Kutoweka kwa Azory Gwanda

Azory Gwanda (alizaliwa 1975 - kutoweka Novemba 21, 2017) ni mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mawasiliano ya Mwananchi[1] jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Alitoweka kwa kushangaza mwishoni mwa mwaka 2017 kutoka nyumbani kwake karibu na Kibiti, Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani, Tanzania.[2][3]

Maisha binafsi

hariri

Azory Gwanda alikuwa ana umri wa miaka 42 wakati wa kutoweka kwake. Gwanda alikuwa akiishi katika shamba karibu na Kibiti, Tanzania, na mkewe Anna Pinoni. Mama yake, Eva Mpulumba kutoka kijiji cha Msimba katika Mkoa wa Kigoma, aliishi na familia yake yote, lakini ndiye ndugu pekee aliyehojiwa kuhusu kupotea kwa Gwanda.[4]

Wakati akifanya kazi katika Kampuni ya Mawasiliano ya Mwananchi kama mwandishi wa habari, Gwanda aliandika mfululizo wa habari za mauaji ya maafisa wa serikali za mitaa na maafisa wa polisi na washambuliaji wasiojulikana.[5] Gwanda alikuwa mwanahabari wa kwanza kuandika habari hizi. Aliliandikia gazeti la Mwananchi machapisho yake na gazeti la The Citizen.[6] Alifanya kazi kutoka Kituo cha Kibiti, ambapo mara ya mwisho alionekana na watu wasiojulikana.[7]

Kutoweka

hariri

Gwanda hajasikika tangu kutoweka kwake mnamo Novemba 2017. Mkewe Ana Pinoni alimwona mara ya mwisho kwenye shamba lao Kibiti kwenye Toyota Land Cruiser akiwa na wanaume wasiojulikana, akidai alikuwa akihama kibiashara kwa dharura wakati pia akiomba amkabidhi funguo zote za nyumba yao.[8]

Baada ya kuondoka kwa Gwanda na wanaume hao, Pinoni alirudi nyumbani na kukuta nyumba imevurugwa, ikionyesha ilikuwa imepekuliwa. [9] Hapo awali, Gwanda alitembelewa na watu hao wasiojulikana katika eneo lake la kazi na kutaka mazungumzo nae, na baadae walimlazimisha kuingia ndani ya gari. Masaa mawili baadaye, Gwanda na wanaume hao walifika nyumbani kwake huko Kibiti.[10] Hapo awali, mke wake Gwanda hakuwa na wasiwasi na kuondoka kwa Gwanda ghafla, lakini aliposhindwa kurudi nyumbani au kujibu simu kwa siku mbili alikwenda kwa mamlaka husika.[11] Kampuni ya mawasiliano ya Mwananchi ilisema haina habari juu ya wapi Gwanda alikuwa amepelekwa, au kwanini.[12] Ingawa kuna habari chache zilizokusanywa ambazo zinaonyesha matukio ambayo yalisababisha kutoweka kwa Gwanda, hakuna ushahidi kamili ambao umekusanywa unaoweza kuonyesha mahali alipo mpaka sasa.[13]

Mapokeo na mwitikio

hariri

Wakati kidogo kinajulikana kuhusu watekaji wa Gwanda, inadhaniwa kuwa walikuwa wanafungamana na mfululizo wa habari za mauaji ambazo Gwanda alikuwa akiziandika. Kesi hii ya jinai ilikuwa ikiendelea kwa miaka mbili na watu wengine karibu arobaini kuuawa kabla ya kutoweka kwa Gwanda.[14] Utoaji wa habari hizi za mauaji zinaweza zikawa chanzo cha kumfanya Gwanda kuwa mlengwa na watu hawa wasiojulikana.[15][16]

