LaShawn Merritt
LaShawn Merritt (amezaliwa 27 Juni 1986) ni mwanariadha wa Marekani wa mbio fupi ambaye huwa ni mtaalamu wa mbio za 400m.
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
LaShawn Merritt baada ya mbio za Osaka,Ujapani | ||
Riadha ya Wanaume | ||
Anawakilisha nchi Marekani | ||
Michezo ya Olimpiki | ||
Dhahabu | 2008 Beijing | 400 m |
Dhahabu | 2008 Beijing | 4x400 m |
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF | ||
Dhahabu | 2007 Osaka | 4x400 m |
Dhahabu | 2009 Berlin | 400 m |
Dhahabu | 2009 Berlin | 4x400m |
Fedha | 2007 Osaka | 400 m |
Merritt ni raia wa 12 ambapo alisoma katika shule ya upili ya Woodrow Wilson.
Wasifu
haririLaShawn alikimbia mwaka mmoja kama mwanariadha wa Chuo Kikuu cha Carolina Mashariki,akatia saini mkataba na kampuni ya Nike katika msimu wake wa kwanza katika mbio za ndani ya ukumbi,hii ikamfanya asiweze kushindana katika mashindano yoyote ya NCAA. Hivi sasa amejiunga na Chuo Kikuu cha Norfolk katika Norfolk,Virginia.
Wasifu wa riadha
haririMerritt alipata umaarufu kama mwanariadha wa daraja la chini katika Mashindano ya daraja la chini ya Mabingwa katika riadha ya 2004. Yeye alishinda medali ya dhahabu katika mbio ya 400m na akavunja rekodi mbili za dunia za daraja la chini akiwa mmojawapo katika timu ya Marekani ya 4 x 100m na 4 x 400m.
Merritt alishinda medali ya fedha katika mbio ya 400m katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2007 mjini Osaka. Alishinda medali yake ya dhahabu ya kwanza katika mashindano makubwa akiwa katika timu ya 4 x 400m katika mbio hizo za Osaka.
Meritt alishinda mbio ya 400m katika Olimpiki ya 2008 mjini Beijing. Mashindano makali kati ya Meritt na Jeremy Wariner yalitarajiwa lakini mbio hiyo ilishindwa na Merritt kwa umbali mrefu sana. Sekunde 0.99 kati ya Merritt na Wariner ilikuwa kubwa kabisa kati ya mshindi na mwanariadha wa nafasi ya pili katika fainali ya Olimpiki katika mbio ya 400m. Muda wake wa 43.75s ulimfanya mwanariadha wa kasi sana wa tano katika historia ya mbio ya 400m.
Alishinda mbio ya 400m katika Mashindano ya Mabingwa wa Marekani ya 2009,akikimbia muda bora wa sekunde 44.50. Katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2009,jijini Berlin,Merritt alienda na akashinda mbio ya 400m katika muda bora duniani wa 44.06s,akimshinda Wariner tena.
Mafanikio
haririMwaka | Shindano | Pahali pa kushindana | Matokeo | Mbio |
---|---|---|---|---|
2004 | Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Vijana ya 2004 | Grosseto, Uitalia | 1 | 400 m |
1 | 4x100 m | |||
1 | 4x400 m | |||
2006 | Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF ya Ndani ya Ukumbi ya 2006 | Moscow, Urusi | 1 | 4x400 m |
World Athletics Final | Stuttgart, Ujerumani | 3 | 400 m | |
Mashindano ya Kombe la Dunia ya 2006 ya IAAF | Athens, Ugiriki | 1 | 400 m | |
1 | 4x400 m | |||
2007 | Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha ya 2007 | Osaka, Ujapani | 2 | 400 m, PB 43.96 |
Mashindano ya Dunia ya Riadha ya IAAF ya 2007 | Stuttgart, Ujerumani | 1 | 400 m | |
2008 | Olimpiki ya 2008 | Beijing, Uchina | 1 | 400 m, 43.75 |
Olimpiki ya 2008 | Beijing, Uchina | 1 | 4x400 m | |
2009 | Mashindano ya Mabingwa wa Dunia Katika Riadha ya IAAF ya 2009 | Berlin, Ujerumani | 1 | 400 m, 44.06 |
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia Katika Riadha ya IAAF ya 2009 | Berlin, Ujerumani | 1 | 4x400 m |
Muda bora wa kibinafsi - Mbio za nje
hariri- Mbio ya mita 200 - 19.98 s (2007)
- Mbio ya mita 300 - 31.30 s (2009)
- Mbio ya mita 400 - 43.75 s (2008)
Muda bora wa kibinafsi - Mbio za ndani ya ukumbi
hariri- Mbio ya mita 60 - 6.68 s (2006)
- Mbio ya mita 200 - 20.40 s (2005)
- Mbio ya mita 300 - 31.94 s (2006)
- Mbio ya mita 400 - 44.93 s (2005)
- Mbio ya mita 500 - 1:03.38 (2006)
Marejeo
hariri- ^ http://www.usatf.org/athletes/bios/Merritt_LaShawn.asp Ilihifadhiwa 12 Februari 2010 kwenye Wayback Machine. LaShawn Merritt
- ^ Grosseto - Three World Junior records set in the space of 90 minutes. IAAF (2004-07-18).
- ^ Forde, Pat (2008-08-08), Hold on to your medals ... The Dash is checking in from Beijing, ESPN, ,
- ^ Hersh, Philip (2008-08-21), In the men's 400 meters, LaShawn Merritt's a fast learner, Los Angeles Times, ,
- ^ IAAF International Association of Athletics Federations - IAAF.org - Statistics - Top Lists
- ^ "400 Metres - M Final". Ilihifadhiwa 16 Agosti 2012 kwenye Wayback Machine. 21 Agosti 2009.
- ^ Grohmann, Karolos (2009-08-21), Merritt crushes Wariner again for 400m title, Ilihifadhiwa 7 Machi 2016 kwenye Wayback Machine. Reuters,
Viungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi ya LaShawn Merritt Ilihifadhiwa 18 Januari 2021 kwenye Wayback Machine.
- IAAF wasifu wa LaShawn Merritt