Troia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|320px|Kuta mashuhuri za Troia zilizotajwa mara nyingi katika utenzi wa [[Iliadi ya Homer]] Image:Plan Troy-Hisarlik-...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 10:37, 26 Mei 2017

Troia (gir.: Τροία, troia, pia Ίλιον, ilion; ing.: Troy)[1] ilikuwa mji katika Asia Ndogo zamani za Ugiriki ya Kale. Inajulikana kutokana na utenzi wa Iliadi ambako mshairi Homer alisimulia habari za Vita ya Troia.[2]

Kuta mashuhuri za Troia zilizotajwa mara nyingi katika utenzi wa Iliadi ya Homer
Awamu za kukua kwa Troia kufuatana na utafiti wa akiolojia
Ramani ya Ugiriki ya Kale zamani za Homer

Kwa karne nyingi mahali pa mji hapajulikana ingawa watu wengi walijaribu kupakuta kwa saabu ya umaarufu wa utenzi huu uliokuwa na maana sana katika utamaduni wa Ulaya. Mnamo mwaka 1868 Mjerumani Heinrich Schliemann alianza kuchimba kwenye kilima cha Hisarlik kilichopo karibu na mji wa Çanakkale kwenye mgharibi kaskazini ya Uturuki. Alikuta mabaki ya majengo na kuta kubwa na baada ya majadiliano marefu leo hii wataalamu hukubaliana hapa palikuwa mahali pa Troia ya Kale.

Maghofu ya Troia yamepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO. Azimio hili lilitoka kwa maelezo yafuatayo:

"Mahali pa kiakolojia pa Troia ni muhimu sana kwa kuelewa vyanzo vya maendeleo ya ustaarabu wa Ulaya. Pana pia umuhimu mkubwa wa kiutamaduni kutokana na athira kubwa ya Iliadi ya Homer juu ya sanaa kwa muda wa zaidi ya milenia mbili". [3]

Tanbihi

  1. Lewis, Charlton T.; Charles Short. "Ilium". A Latin Dictionary. Tufts University: The Perseus Digital Library. Iliwekwa mnamo 2008. 
  2. March, Jenny (2008). The Penguin Book of Classical Myths. Penguin Books. uk. 294. ISBN 978-0-141-02077-8. 
  3. UNESCO citation