Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia

Lango la Historia

Historia ni somo kuhusu maisha ya binadamu na utamaduni wao wa wakati uliopita. Mara nyingi neno historia pia lina maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu (kwa mfano "historia ya ulimwengu").

Wanahistoria wanapata maarifa zao kutoka maandishi ya zamani (hasa kwa Historia andishi), kutoka fasihi simulizi na kutoka akiolojia (hasa kwa Historia ya awali).

Makala nzuri ya mwezi

Alama ya SS zilikuwa S mbili kwa mwandiko wa Kigermanik
Alama ya SS zilikuwa S mbili kwa mwandiko wa Kigermanik

Schutzstaffel (Kikosi cha ulinzi) -kwa kifupi SS- ilikuwa jina la kitengo cha Chama cha Nazi au NSDAP nchini Ujerumani kilichoanzishwa mwaka 1925kama kundi la walinzi wa kiongozi wa chama cha Adolf Hitler. SS ilishiriki katika maangamizi makuu dhidi ya Wayahudi wa Ulaya na kutawala makambi ya mauti. Kutoka kundi dogo la walinzi wa binafsi iliendelea kuwa tawi la kijeshi la Chama cha Nazi lililoshiriki pia kwenye mapigano ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Ikapigwa marufuku kama chama cha kihaini mwaka 1945.

SS iliundwa kama kitengo cha wanamgambo wa NSDAP waliojulikana kama SA. Awali kazi ya wanamgambo 8 walioteuliwa ilikuwa kumlinda kiongozi wa chama cha Adolf Hitler kwenye maandamano na mikutano ya chama. Tangu 1929 iliongozwa na Heinrich Himmler. Wakati ule kikosi kilikuwa na wanachama 280. Himmler aliendelea kupanusha kikosi. Hadi mwisho wa 1929 alikuwa wanamgambo 1,000 chini yake waliongezeka kuwa 52,000 mwaka 1932.

Je, wajua...?

Je wajua ya kwamba mkoa wa Pwani pekee kuandikwa kiswahili na kingereza.(coast na pwani)

Vitu unavyoweza kufanya

WikiProjects

Masharika ya Wikimedia

Purge server cache