Leontine Nzeyimana

Mwanasiasa wa Burundi.


Leontine Nzeyimana, (alizaliwa 27 Desemba 1973) ni mwanasiasa wa Burundi ambaye amewahi kuwa Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika Ofisi ya Rais wa Burundi kuanzia tarehe 8 Mei 2012. Pia ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Burundi.[1] Kabla ya hapo, kuanzia Agosti mwaka 2011 hadi Mei mwaka 2012 alikuwa Mbunge mteule wa Jimbo la Makamba.[1]

Leontine Nzeyimana
Tarehe ya kuzaliwa 27 Desemba 1973
Kazi Mwanasiyasa

Maisha na Elimu

hariri

Leontine Nzeyimana alizaliwa katika wilaya ya Nyanza Lac katika Mkoa wa Makamba, kusini mwa Burundi. Alisoma shule ya msingi na sekondari za eneo hilo.[1]Alisoma katika Chuo Kikuu cha Tumaini kwenye kampasi yao iliyopo Iringa Mjini (sasa Chuo Kikuu cha Iringa) na alihitimu mwaka 2002 na kupata Shahada ya Utawala wa Biashara. Pia ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya Uhusiano wa Kimataifa aliyopata kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani mwaka wa 2005.[1]

Mnamo mwaka 2005, Léontine Nzeyimana alifanya kazi kama msaidizi wa Mshauri Mkuu wa "Mradi wa Utawala wa Sheria" wakati wa uundaji wa Burundi mpya. Kisha alifanya kazi katika Benki ya Burundi kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2007 kama msaidizi wa Gavana wa Benki Kuu ambapo majukumu yake yalijumuisha ratiba ya kila siku ya Gavana na kutafsiri hati kutoka Kifaransa kwenda Kiingereza na kutoka Kiingereza kwenda Kifaransa.[1]

Kisha alijiunga na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) akifanya kazi huko kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2010.Kazi yake ililenga kuboresha utendaji kazi wa mahakama ya Burundi.[1]Mbali na majukumu yake ya uwaziri nchini Burundi, Leontine Nzeyimana anahudumu kama mjumbe wa Bunge la nne la Afrika Mashariki kuanzia mwaka 2017 mpaka mwaka 2022.[2]

Majukumu Mengine

hariri

Kama mjumbe wa Bunge la Burundi aliwahi kuwa Katibu wa Kamati ya Kudumu inayoshughulikia Masuala ya Kisiasa, Utawala, Mambo ya Nje na Jumuiya ya Afrika Mashariki.[1]

Leontine anaripotiwa kuwa ana uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika lugha nne ambazo ni Kirundi, Kifaransa, Kiingereza na Kiswahili.[1]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-01. Iliwekwa mnamo 2022-04-02.
  2. "Nzeyimana, Léontine —East African Legislative Assembly". www.eala.org. Iliwekwa mnamo 2022-04-02.
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Leontine Nzeyimana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.