Mabilionea Ulimwenguni
Mabilionea Ulimwenguni ni orodha ya kila mwaka ya thamani ya utajiri ya mabilionea wakubwa duniani inayoandaliwa na kuchapishwa mwezi Machi kila mwaka na gazeti la Forbes la Marekani. Orodha ya kwanza ilichapishwa Machi 1987. Jumla ya thamani ya utajiri wa kila mmoja kwenye orodha hiyo unakadiriwa na kutolewa kwa dola ya Marekani kutegemeana na mali zao na madeni. Familia za Kifalme au madikteta ambao utajiri wao unatokana na nafasi zao na sio jasho huwa hawawekwi kwenye orodha hii.
Mwaka 2018, watu 2,208 wametokea kwenye orodha hii, ambayo ilijumuisha mabilionea wapya 259 wengi wao wakitokea China na Marekani, na watu 63 wenye umri chini ya 40 na wanawake 256.
Hadi 2018, mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates alikuwa ndio namba moja kwenye orodha hii kwa miaka 18 kati ya miaka 24, wakati mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos ameshika nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza na tajiri wa kwanza kwenye orodha mwenye utajiri thamani ya dola bilioni 100.[1] Mark Zuckerberg ni mtu pekee kwenye orodha ya mabilionea wakubwa 10 duniani mwenye umri wa chini ya miaka 50.[2]
Orodha ya kila mwaka
haririOrodha huchapishwa kila mwaka mwezi Machi. Orodha hizi zinaonyesha mabilionea wakubwa 10 tu kila mwaka.
Maelezo
haririAlama | Maana |
---|---|
▬ | Haijabadilika toka mwaka uliopita. |
Imeongezeka toka mwaka ulliopita. | |
Imepungua toka mwaka uliopita. |
2019
haririKwenye orodha ya Forbes ya 33, kuna mabilionea 2,153 ambao kwa ujumla wana thamani ya dola za Kimarekani trilioni 8.7.[3]
Na. | Jina | Thamani (USD) | Umri | Utaifa | Chanzo cha utajiri |
---|---|---|---|---|---|
▬ | 1Jeff Bezos | $131 billion | 55 | Marekani | Amazon |
▬ | 2Bill Gates | $96.5 billion | 63 | Marekani | Microsoft |
▬ | 3Warren Buffett | $82.5 billion | 88 | Marekani | Berkshire Hathaway |
▬ | 4Bernard Arnault | $76 billion | 70 | Ufaransa | LVMH |
5 | Carlos Slim | $64 billion | 79 | Meksiko | América Móvil, Grupo Carso |
▬ | 6Amancio Ortega | $62.7 billion | 82 | Hispania | Inditex, Zara |
7 | Larry Ellison | $62.5 billion | 74 | Marekani | Oracle Corporation |
8 | Mark Zuckerberg | $62.3 billion | 34 | Marekani | |
9 | Michael Bloomberg | $55.5 billion | 77 | Marekani | Bloomberg L.P. |
10 | Larry Page | $50.8 billion | 45 | Marekani | Alphabet Inc. |
Marejeo
hariri- Specific
- ↑ Kroll, Luisa. "Forbes 2017 billionaires list: Meet the richest people on the planet", Forbes.
- ↑ Shinal, John (2017-08-01). "Mark Zuckerberg is less than half the age of his super-wealthy peers". www.cnbc.com. Iliwekwa mnamo 2019-01-15.
- ↑ "Billionaires 2019". Forbes. 5 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 13 Machi 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)