Kurt Georg Kiesinger
Kurt Georg Kiesinger (6 Aprili 1904 - 9 Machi 1988) alikuwa mwanasiasa kutoka nchini Ujerumani.
Kiesinger alizaliwa Ujerumani ya Kusini. Alisomea masuala ya historia mjini Tübingen na baadaye sheria mjini Berlin.
Alijiunga na Chama cha Nazi mnamo mwaka 1933, na kufanyakazi katika serikali hiyo. Baada ya vita kwisha aliswekwa lumande mjini Ludwigshafen. Aliachiwa huru baada ya kuonekana baadhi ya kumbukumbu zake katika kijitabu chake binafsi kilichokuwa kikielezea kupinga maangamizi ya Uyahudi katika kitengo chake, na akajaribu kuwazuia wahusika wa matendo hayo.
Mnamo mwaka wa 1946, alianza rasmi shughuli za kisiasa kwa kupitia chama cha CDU.
Kuanzia mwaka 1958 hadi 1966, alikuwa Rais Waziri wa Baden-Württemberg, kuanzia mwaka 1967 hadi 1971 alikuwa mwenyekiti wa chama cha CDU.
Kuazia mwaka 1966 hadi 1969, alikuwa Chansela wa Ujerumani ya Magharibi.