Kupotea kwa Gwanda kumechochea mashirika mengi kujitolea kusimamia na kulinda haki za waandishi wa habari ulimwenguni kote. Haukupita hata mwezi mmoja baada ya kutoweka kwa Gwanda, shirika MISA Tanzania ilitoa tamko la kufadhaika kwao juu ya  ukosefu wa taarifa kamili kuhusiana na kutoweka kwa Gwanda, na kukiita kitendo hicho kuwa "shambulio la uhuru wa waandishi wa habari ambalo lazima lihukumiwe"[17] Theophil Makunga, mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wa Tanzania, alisema watu wenye nia mbaya na Gwanda na taifa kwa ujumla walikuwa wakiendelea kufanya uovu wao hata kwa waandishi wa habari akiwemo Gwanda.[18][19] Mwigulu Nchemba, waziri wa mambo ya ndani Tanzania, aliahidi kuzungumza na wakuu wa idara ya polisi kuhusu Gwanda.[20]

IFEX, taasisi nyingine inayojihusisha na uhuru wa kujieleza, ilitoa tamko la kuwa na wasiwasi kwamba kupotea kwa Gwanda "kunaweza kuwakatisha tamaa" waandishi wengine wanaofuatilia uchunguzi kama huo.[21] Kampuni ya habari ambayo Gwanda ndo alipokuwa akifanya kazi, Mwananchi Communication Limited, pia iliomba kwamba mashirika ya aina hii pamoja na serikali ya Tanzania yazidishe utaftaji wa habari ya kutoweka kwa Gwanda.[22]

Mnamo Septemba 2018 Gwanda alipokea Tuzo ya Daudi Mwangosi kwa ujasiri katika uandishi wa habari kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania.[23]

Mnamo Novemba 2018 wawakilishi wawili wa Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari walikamatwa nchini Tanzania wakati wakisoma vitisho kwa waandishi wa habari nchini, pamoja na kupotea kwa Gwanda.[24]

Marejeo

hariri
  1. "Mwananchi marks two years since its journalist Azory Gwanda went". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  2. "Journalist reported missing in Tanzania". Associated Press (kwa American English). 2017-12-04. Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  3. Wahariri wawataka polisi wazidishe kasi kumtafuta Azory Gwanda (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2017-12-07, iliwekwa mnamo 2019-12-26
  4. <meta name="google-site-verification" content="HcOjUGLXTeJsnITjc-gp8XYHXCadkyqKwX4Z437I44c" /> (2017-12-18). "Tanzanian journalist Azory Gwanda goes missing for 28 days". Alleastafrica (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-26. Iliwekwa mnamo 2019-12-26. {{cite web}}: |author= has generic name (help)CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  5. "Tanzania: Concern grows for missing journalist Azory Gwanda". ARTICLE 19 (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  6. "Azory Gwanda". cpj.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  7. "Tanzania: Concern grows for missing journalist Azory Gwanda". ARTICLE 19 (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  8. Wahariri wawataka polisi wazidishe kasi kumtafuta Azory Gwanda (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2017-12-07, iliwekwa mnamo 2019-12-26
  9. "Tanzanian journalist missing after murder reports". News24 (kwa Kiingereza). 2017-12-05. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-26. Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  10. "Voices of concern intensify over whereabouts of missing journalist". www.ippmedia.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  11. "TZ journalist missing for two weeks". Daily Nation (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  12. B. T. Correspondent (2017-12-08). "Missing journalist was picked by white car". Business Today Kenya (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  13. "Disappearance of Azory: what we know so far". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  14. "Azory Gwanda". cpj.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  15. "Azory Gwanda". cpj.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  16. "EDITORIAL: AZORY GWANDA- A MONTH IS GONE, WE ARE STILL HOPING". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  17. MISA. "Azory Gwanda Archives". MISA (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-26. Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  18. https://allafrica.com/stories/201712180125.html
  19. "A year on and Azory Gwanda is still missing". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  20. "Tanzania govt hints on Azory disappearance". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  21. "Azori Gwanda disappearance "may discourage" investigative journalists". IFEX (kwa American English). 2017-12-15. Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  22. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-29. Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  23. "Missing journalist wins Sh10 million Mwangosi award". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  24. "One year after disappearance, CPJ calls for credible investigation into Tanzanian journalist Azory Gwanda's fate". cpj.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-26.