Ziwa Vostok
77°30′S 106°00′E / 77.500°S 106.000°E
| |
Nchi zinazopakana | Antaktiki |
Eneo la maji | km2 12,500 |
Kina cha chini | mita 432 |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
,ita -500 |
Ziwa Vostok ni ziwa lililopo kwenye Bara la Antaktiki chini ya ngao ya barafu. Ni moja kati ya maziwa 400 yaliyotambuliwa chini ya barafu ya Antaktiki; ni ziwa kubwa la bara hilo.
Ni ziwa lenye maji ya kumiminika yaliyo mita 4000 chini ya uso wa barafu ya Antaktiki.
Jina lake limetokana na Kituo cha Vostok cha Urusi kilichopo kwenye uso wa barafu juu yake.
Kuwepo kwa ziwa hilo liligunduliwa na wanasayansi wa Urusi na Uingereza waliotumia mitambo ya rada.
Ziwa lina maji safi. Jotoridi ya maji ni karibu -3 °C lakini hayagandi, hubaki kiowevu kwa sababu ya shinikizo kubwa la barafu juu yake.
Uhai
haririHakuna uthibitisho bado kama huna uhai wowote katika maji ya ziwa hili. Sehemu hii haikuwa na uhusiano na nje kwa miaka milioni kadhaa kwa sababu imefungwa chini ya ngao ya barafu ya Antaktiki. Wanasayansi walitoboa barafu hadi uso wa ziwa mara 3 wakakuta baadaye bakteria katika sampuli za maji lakini imegunduliwa baadaye kwamba bakteria wote ni machafuko yaliyoingizwa na vifaa vya kutobolea barafu. Enzymes ya kinga.
Mazingira katika ziwa yanaaminiwa kufanana na yale ya mwezi Europa wa Mshtarii (Jupiter) au mwezi Enceladus wa Zohali. Kupata uhai katika ziwa hilo kungeongeza uwezekano wa kukuta uhai umekuwepo katika moja ya miezi hiyo. [1]
Marejeo
hariri- ↑ "Mystery of Antarctica's 15-million year-old lake". The Daily Galaxy. 2007-12-04. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-16. Iliwekwa mnamo 2009-07-01.
Tovuti za Nje
hariri- Mailiya Chini ya barafu ya Antarctic, Maisha ya Ziwa La Maji Meupe la Bahari ya Maji . Robert Lee Hotz, Los Angeles Times .
- Columbia.edu: About Lake Vostok
- Columbia.edu: "Lake Vostok: A Curiosity or a Focus for Interdisciplinary Study?" Ilihifadhiwa 27 Aprili 2020 kwenye Wayback Machine. (1998)
- ASOC.org: Lake Vostok Letter of Appeal to Russia Ilihifadhiwa 4 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
- OperationReality.org: video documentary about Lake Vostok
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|