Linah Kilimo

Mwanasiasa wa Kenya na mwenyekiti wa zamani wa Bodi ya Kupambana na Ukeketaji, Kenya

Linah Jebii Kilimo (alizaliwa mnamo 22 Oktoba 1963) ni Mbunge wa kike nchini Kenya aliyekuwa anahudumu katika serikali.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2002 alichaguliwa kuwakilisha eneo bunge la Marakwet Mashariki kwa tiketi ya NARC. Wapinzani wake wa kisiasa walikuwa wamepinga kukimbilia kwake kwa kiti cha ubunge kwani msingi wao ulikuwa kwamba Linah hakuwa amepashwa tohara na hivyo basi hakuwa katika hali mwafaka ya kukimbilia ofisi ya umma.

Hata hivyo amefanya kazi kwa ufanisi pamoja na mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya Kiserikali (NGO) huku lengo lao kuu likiwa kutokomeza ukeketaji. Pia amefanya kazi kwa ufanisi katika kuleta amani ya kudumu kati ya jamii ya Wapokot na jamii ya Wamarakwet. Jamii ya Wamarakwet na hasa wale wanaotoka katika eneo bunge ya Marakwet Mashariki walikuwa wamevamiwa na kuteswa vibaya sana na mashujaa wa Kipokot ambao walikuwa wezi wa kimabavu na ambao Serikali ya KANU ilikuwa imeshindwa kuwasimamisha licha ya kuwepo kwa Jeshi, Polisi na kijeshi cha polisi katika eneo hilo. Amani hii ilipatikana tu baada ya Serikali ya NARC kuchaguliwa mnamo Desemba mwaka wa 2002. Kama matokeo jamii hizi mbili sasa zinaishi kwa amani na utulivu.

Lina Kilimo pia amefanikiwa katika kuendeleza eneo bunge la Marakwet Mashariki, kwa kutoa ufadhili kwa shule za mitaa kwa njia ya vitabu, walimu zaidi, mipango ya chakula na hata nguo. Jebii amefanya kazi pamoja na Serikali kuboresha barabara ya kuingia katika eneo bunge hilo kupitia ujenzi wa barabara ya hali ya hewa zote ("all-weather road" kwa lugha ya kimombo) huku nia na lengo kuu likiwa kuweka lami katika barabara hiyo kwa muda usiyokuwa mrefu.

Linah ameolewa kwa mhandisi anayehudumu katika Serikali na walijaliwa kuwa na wana watano.

Katika kura ya maoni ya katiba ya Kenya ya mwaka wa 2005, aliunga mkono kupinga katiba hiyo. Pamoja na idadi ya mawaziri wengine, alikuwa mateke nje ya serikali baada ya kura ya maoni, ambayo imeshindwa kupitisha mapendekezo ya katiba pamoja na idadi ya mawaziri wengine, alifukuzwa kutoka serikalini baada ya kura ya maoni, ambayo ilishindwa kupitisha katiba mpya iliyopendekezwa.

Alijiunga na chama cha Orange Democratic Movement, lakini baadaye alikiondoka chama hicho ili kuunga mkono uchaguzi wa pili wa rais Mwai Kibaki. Hatimaye alikimbilia kiti cha eneo bunge lake kwa tikiti ya chama cha KENDA na kukihifadhi kiti chake cha ubunge.

Marejeo hariri