Nehemiah Shukuru Senyagwa (anajulikana kwa jina la M Nex Nex I; alizaliwa Sagara, Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma, Januari 15, 1999) ni msanii, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Tanzania.

M Nex Nex I
M Nex Nex I (2024)
M Nex Nex I (2024)
Alizaliwa Januari 15, 1999
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwimbaji

M Nex Nex I ameanza kuonyesha Kipaji chake akiwa na Umri wa Miaka 10 ambapo dada yake anaejulikana Kama Jemima pamoja na Mama mzazi wa M Nex Nex I walikuwa Watu wa Kwanza kugundua Kipaji na uwezo mkubwa aliokuwa nao katika kutunga mashairi na kuyaimba katika mfumo wa Hip hop.

Jemima, dada yake, alimsaidia M Nex Nex I kuandika Mashairi ya wasanii wa kubwa na Maarufu Nchini Tanzania ili aweze kuyakariri na kuyaimba kwa urahisi.

Alipokuwa shuleni M Nex Nex I alijiunga na Vikundi vya Kwaya pamoja na wanafunzi wenzake na kushirikishwa katika Matamasha mbalimbali ya kidini pamoja na sherehe mbalimbali zilizokuwa zikifanyika shuleni hapo.

Alipomaliza elimu ya Sekondari, M Nex Nex I alielekea Jijini Dar es Salaam ambako huko alikutana na Baadhi ya wasanii pamoja na wazalishaji wa Muziki ambao walimshauri namna ya kukuza Kipaji chake Cha Muziki.

Mnamo Aprili 2020 M Nex Nex I alifanikiwa kurekodi wimbo wake wa Kwanza alioupa jina la Come Now lenye maana ya (Njoo Sasa hivi) kwa tafsiri ya lugha ya kiswahili.

Juni, 2021 M Nex Nex I aliingia studio na kurekodi wimbo wa pili uliokwenda kwa jina Sio Poa ulioimbwa na Kenny Son ambapo alisimama Kama Msanii wa kushirikishwa. Wimbo huo uliandaliwa na Nayzer Touch chini ya studio za GM Records ambako ndiko ulipofanyika wimbo wa Kwanza wa M Nex Nex I - Come Now

Baada ya kuachia wimbo huo M Nex Nex I akaanza kupata mialiko ya mahojiano katika vyombo vya habari mbalimbali hususani ndani ya Mkoa wa Dodoma Kama vile A fm radio 92.9 , Dodoma Fm 98.4 n.k.

Februali, 2022 M Nex Nex I akiwa ameshajiunga na elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) akisomea shahada ya awali ya Sanaa ya Habari na Mahusiano Ya Umma , aliachia wimbo wake wa pili uliokwenda kwa jina la My Valentine aliomshirikisha Msanii wa hip hop Benchar Mc. Wimbo huu ulimpa nafasi kubwa ya kuongeza idadi ya mashabiki na wafuasi wa Muziki wake ndani na nje ya chuo kikuu Cha Dodoma.

Baada ya kuachia wimbo huo, M Nex Nex I aliachia Nyimbo zingine 4 ndani ya muda wa miezi miwili tu. Nyimbo hizo Ni Nakuwaza aliomshirikisha Msanii na Mwimbaji wa kike anaejulikana kwa jina la Mamilzy, wimbo mwingine ni Dream In love aliowashirikisha Wasanii wa Rap , (Ibrah Rapper na Rapper Tzee), Nyimbo zingine ni Sorry , Gimme Right Now, Pretty Girl pamoja na Useme aliomshirikisha msanii wa R&B kutoka Dodoma Imocy.

Marejeo hariri