Leonidas Gama

Mwanasiasa Mtanzania
(Elekezwa kutoka Leonidas Tutubert Gama)

Leonidas Tutubert Gama (15 Septemba 1959 - 24 Novemba 2017) alikuwa mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni .

Alichaguliwa kuwa mbunge wa Songea Mjini kwa miaka 20152020. [1]

Leonidas Gama katika enzi za uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, mkuu wa wilaya za Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya mjini na Ilala katika nyakati tofauti. Aidha mheshimiwa Leonidas Gama aliwahi kuwa kiongozi wa mbio za mwenge Taifa mwaka 1991.

Sambamba na utumishi katika serikali, Gama alikuwa kada wa chama tawala na kushika nafasi mbalimbali za juu za uongozi katika ngazi ya chama hicho.

Marejeo hariri

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017