Louise Carver (mwimbaji wa Afrika Kusini)

mwandishi na mpiga kinanda kutoka Afrika kusini

Louise Carver (alizaliwa 10 Januari 1979) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za rock na mpiga kinanda wa nchini Afrika Kusini.

Louise Carver
Louise Carver

Carver alizaliwa Cape Town, na ana uraia wa nchi mbili nchini Afrika Kusini na Uingereza. Alianza kupiga piano akiwa na umri wa miaka 11, na alipokea kandarasi yake ya kwanza ya kurekodi akiwa na umri wa miaka 15. Alifuzu katika shule ya wasichana ya Rustenburg, mwaka 1996. Alipata shahada ya heshima katika siasa, falsafa na uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town mnamo 2002.

Muziki

hariri

Carver alitoa wimbo wake wa kwanza, It Don't Matter (1996) alipokuwa na umri wa miaka 17. Wimbo huo uliongoza kwenye Chati za kampasi ya Kitaifa ya Afrika Kusini. Ilitumia wiki 11 kwenye chati bora ya nyimbo za Afrika Kusini, ambapo ilishika nafasi ya tatu.  Akiwa na umri wa miaka 18 alifuatisha nyimbo kadhaa na albamu yake ya kwanza, Mirrors na Windows (1998). [1]

Albamu za studio

hariri
  • Mirrors and Windows (1998)
  • Looking Around (2002)
  • Silent Scream (2005)
  • Saved by the Moonlight (2007)
  • Look to the Edge (2010)
  • Say It to My Face (2013)
  • Hanging in the Void (2016)

Marejeo

hariri
  1. "Louise Carver," Who's Who Southern Africa. Found at Who's Who SA. Accessed 29 September 2010.
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Louise Carver (mwimbaji wa Afrika Kusini) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.