Lango:Afrika/Wasifu uliochaguliwa

Wasifu Uliochaguliwa

hariri

Wasifu Uliochaguliwa kwa Desemba 2012

hariri
 
Olusegun Obasanjo Rais wa Nigeria 1999 - 2007

Matthew Olusegun Aremu Obasanjo (* 5 Machi, 1937) ni jenerali mstaafu wa Jeshi la Nigeria aliyekuwa rais wa Nigeria mara mbili. Awamu lake la kwanza lilikuwa kama rais wa kijeshi kati ya 1976 hadi 1979 halafu awamu la pili kama rais aliyechaguliwa na wananchi kati ya 1999 hadi 2007. Obasanjo alizaliwa katika kabila la Wayoruba akalelewa kama Mkristo wa kibaptisti. 1958 akajiunga na jeshi akapanda ngazi haraka. 1967-1970 alishiriki katika vita dhidi ya Biafra.