Lil Wayne
Dwayne Michael Carter, Jr. (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lil Wayne; amezaliwa 27 Septemba 1982) ni mshindi wa Tuzo za Grammy - akiwa kama rapa wa muziki wa hip hop bora kutoka nchini Marekani.
Lil Wayne | |
---|---|
Lil Wayne mnamo 2011
| |
Maelezo ya awali | |
Amezaliwa | 27 Septemba 1982 |
Asili yake | New Orleans, Louisiana, United States |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Rapa, Mwigizaji, CEO, Msanifu |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 1993–mpaka sasa |
Studio | Cash Money, Young Money, Universal |
Ame/Wameshirikiana na | Hot Boys, Birdman, T-Pain, Drake, Young Money, Kanye West, Young Jeezy, DJ Khaled, Mack Maine, Rick Ross |
Tovuti | www.lilwayne-online.com |
Alijiunga na studio ya Cash Money Records akiwa bado yungali bwana mdogo na akabahatika kufanya rekodi kadhaa katika studio hiyo. Wayne alikuwa mmoja kati ya waliokuwa wanachama wa kikundi cha muziki wa rap cha Hot Boys.
Waasifu
haririMaisha ya awali
haririAlizaliwa kama Dwayne Michael Carter, Jr. na kukulia mjini Hollygrove karibu kidogo na mji wa New Orleans, Louisiana. Akiwa na umri wa miaka kumi na moja, akakutana na Bryan Williams, rapa na ndiyo mmiliki wa studio ya Cash Money Records.
Baada ya makutano hayo, Wayne akarekodi rap flani ya michano katika studio hiyo ya Williams kwa kutumia chombo maalum cha kuweza kukujibu wakati unachana. Na kwa bahati nzuri michano hiyo ilimwacha hoi mmiliki huyo wa studio na kuthubutu hata kumwingiza Wayne katika studio yake.
Wayne pia ana mtoto wa kike mmoja aitwaye Reginae Carter, aliyezaliana na Antonia "Toya" Johnson, mpenzi wake wa kitambo toka shule. Wawili hao walikuja kuoana wakati wa Siku Kuu ya Wapendanao ya mwaka wa 2004, lakini walikuja kutalikiana mnamo mwaka wa 2006.
Muziki
haririAlbamu za Lil Wayne
hariri- 1999: Tha Block Is Hot
- 2000: Lights Out
- 2002: 500 Degreez
- 2004: Tha Carter
- 2005: Tha Carter II
- 2008: Tha Carter III
- EP albums
- 2007: The Leak
Filamu
haririMarejeo
hariri- ↑ [1] Ilihifadhiwa 28 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine. DefSounds.com
- ↑ Lil' Wayne
- ↑ [2] Ilihifadhiwa 2 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine. Fox Business
- ↑ [3] The Boombox
Viungo vya nje
hariri- Lil Wayne katika MySpace
- Lil Wayne at the Internet Movie Database
- Cash Money Records