Luxemburg

nchi katika Ulaya Magharibi

Luxemburg (pia: Lasembagi) ni nchi ndogo katika Ulaya. Imepakana na Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani.

Luxemburg


Ramani ya Luxemburg.

Ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya, tena ilikuwa kati ya nchi sita zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya mwaka 1957.

Historia hariri

Luxemburg kama nchi ndogo ilikuwa mara nyingi chini ya athira ya majirani wakubwa waliotawala juu yake kwa vipindi mbalimbali.

Kwa vipindi vingi vya historia yake Luxemburg ilikuwa sehemu ya Ujerumani.

Katika karne ya 14 watemi wa Luxemburg walichaguliwa kuwa wafalme wa Ujerumani.

Baada ya vita za Napoleoni, Ufaransa na Prussia zilivutana juu ya Luxemburg. Walipatana kwenye Mkutano wa Vienna (1815) ya kurudisha Luxemburg kama nchi ya pekee itakayotawaliwa na Mtemi Mkubwa. Mfalme wa Uholanzi alikuwa mtemi wa Luxemburg na nchi yenyewe iliungwa katika Shirikisho la Ujerumani.

Baada ya mwisho wa Shirikisho la Ujerumani (1866) Luxemburg haikujiunga (1870) na Dola jipya la Ujerumani.

Badiliko la familia ya kifalme katika Uholanzi lilisababisha uchaguzi wa mtemi wa pekee (1890).

Watu hariri

Ina wakazi 613,894 (Januari 2019) katika eneo la km² 2,586 pekee. Kati yao 49.1% ni wahamiaji kutoka Ureno (18.2% za wakazi wote), Ufaransa (13.5%), Ujerumani (10.3%), Italia (3.4%), Ubelgiji (3.3%), na nchi nyingine.

Lugha ya taifa ni Kiluxemburg ambayo ni lahaja ya Kijerumani yenye athira nyingi za Kifaransa. Karibu wakazi wote huweza kuongea lugha hizo zote tatu na Kiingereza, lakini zaidi Kifaransa.

Upande wa dini, 68.7% wanajitambulisha kama Wakatoliki na 3.7% wanajitambulisha kama Wakristo wa madhehebu mengine. Waislamu ni 2.3%. Wasio na dini ni 26.8%.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Umoja wa Ulaya  
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Luxemburg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.