Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia

Lango la Sanaa

Sanaa ni usanii wowote, yaani utendaji wa binafsi au wa pamoja ambao, kwa kutumia vipaji vya kuzaliwa navyo au mbinu zinazotokana na mang'amuzi na masomo, unabuni na kuleta uzuri. Sanaa imegawanyika sehemu nyingi: k.mf. muziki, uigizaji, uchezaji, uchoraji, upigaji picha, sinema, ushonaji, uhariri, uchongaji, uandishi, ushairi.

Makala iliyochaguliwa

Mozaiki ya maua ya Ugiriki ya Kale, katika Uturuki ya leo

Mozaiki (au mosaiki) ni mtindo wa pekee wa uchoraji picha unaotumia vipande vidogo vya kioo cha rangi au vigae vya rangi mbalimbali vinavyounganishwa kuwa picha. Kunawezekana pia kutumia vipande vya vitu vyovyote vyenye rangi vinavyoweza kuunganishwa kuwa picha.

Mtindo huu ulionekana mara ya kwanza huko Phrygia (katika Uturuki ya leo) iliyokuwa sehemu ya ustaarabu wa Ugiriki ya Kale. Mawe ya rangi nyeupe na nyeusi yalipangwa ukutani au kwneye sakafu kuwa tarakibu. Baadaye Wagiriki na zaidi Waroma waliendelea kuongeza rangi na kutunga picha kamili si tarakibu tu kwenye kuta za nyumba. Maghofu ya Kiroma yanaonyesha mifano mingi iliyodumu hadi leo.

Sanaa ya mozaiki iliendelezwa katika ustaarabu wa Bizanti. Wabizanti walipamba makanisa, majumba ya kifalme na pia nyumba za matajiri kwa mozaiki nzuri kabisa.

Waarabu Waislamu walipotwaa shemu kubwa za milki ya Bizanti waliendelea kuwaajiri wasanii Wabizanti wakipamba misikiti kama msikiti wa Umawiya huko Dameski au majumba ya masultani.

Baadaye walikuwa mafundi Waislamu waliopamba makanisa na nyumba katika Italia ya kusini.

Wasifu Uliochaguliwa

Vasili Vereshchagin
Vasili Vereshchagin
Vasili Vasilyevich Vereshchagin (Kirusi: Василий Василиевич Верещагин 1842 - 1904) alikuwa mchoraji kutoka Urusi aliyefahamika sana kutokana picha zake za vita na mapigano.

Alikuwa mtoto wa mkulima aliyepata elimu kwenye shule ya kijeshi akandelea kuwa afisa wa jeshi la Urusi. Aliondoka jeshini akawa mwanafunzi wa uchoraji huko Sankt Peterburg akamaliza masomo yake kwenye Chuo cha Sanaa mjini Paris.

Kama afisa wa jeshi alipata nafasi ya kuongozana na jeshi la Kirusi kwenye kempeni zake katika Asia ya Kati. Aliona vita kali na mauaji mengi akaamua kuonyesha uharibifu wa vita kwa umakini kwa matumaini ya kwamba watu wangekataa vita baada ya kuona ubaya wake. Kwa hiyo alichora mara nyingi maiti, askari wajeruhiwa, uharibifu wa vijiji na mahospitali.

Je, wajua...?

Vitu unavyoweza kufanya

Masharika ya Wikimedia