Kura ya maoni zinatumika katika demokrasia ili kuchagua viongozi wa nchi au kuamua kama sheria fulani itumike. Kawaida kura ya maoni hupigwa na wale wote wenye umri halali wa kupiga kura ili kukubali au kukataa pendekezo, sera, sheria, mabadiliko ya katiba, katiba mpya, kukataa au kumuunga mkono kiongozi fulani. Kura ya maoni huchukuliwa kuwa ni aina mojawapo ya demokrasia ya moja kwa moja.

Kura ya maoni juu ya aina ya serikali ya Italia mwaka 1946: Jamhuri au ufalme?