Leonardo
Leonard Datus Butindi (maarufu kama Leonardo, alizaliwa wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, 25 Januari 1998) ni mchekeshaji kutoka Tanzania ambaye alipata kujulikana kupitia maonesho yake kwenye jukwaa la Cheka Tu pamoja na video zake za mtandaoni.[1]
Leonardo alipata umaarufu mkubwa mwaka 2021 mara baada ya kushinda shindano la Cheka Tu Comedy Search lililoandaliwa na Cheka Tu pamoja na Wasafi TV [2]
Mwaka 2024, mtandao wa Notjustok kutokea nchini Nigeria ulimtaja Leonardo kuwa ni miongoni mwa mchekeshaji wenye ushawishi mkubwa zaidi Tanzania [3]
Maisha ya awali
haririMwaka 2007, akiwa na miaka 9, familia yake ilihamia mkoani Morogoro. [4]
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Kilakala, kisha akapata nafasi ya kujiunga na Morogoro Secondary School kwa masomo ya Sekondari na akamalizia elimu yake ya kidato cha tano na sita Galanosi High School [5]
Leonardo ni kati ya wachekeshaji wachache kutoka Tanzania wenye elimu kwani ana shahada ya Water Resources and Irrigation Engineering kutoka Tanzania Water Institute, maarufu kama Chuo Cha Maji.[6] [7]
Tangu akiwa mtoto, Leonardo alikuwa na kipaji cha ucheshi na kupenda sana utani. Yeye pamoja na familia yake waliishi Morogoro hadi alipohamia tena Dar es Salaam kwa ajili ya kujiunga na chuo.[8]
Kuingia kwenye sanaa
haririLeonardo aliingia rasmi kwenye sanaa ya uchekeshaji mwaka 2019 alipojiunga na kampuni ya Punchline Comedy Club chini ya Evans Bukuku. [9]
Mwaka 2021, aliibuka kidedea Cheka Tu Comedy Search na kushinda kitita cha milioni 10, hivyo kujiunga rasmi na Cheka Tu kama mchekeshaji wa kudumu. [10]
Watu waliomshawishi
haririLeonardo ameeleza kuwa mchekeshaji na muigizaji maarufu kutoka Marekani, Eddie Murphy, ni mmoja wa watu waliomshawishi kuingia kwenye sanaa ya uchekeshaji baada ya kutazama filamu au tamthilia ya Murphy iitwayo "Delirious" ya mwaka 1983.
Tanbihi
hariri- ↑ "Mambo Manne Usiyoyajua Kuhusu mchekeshaji Leonardo - Millard Ayo" (kwa American English). 2024-06-21. Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
- ↑ "Leonardo Biography: 5 Things You Should Know About The Tanzanian Comedy Heavyweight ⚜ Latest music news online". mdundo.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
- ↑ "The 10 most impactful online Tanzanian comedians in 2024". Latest East African & Bongo Flava Music, Songs & Video - Notjustok (kwa American English). 2024-06-02. Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
- ↑ "Leonardo kumbe ni rapper ? achana mistari aeleza alichoambiwa na Diamond – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
- ↑ Chalz Writes (2024-06-19). "How Tanzania's Leonardo Became 'Unknown' to 'Unstoppable'". Cityelevens (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-07-10. Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
- ↑ "Biography: Leonardo is the new Messi of Tanzanian comedy | Notjustok". Latest East African & Bongo Flava Music, Songs & Video - Notjustok (kwa American English). 2024-06-18. Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
- ↑ "Stand-up comedy and its special place among Dar revelers". The Citizen (kwa Kiingereza). 2020-10-22. Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
- ↑ "Leonardo atoboa Siri ya neno bila D mbili, asimulia alivyokutana na Diamond (Video) – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
- ↑ "Ukubwa wa Leonardo haukujengwa kwa siku moja | East Africa Television". www.eatv.tv (kwa Kiingereza). 2024-06-20. Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
- ↑ "Ukubwa wa Leonardo haukujengwa kwa siku moja | East Africa Television". www.eatv.tv (kwa Kiingereza). 2024-06-20. Iliwekwa mnamo 2024-07-10.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Leonardo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |