2024/10/19/drone-hits-netanyahus-home-as-hezbollah-rockets-target-northern-israel
  5. https://www.palestinechronicle.com/netanyahus-caesarea-home-hit-by-drone-from-lebanon-unprecedented-attack/
  6. https://www.deccanherald.com/world/israel-prime-minister-benjamin-netanyahus-home-targeted-by-drone-attack-days-after-hamas-chief-yahya-sinwars-killing-3239678