Liloca
Luísa Zélia Sebastiana da Graça Madade anajulikana kama " Liloca " (alizaliwa 29 Aprili, 1985) ni mwimbaji wa Msumbiji .
Maisha
haririAlizaliwa Tete mnamo mwaka 1985. Wazazi wake walikuwa ni Sebastião Mabuze Madade na Natália Paulo Zimba. [1] Akiwa katika umri mdogo alipendezewa sana na densi.
Alisoma katika Shule ya Msingi ya SOS na ISCTEM - Instituto Superior de Ciências e Tecnologias de Moçambique ambapo alisomea sheria, lakini matarajio yake yalikuwa muziki. [2] Alianza kazi ya densi kwa kufanya kazi na mwimbaji wa Msumbiji "MC Roger". [1] Hatimaye alijitenga na kuunda kikundi chake cha densi kilichoitwa " Sweet Dance ". Wimbo wake wa kwanza uliotolewa ulikuwa " Como ela Dance " mnamo 2006 na kufuatiwa na ' ' Muyive '' . [1]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 Manusse, Jacinto G. (2016-04-09). "Biografia da Liloca". INFROMOZ Notícias de Moçambique, Emprego, Entretenimento (kwa Kireno (Ulaya)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-03. Iliwekwa mnamo 2020-02-07.
- ↑ "Coke Studio Africa - Artist - Liloca". www.coca-cola.co.ke (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-30. Iliwekwa mnamo 2020-02-07.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liloca kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |