Linet Masai

Mwanariadha wa mbio ndefu kutoka Kenya

Linet Masai Chepkwemoi (alizaliwa mnamo 5 Desemba 1989 sehemu ya Kapsokwony, Wilaya ya Mlima Elgon) ni mkimbiaji wa masafa marefu kutoka Kenya na mshindi wa mbio za mita 10,000 katika mashindano ya dunia ya IAAF ya mwaka wa 2009 yaliyofanyika katika mji mkuu wa Berlin, Ujerumani.

Rekodi za medali

Linet Masai
Women's Wanariadha
Anawakilisha nchi Bendera ya Kenya Kenya
World Championships
Dhahabu 2009 Berlin 10000 m

Wasifu

hariri

Masai anatoka katika kijiji cha Bugaa, kilomita nne ukielekea katika mji wa Kapsokwonyi Wazazi wake ni John Barasa Masai na Leonida Cherop na ni mzaliwa wa nne wa jumla ya watoto kumi Alisomea shule ya Msingi ya Kapsagom na kisha skuli ya sekondari ya Askofu Okiring ambapo alihitimu mwaka wa 2005. Alianza kukimbia mwaka wa 2005, wakati kaka yake mkubwa, Musa Ndiema Masai, alishinda mbio za mita 5000 na 10000 katika mashindano ya vijana ya Kiafrika, akitumai angeweza kuiga mafanikio ya kakake. Ndugu zake wachanga, Dennis [8] Ndiema [9] na Magdaline pia ni wakimbiaji. Baba yao, John Barasa Masai, pia alikuwa mkimbiaji [11] huku Ben Jipcho akiwa mjomba wao wa mbali. Yeye hufanyia mazoezi katika kambi ya PACE Sports Management Training katika eneo la Kaptagat.

Wasifu

hariri

Alishinda mbio za wanawake wachanga katika mashindano ya IAAF World Cross Country ya mwaka wa 2007 iliyofanyika katika mji mkuu wa Mombasa, nchini Kenya. Alimaliza katika nafasi ya nne katika majaribio ya Kenya ya mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya mwaka wa 2007 katika mbio za mita 5000 na kukosa tiketi ya kushiriki katika mji mkuu wa Osaka. Hata hivyo, alishiriki katika mashindano ya IAAF World Athletics Final mwaka wa 2007, na kumaliza katika nafasi ya nne mara mbili (mbio za mita 3000 na 5000).

Mafanikio yake yalianza mwaka wa 2008. Katika msimu wa SPRING alishinda medali ya shaba katika mashindano ya World Cross Country ya mwaka wa 2008. Katika majira ya jua alishiriki katika Michezo ya Olimpiki na kumaliza katika nafasi ya nne katika mbio za mita 10,000 katika rekodi mpya ya vijana ya ulimwengu ya dakika 30:26.50. Rekodi ya zamani (30:31.55) ilikuwa inashikiliwa na Huina Xing wa Uchina na uliwekwa mwaka wa 2003. Pia ilikuwa rekodi mpya ya Kenya, rekodi ya hapo awali (30:30.26) ilikuwa inashikiliwa na Edith Masai na uliwekwa mwaka wa 2005. Rekodi ya Masai ya kitaifa ilisimama kwa muda usiozidi mwaka, kwani mnamo juni mwaka wa 2009 Florence Kiplagat alikimbia kwa muda wa dakika 30:11.53 mjini Utrecht, Uholanzi.

Mnamo 15 Agosti 2009, Masai alimshinda Meselech Melkamu wa Ethiopia NARROWLY katika fainali za mita 10,000 katika mashindano ya dunia ya IAAF ya mwaka wa 2009 iliyofanyika katika mji mkuu wa Berlin nchini Ujerumani. Bingwa wa wakati huo wa mbio za mita 10000 katika Michezo ya Olimpiki na Mashindano ya Dunia, Tirunesh Dibaba, alikuwa hakuweza kushiriki kutokana na jeraha. Alianza kuifanyia mazoezi mashinano ya Dunia ya Cross Country ya mwaka wa 2010 kwa kufanikiwa kupata ushindi katika mashindano ya Cross Internacional Valle de Llodio na Cross Internacional de Soria, kwa kuwashinda wakimbiaji wenzake kwa umbali mkubwa katika mashindano yote mawili. Masai alishinda tuzo la mwanaspoti wa kike bora wa Kenya wa mwaka wa 2009 [15] Pia alituzwa tuzo la Race Results Weekly la mkimbiaji wa kike wa mwaka, mwaka wa 2009

Majalio

hariri
Mwaka Mchuano Ukumbi Tokeo Ziada
2007 Mashindano ya dunia ya Cross Country Mombasa, Kenya 1 Mbio za Vijana
mbio za mwisho duniani Stuttgart, Ujerumani 4 mita 3000
4 mita 5000
2008 Mashindano ya dunia ya Cross Country Edinburgh,Scotland 3 Mbio za Mwandamizi
2 Ushindani wa Timu
Michezo ya Olimpiki Beijing, Uchina 4 mita 10,000
Fainali za mbio za dunia Stuttgart, Ujerumani 5 mita 3000
4 mita 5000
2009 Mashindano ya dunia ya Cross Country Amman,Jordan 2 Masafa marefu
1 Timu
Mbio za Mabingwa wa Dunia mwaka 2009 Berlin, Ujerumani 1 mita 10,000

Ubora wa kibinafsi

hariri
  • Mita 3000 - dakika 8:38.97 (2007)
  • Mita 5000 - dakika 14:34.36(2009)
  • Mita 10,000 - dakika 30:26.50(2008)
  • Kilomita 10 - dakika 31:30 (2009)

Viungo vya nje

hariri

Marejeo

hariri