Mkoa wa Kigoma

Mkoa wa Tanzania


Mkoa wa Kigoma uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mkoa wa Kigoma
Mahali paMkoa wa Kigoma
Mahali paMkoa wa Kigoma
Mahali pa Mkoa wa Kigoma katika Tanzania
Majiranukta: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E / -4.883; 29.667
Nchi Tanzania
Wilaya 8
Makao makuu Kigoma Ujiji
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga
Eneo
 - Jumla 46,066 km²
 - Kavu 37,037 km² 
 - Maji 8,029 km² 
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 2,470,967
Tovuti:  kigoma.go.tz

Jiografia Edit

Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu.

Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu.

Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750.

Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa Kigoma ni Malagarasi, Luiche, Ruchugi na Rugufu.

Hifadhi za wanyama na za kihistoria Edit

 
Sokwe wa hifadhi ya Gombe
 
Sokwe wa Milima ya Mahale

Kuna maeneo mawili yenye sokwe: ndipo Hifadhi ya Taifa ya Gombe (alikofanya utafiti wake mwanabiolojia Jane Goddall) na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale. Pia kuna Pori la Akiba la Moyowosi ambalo makao yake makuu yapo katika kijiji cha Kifura, Wilaya ya Kibondo.

Utawala Edit

 
Mkutano wa Stanley na Livingstone huko Ujiji.

Kuna wilaya nane ambazo ni (idadi ya wakazi katika mabano): Kigoma Mjini (144,852), Kigoma Vijijini (490,816), Kibondo (414,764), Kasulu (628,677), Uvinza (383,640), Buhigwe (254,342) na Kakonko (167,555) . Jumla ya wakazi ni 2.127.930 (sensa ya mwaka 2012).

Makao makuu ya mkoa ni Kigoma mjini.

Mji wa Ujiji ulioko karibu na Kigoma mjini ndio mji wa kale zaidi katika Tanzania ya Magharibi penye makumbusho ya David Livingstone.

Wilaya au manisipaa Eneo km² Wakazi[1] Kata
1 Buhigwe 9,324 254,342 15
2 Kakonko 9,324 167,555 11
3 Kasulu Mjini 2,128 208,244 9
4 Kasulu Vijijini 7,196 425,794 19
5 Kibondo 16,058 261,331 13
6 Kigoma - Ujiji 93 215,458 19
7 Kigoma Vijijini 968 211,566 11
8 Uvinza 9,324 383,640 14
Jumla 45,066 2.127.930 121

Mnamo Machi 2012 zimeongezwa wilaya mpya za Buhigwe, Kakonko na Uvinza.

Wakazi Edit

Kadiri ya sensa ya mwaka 2022 wakazi walikuwa 2,470,967[2].

Kabila kubwa ni Waha, likifuatwa na Wamanyema, Wabembe na Watongwe. Kuna pia Wavinza, Wanyamwezi, Wasukuma, Wafipa na watu wenye asili ya Kongo, Rwanda na Burundi.

Idadi au msongamano wa watu katika maeneo ya mkoa huu imetegemea sana shughuli zinazofanyika kama vile kilimo na uvuvi pamoja na kupatikana kwa nzi aina ya ndorobo: penye ndorobo wengi huwa na watu wachache.

Uchumi na mawasiliano Edit

Mkoa wa Kigoma bado hauna maendeleo yanayolingana na mazingira yake. Hali ya barabara na mawasiliano mengine ni mbaya. Umbali hadi Dar es Salaam ni km 1316, hadi Mwanza 830, hadi Arusha 1204. Ipo barabara nzuri ya lami kuanzia wilaya ya Kaliua (mkoa wa Tabora) kupitia Uvinza, Malagarasi, Nguruka, Kaziramimba hadi Kigoma mjini, isipokuwa kipande cha kilomita 400 ni cha muramu ambayo nayo inapitika vizuri kama si kipindi cha mvua nyingi za uharibifu.

Usafiri muhimu ni reli kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupitia Tabora na Dodoma. Isipokuwa reli hii imeshazeeka kutokana na kujengwa zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Treni (gari moshi) zake huchelewachelewa kwa kuchukua muda mrefu. Wakati wa mvua inatokea ya kwamba mawasiliano yanavurugika.

Uwanja wa ndege wa Kigoma unashughulika na shirika la ndege la Tanzania lenye ndege nne zinazofanya safari kwa sasa nchi nzima na usafiri ni wa uhakika, pia yapo mashirika madogo yanyofanya shughuli zake kama auric air, nyingi zikiwa za kubeba watalii.Shukrani za kipekee zimwendee Rais wa nne(Mh Jakaya Mrisho Kikwete) wa Jamhuri ya Muungano aliepigana kiume kuufungua mkoa wa kigoma kwa njia ya mawasiliano ya barabara.

Takribani 85% ya wakazi wote hutegema kilimo, walio wengi kilimo cha kujitegemea tu, tena cha jembe la mkono.

Kuongezeka kwa wakimbizi kutoka nchi jirani na kukua kwa makambi kulikuwa tatizo kubwa.

Majimbo ya bunge Edit

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia Edit

Marejeo Edit

  1. kufuatana na sensa ya mwaka 2012 Sensa ya 2012, Kigoma Region
  2. https://assengaonline.com/2022/11/05/matokeo-ya-sensa-2022-tanzania/

Viungo vya nje Edit