Tiva
(Elekezwa kutoka Laniarius)
Tiva ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Laniarius katika familia Malaconotidae. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Spishi nyingine ni nyeusi na nyeupe lakini nyingine zina rangi kali chini na pengine kwa utosi, kama nyekundu, machungwa na njano. Tiva wana domo nene lenye ncha kwa kulabu na mkia wao ni mrefu kiasi. Hula wadudu na vertebrata wadogo. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini au kichakani na jike huyataga mayai 2-3.
Spishi
hariri- Laniarius aethiopicus
- Laniarius a. aethiopicus, Tiva Habeshi (Ethiopian Boubou)
- Laniarius a. ambiguus, Tiva-milima (Highland Boubou)
- Laniarius amboimensis, Tiva wa Angola (Gabela Bushshrike)
- Laniarius atrococcineus, Tiva Kidari-chekundu (Crimson-breasted Gonolek)
- Laniarius atroflavus, Tiva Kidari-njano (Yellow-breasted Boubou)
- Laniarius barbarus, Tiva Utosi-njano (Yellow-crowned Gonolek)
- Laniarius bicolor, Tiva-kinamasi (Swamp Boubou)
- Laniarius brauni, Tiva Kidari-machungwa (Braun's Bushshrike au Orange-breasted Boubou)
- Laniarius erythrogaster, Tiva Tumbo-jekundu (Black-headed Gonolek)
- Laniarius ferrugineus, Tiva Kusi (Southern Boubou)
- Laniarius fuelleborni, Tiva wa Fülleborn (Fülleborn's Boubou)
- Laniarius funebris, Tiva Kijivucheusi (Slate-coloured Boubou)
- Laniarius leucorhynchus, Tiva Mweusi (Lowland Sooty Boubou)
- Laniarius luehderi, Tiva wa Lühder (Lühder's Bushshrike)
- Laniarius major, Tiva Magharibi (West African au Tropical Boubou)
- Laniarius mufumbiri, Tiva-mafunjo (Papyrus Gonolek)
- Laniarius nigerrimus, Tiva Somali (Black au Somali Boubou)
- Laniarius poensis, Tiva-milima Mweusi (Mountain Sooty Boubou)
- Laniarius ruficeps, Tiva Kisogo-chekundu (Red-naped Bushshrike)
- Laniarius sublacteus, Tiva-pwani (East Coast Boubou)
- Laniarius turatii, Tiva wa Turati (Turati's Boubou)
- Laniarius willardi, Tiva wa Willard (Willard's Sooty Boubou)
Picha
hariri-
Tiva kidari-chekundu
-
Tiva utosi-njano
-
Tiva kusi
-
Tiva kijivucheusi
-
Tiva wa Lühder
-
Tiva magharibi
-
Tiva-mafunjo