Kigusii
Kigusii ni lugha ya Kibantu nchini Kenya inayozungumzwa na Wakisii. Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kigusii imehesabiwa kuwa watu 2,205,000. Pia kuna wasemaji 300 tu nchini Tanzania. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kigusii iko katika kundi la E40. Hasa Kigusii huzungumzwa eneo la Kisii ambalo makao yake makuu ni Mji wa Kisii (kati ya Ziwa Victoria na mpaka wa Kenya-Tanzania) katika Mkoa wa Nyanza.
Ainisho
haririKigusii imeainishwa kama lugha ya Bantu ya Kati, kundi moja na Lugha ya Kikuria, kundi ambalo limepewa anwani ya E.10 katika makala ya Aina za Lugha za Bantu yaliyotungwa na Malcolm Guthrie. Lugha zinazofanana zinapatikana nchini Tanzania nazo ni:
Sauti
haririSauti za Gusii takribani zote zinaambatana na irabu.
Irabu
haririLugha ya Kisii ina irabu saba, zingine zikiundwa kutokana na urefu wa kuzitamka. Kwa mfano, maneno 'bora' (kosekana) na 'boora' (sema) yanatofautishwa tu na urefu wa irabu 'o' n 'oo'.
. | Mbele | Kati | Nyuma |
---|---|---|---|
Iliyofungwa | i | u | |
Karibu-Iliyofungwa | ɪ | ʊ | |
Kati-Wazi | ɛ | ɔ | |
Wazi | a |
Konsonanti
haririKatika jedwali lifuatalo, alama za uandishi ambazo hutofautiana na zile za Alfabeti ya Kimataifa (IPA) zimewekewa mabano. palipo na alama mbili pamoja, ya kulia inaashiria konsonanti inavyotamkwa.
. | bilabial | alveo-palatal | palatal | velar |
---|---|---|---|---|
plosive | p b | t | c (c) | k g |
fricative | s | |||
affricate | cç (c) | |||
nasal | m | n | ɲ (ny) | ŋ (ng') |
trill | r | |||
approximant | w | j (y) |
Mofolojia ifuatayo pia inatumika:
- n+r = nd
- n+b = mb
- n+g = ŋg
- n+k = ŋk
- n+m = mm
Marejeo
haririBickmore, Lee
- 1997. Problems in constraining High tone spread in Ekegusii. Lingua, Toleo la 102, uk. 265-290.
- 1998. Metathesis and Dahl’s Law in Ekegusii. Studies in the Linguistic Sciences, Toleo la. 28:2, uk. 149-168.
- 1999. High Tone Spreading in Ekegusii Revisited: An Optimality Theoretic Account. Lingua, toleo. 109, uk. 109-153.
Cammenga, Jelle
- 2002 Phonology and morphology of Ekegusii: a Bantu language of Kenya. Köln: Rüdiger Köppe Verlag.
Whiteley, Wilfred H.
- 1956 A practical introduction to Gusii. Dar es Salaam/Nairobi/Kampala: East African Literature Bureau.
- 1960 The tense system of Gusii. Kampala: East African Institute of Social Research.
- 1974 Language in Kenia. Nairobi: Oxford University Press.
Viungo vya Nje
hariri- Ekegusii-English English-Ekegusii Dictionary Ilihifadhiwa 10 Mei 2007 kwenye Wayback Machine.
- Kigusii kwenye tovuti la Ethnologue
- Partial Gusii Swadesh list at Rosetta Project Ilihifadhiwa 1 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Ekegusii Encyclopedic Projects Ilihifadhiwa 4 Agosti 2010 kwenye Wayback Machine.
Kusikiza
hariri- lugha ya Kigusii kwenye Multitree
- http://www.ethnologue.com/language/guz
- Hadithi katika Redio ya Kitaifa kuhisi Lugha ya Kisii (kutoka Kipindi cha All Things Considered , 29 Aprili 2006)