Lola Pagnani
Lola Pagnani (amezaliwa 3 Aprili 1972) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Italia.
Lola Pagnani | |
---|---|
Amezaliwa | Anna Lola Pagnani Stravos 3 Aprili 1972 Roma, Italy |
Jina lingine | Lola Stravos Anna Lola Pagnani |
Miaka ya kazi | 1989 - hadi leo |
Tovuti rasmi |
Alizaliwa mjini Roma na jina la Anna Lola Pagnani Stavros, akiwa binti wa mtunzi na mwandishi wa muswada andishi Enzo Pagnani. Alihitimu elimu yake ya unenguaji mjini Paris akiwa na umri wa miaka 17, na akawa ndiyo mnenguaji wa kwanza wa Kampuni ya Momix wakati wa Matamasha ya Kimataifa ya kampuni, akafanya vyema kabisa huko mjini Montréal.
Alikuwa mnenguaji wa kwanza kucheza katika Jumba la Opera la mjini Munich akiwa chini ya uongozi wake Lina Wertmuller na mwelekezi Giuseppe Sinopoli. Baada ya hapo akaja kumalizia elimu yake hiyo ya kucheza katika chuo cha Alvin Ailey American Dance Theater cha mjini New York City, Marekani.
Baadaye alisomea masomo ya uigizaji katika studio ya HB, na pia New York. Halafu baadaye akarudi zake nchini Italia.
Alivyorudi Italia akaanza kushirikiana na waigizaji na waongozaji kadhaa makubwa-kubwa wa filamu. Kwa namna moja au nyingine alishirikiana na Ettore Scola, Giulio Base, Lina Wertmuller; na pia alicheza na Spike Lee na John Turturro na Abel Ferrara.
Pia alishawahi kufanya kazi kama mtangazaji wa kipindi cha Maurizio Costanzo Show. Akiwa hapo, aliweza kuhojiana na Enrico Montesano, Marco Columbro, Barbara De Rossi, Blas Roca Rey, Enrico Brignano, Nino Manfredi, Vittorio Gassman na Shelley Winters, ambaye baadaye alimchukua na kwenda kumpeleka katika shule ya uigizaji ya Los Angeles. Alipata masomo ya faragha na Bw. Teddey Sherman mjini Los Angeles.
Alishafanya kazi na Rai International ya mjini New York katika vipindi kadhaa na kutangaza katika kipindi cha PoP Italia. Mwanamama huyu anaweza kuongea lugha kadhaa kifasaha kabisa. Lugha hizo ni pamoja na Kiitalia, Kifaransa, Kihispania na Kiingereza.
Sanaa
haririFilamu
hariri- Trafitti da un raggio di sole (1995) - Fabiola
- Polvere di Napoli (1996) - Rosita
- Ninfa plebea (1996) - Lucia
- Ferdinando e Carolina (1999) - Sara Goudar
- La bomba (1999) - Daisy
- Il pranzo della domenica (2002)
- Gente di Roma (2003)
- Women Seeking Justice (2007)
Televisheni
hariri- Pazza famiglia (1995)
- Commissario Raimondi (1998) - Esmeralda
- Anni 50 (1998)
- La squadra (2000)
- Un posto al sole (2001) - Roberta Cantone
- Francesca e Nunziata (2001)
- Carabinieri 5 (2005)
- Un ciclone in famiglia 2 (2005)
- Donne sbagliate (2006)
- Capri (2006) - Maria Rosaria
Sanaa ya ukumbini
hariri- Vergine Regina (1996)
- Anatra all'arancia (1997)
- Carmen (1987)
Viungo vya nje
hariri- Lola Pagnani kwenye Internet Movie Database
- Tovuti Rasmi ya Lola Pagnani Archived 24 Julai 2008 at the Wayback Machine.
- Studio Morea-Lo Cascio, Lola's Press in Rome Archived 5 Desemba 2008 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lola Pagnani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |