Kwando
Kwando (au: Cuando; kabla ya mdomo pia Linyanti halafu Chobe) ni mto wa Afrika ya Kusini na tawimto la Zambezi. Chanzo chake kiko nyanda za juu za Bié (Angola) inapoelekea kusini-mashariki. Inakuwa mpaka kati ya Angola na Zambia kwa km 140, halafu inapita Kishoroba cha Caprivi na kuwa mpaka kati ya Namibia na Botswana.
Chanzo | Nyanda za juu za Bié (Angola) |
Mdomo | Mto Zambezi kwa mji wa Kazungula (Zambia) |
Nchi | Angola, Zambia, Namibia, Botswana |
Urefu | km 1,500 |
Kimo cha chanzo | m 1,700 hivi |
Mkondo | ?? |
Eneo la beseni | km² 96,778 |
Inaingia katika mabwawa wa Linyanti yenye km² 1,425. Katika sehemu hizo mto huitwa Chobe au Liyanti.
Kwa jina la Chobe unaingia katika mto Zambezi kwenye mji wa Kazungula pale ambapo nchi nne za Botswana, Namibia, Zambia na Zimbabwe zinapokutana.
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kwando kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |