Zambezi (mto)
Zambezi ni kati ya mito mirefu ya Afrika ikishika nafasi ya nne baada ya Nile, Kongo na Niger. Ni mto mrefu wa Afrika wa kuingia Bahari Hindi.
Mto wa Zambezi | |
---|---|
| |
Chanzo | karibu na Mwinilunga, Zambia |
Mdomo | Bahari ya Hindi |
Nchi za beseni ya mto | Zambia, Kongo, Angola, Namibia, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji |
Urefu | km 2,574 |
Kimo cha chanzo | m 1,500 |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | m³/s 7,000 |
Eneo la beseni (km²) | km² 1,570,000 |
Beseni lake lina km² 1,570,000 au nusu ya mto Nile. Chanzo chake kiko Zambia, halafu mto unapita Angola mpakani na Namibia, Botswana, Zambia na Zimbabwe kwenda Msumbiji inapofikia Bahari Hindi katika delta ya km² 880.
Kwenye mwendo wa Zambezi pana maporomoko kadhaa hasa maporomoko ya Victoria Falls. Mengine ni maporomoko ya Chavuma mpakani mwa Zambia na Angola, halafu Ngonye Falls karibu na Sioma, Zambia ya magharibi.
Zambezi ina madaraja matano pekee kati ya chanzo na mdomo mahali pafuatapo: Chinyingi, Katima Mulilo, Victoria Falls, Chirundu na Tete.
Zambezi ni chanzo cha umeme kwa ajili ya sehemu kubwa ya Afrika ya Kusini. Umeme unatengenezwa kwa nishati ya maji huko lambo la Kariba (Zambia) na lambo la Cabora-Bassa (Msumbiji).
Matawimto
haririMiji muhimu mtoni
hariri- Mongu
- Lukulu
- Katima Mulilo (Namibia), Sesheke (Zambia)
- Livingstone (Zambia), Victoria Falls (mji) (Zimbabwe)
- Kariba
- Songo
- Tete
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Watersheds of Africa: A20 Zambezi Ilihifadhiwa 12 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Zambezi (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |