Bunduki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: thumb|Aina mbalimbali za bunduki thumb|Bunduki ya Kalachnikov '''Bunduki''' ni silaha inayorusha [[ri...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 16:10, 16 Machi 2008

Bunduki ni silaha inayorusha risasi dhidi ya shabaha yake. Ndani ya bunduki inatokea mlipuko wa baruti na gesi joto za mlipuko zinasukuma risasi kuelekea mwendo wa kasiba yake.

Aina mbalimbali za bunduki
Bunduki ya Kalachnikov

Aina za bunduki

Kwa kawaida neno lataja silaha za aina hii zenye kasiba ndefu zinazoshikwa mkononi.

  • Bunduki kubwa zaidi zinazosimama kwa magurudumu huitwa mzinga.
  • Bunduki ndogo yenye kasiba fupi ni bastola.
  • Bunduki kubwa kiasi inayofyatua risasi nyingi wakati moja ni bombomu (au: mzinga wa bombom; bunduki ya mtombo; bunduki ya rashasha).
  • Bunduki ya upepo inazotumia nguvu ya gesi yenye shindikizo bila mlipuko. Hii ni . Kwa silaha ndogo ya aina hii shindikizo inapatikana kwa kukandamiza hewa katika chumba cha bunduki. Aina zenye nguvu zinatumia ramia isiyo na baruti bali na gesi iliyokandamizwa ndani yake. Faida yake ni hazina kelele kubwa.
  • Bunduki ya marisau hutumiwa kwa kuwinda wanyama ikifyatua risasi nyingi ndogondogo. Ni rahisi zaidi kushika shabaha lakini haipigi mbali.