Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia

hariri  fuatilia  

Lango la Afrika

Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika.

Neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Roma ya Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile. Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini kwa Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).

hariri  fuatilia  

Nchi za Afrika

hariri  fuatilia  

Jamii

hariri  fuatilia  

Wasifu Uliochaguliwa

Robert Mugabe (2009)

Robert Gabriel Mugabe (* 21 Februari 1924) amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza nchini waliofuata siasa ya ubaguzi wa rangi. Mugabe alirudiwa katika uchaguzi mbalimbali. Tangu mwaka 2000 uchaguzi hizi zimekuwa mashakani kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani. Utawala wa Mugabe umeitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002. Kutokana na mashataka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharau haki za binadamu nchi Zimbabwe ilisimamishwa ndani ya Jumuiya ya Madola.


hariri  fuatilia  

Makala iliyochaguliwa

Faili:Askari.jpeg
Askari wa jeshi la kijerumani
Kampeni za Afrika ya Mashariki ulikuwa mfululizo wa mapigano ya kivita yaliyotokea Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (Tanganyika, Rwanda na Burundi ya leo) na koloni jirani za Msumbiji, Rhodesia ya Kaskazini (Zambia), Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (Kenya), Uganda, na Kongo ya Kibelgiji. Kampeni hizi zilianza mwezi wa Agosti 1914 zikaisha rasmi mnamo mwezi wa Novemba katika mwaka wa 1918. Wapiganaji katika vita hii walikuwa jeshi la kikoloni cha Kijerumani lililofanywa hasa na askari Waafrika waliosimamiwa na maafisa Wajerumani pamoja na walowezi Wajerumani na wanamaji wa manowari waliokaa Afrika ya Mashariki wakati wa mwanzo wa vita 1914. Dhidi yao walisimama jeshi dogo la kikoloni la Kiingereza katika Kenya na Rhodesia, halafu vikosi vya jeshi la kikoloni la Uhindi ya Kiingereza na vikosi kutoka Afrika Kusini.


hariri  fuatilia  

Picha Iliyochaguliwa


Apalis flavida kutoka Abuko, Gambia.
(kupata bango)


hariri  fuatilia  

Je, wajua...?

......kwamba Hifadhi ya Arusha inapatikana katika mji wa Arusha nchini Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 542, iko umbali wa kilometa 32 kutoka katika mji wa kitalii wa Arusha.

hariri  fuatilia  

Masharika ya Wikimedia