Madaktari wasio na Mipaka-MSF

(Elekezwa kutoka Médecins sans Frontières)

Madaktari wasio na Mipaka (linajulikana mara nyingi kwa jina lake la Kifaransa Médecins Sans Frontières au kifupi chake MSF) ni shirika lisilo la serikali la kimataifa.

Kliniki ya MSF huko Chadi yahudumia wakimbizi ktoka Darfur

Ni maungano ya madaktari na wauguzi pamoja na wasaidizi wengine wanaojitolea kuwasaidia wagonjwa katika maeneo pasipo na huduma za kiafya hasa katika nchi penye vita za wenyewe kwa wenyewe au maafa asilia.

Shirika la MSF lilianzishwa 1971 na kundi la madaktari Wafaransa (kati yao Bernard Kouchner) baada ya vita ya Biafra huko Nigeria.

MSF hutawaliwa siku hizi na kamati ya wakurugenzi wanaokutana kwenye makao makuu mjini Geneva (Uswisi). Kila mwaka takriban madaktari na wauguzi 3,000 waingia katika miradi mbalimbali kwenye nchi 70 na wengi wao hukitolea wakati wa likizo bila malipo yoyote. Kuna waajiriwa takriban 1,000. Makisio ya mwaka hufikia jumla la dola za Marekani milioni 400 na asilimia 80 zachangiwa kwa njia ya zawadi za watu wa binafsi. Inayobaki ni pesa za serikali mbalimbali au shirika za kimataifa kama UM au Umoja wa Ulaya.

Mifano ya miradi ya MSF ni mahali kama Kosovo wakati wa vita, Sudan ya Kusini, Darfur, Chechniya au maeneo yaliyoathiriwa na tsunami ya Bahari Hindi mwaka 2004.

MSF ilipokea tuzo ya Nobel ya Amani mwaka 1999.

Viungo vya Nje

hariri

Matawi ya MSF

hariri