Simu za mikononi

(Elekezwa kutoka Simu ya mkononi)

Simu ya mkononi (lakabu simu ya kiganjani, simu bila waya, simumnara, simu-selula, rununu, rukono[1]) ni simu ndogo inayobebeka.

Siemens AX72
Ndani ya simu za mikononi

Simu ya mkononi inaweza kutumika kwa mawasiliano ya mbali bila waya. Inafanya kazi kwa kuwasiliana na kituo cha mawasiliano kwa njia ya mnara (vilevile huita "mnarani") ambayo inaunganisha na mtandao mkuu wa simu. Ikiwa inatembea, kama simu inakuwa mbali sana na mnara iliyoungana nao awali, ule mnara unatuma ujumbe kwa mnara mwingine wa karibu kupokea mawasiliano. Utaratibu huu unasaidia simu isikatike, hivyo basi mawasiliano yanaendelea kwa kuunganishwa huko. Kupasiana huko kwa minara (lugha ya kitaalamu "hand-off"), kunatokea kiasi kwamba hata mtumiaji hawezi kujua kitu kama hicho kimetokea.

Teknolojia hii wakati ilipoanza ilikuwa ghali mno. Lakini kadiri inavyozidi kujulikana kutumika, ndivyo inavyozidi kuwa na gharama za chini, kiasi kwamba siku hizi karibu kila mtu anaweza kumudu gharama za matumizi ya simu ya mkononi.

Muundo mpya wa simu za mkononi unaitwa "SimuJanja" au "simu mtelezo". Muundo huu umekuwa maarufu ndani ya muda mfupi. Sehemu kubwa ya simu zilizotengenezwa kuanzia mwaka wa 2010 ni "simujanja". Zinaweza kutumika kama kompyuta na vilevile kupiga simu.

Marejeo

hariri
  1. Ulyseas, Mark (2008-01-18). "Of Cigarettes and Cellphones". The Bali Times. Iliwekwa mnamo 2008-02-24.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: