Idris I (kwa Kiarabu: إدريس الأول idris-al-auwwal) (12 Machi 1890 - 25 Mei 1983) alikuwa mfalme wa kwanza na wa mwisho wa Libya kati ya miaka 1951 na 1969.

Idris I wa Libya

Jina lake la kiraia lilikuwa Muhamad Idris bin as-Sayyid ibn Muhamad as-Senussi (kwa Kiarabu: محمد إدريس بن السيد المهدي ابن محمد السنوسي ). Alikuwa mjukuu wa Muhamad ibn Ali as-Senussi aliyeanzisha jumuiya ya Wasufi wa Senussi. Muhamad alirithi cheo cha babu yake. Alikubaliwa kama Emir wa Cyrenaika na Uingereza na Italia baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Italia kuvamia Libya (1911) aliongoza vita vya porini.

Tangu mwaka 1951 aliongoza taifa jipya la Libya. Mwaka 1969 alipinduliwa na wanajeshi chini ya uongozi wa Muammar al-Gaddafi. Alikufa Misri uhamishoni mwaka 1983.

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Idris I wa Libya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.