Kuponi (kutoka Kiingereza "coupon"), katika mada ya soko na uuzaji, ni tiketi, kijifurushi ama kijikaratasi ambacho kinaweza kukombolewa kwa fedha na kurejeshwa wakati wa ununuzi wa vitu. Kuponi ni njia moja ya kuwapa wateja punguzo la bei kwa bidhaa wanazozinunua.

Kuponi

Kawaida kuponi hutolewa na watengenezaji ili itumike ndani ya uuzaji kama njia moja ya kukuza mauzo. Mara kwa mara husambazwa kupitia bahasha, magazeti, wavuti kama vile mitandao ya kijamii, barua pepe, moja kwa moja kutoka kwa muuzaji, simu kama vile rununu ama simu ya mkononi.

Kuponi hufanya kazi kama vile ubaguzi wa bei, kuwezesha muuzaji kupewa bei iliyo chini kwa wale watumiaji ambao wanaweza kwenda mahala pengine. Kuponi zinaweza kutolewa kwa masoko fulani ambapo kuna ushindani mkubwa. Kwa serikali, kuponi ni kijikaratasi ama kijifurushi ambacho hutumika kwa umuhimu ama ruhusa.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuponi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.