Machozi Jasho na Damu


"Machozi Jasho na Damu", ni jina la kutaja albamu ya kwanza kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Kitanzania, Professor Jay. Albamu imetoka mwaka 2001, mwaka mmoja tangu kutolewa albamu aliyofanya na kundi zima la Hard Blasters Crew, Funga Kazi (2000). Jay anarudi tena kama msanii wa kujitegemea, lakini safari hii anaamua kutoa na albamu kabisa badala ya kufanya moja-moja. Kabla ya albamu na kujiunga HBC, Jay (wakati huo Nigga Jay) alifanya wimbo na Taff B. (Fascinating Rhymes) na amepita makundi mengi tu kabla kufika HBC halafu baadaye kurudi kama msanii wa kujigetemea. Albamu imetazama nyanja nyingi, kuanzia siasa, maisha, historia na hoja nzito kuhusu vijana na wazee.

Macho Jasho na Damu
Macho Jasho na Damu Cover
Studio album ya Professor Jay
Imetolewa 2001
Imerekodiwa 2000-2001[1][2][3]
Aina Hip hop, Bongo Flava
Lebo Bongo Records
usambazi ulifanywa na "FKW"
Mtayarishaji P. Funk
Wendo wa albamu za Professor Jay
"Machozi Jasho na Damu
(2001)
"Mapinduzi Halisi"
(2003)

Jay ameenda mbali zaidi katika albamu hii kwa kuenzi muziki wa hip hop wa Tanzania kwa kuelezea mengi tangu muziki huu unaanza katika miaka ya 1980 na 1990 mwanzoni. Katika "Tathmini" anaelezea jinsi walivyopata tabu katika kuanzishwa kwa muziki huu katika Tanganyika ya Kijamaa.

Halkadhalika ame-enzi kazi ya mwanzilishi halisi wa rap ya Kiswahili nchini Tanzania bwana Edward Mtui (maarufu kama Fresh XE) kwa kuchukua kiitikio chake cha "Piga Makofi" ambacho kilimpelekea ashinde tuzo ya Yo Rap Bonanza katika miaka ya 1980, lakini hakutoa nyimbo. Jay anatungia wimbo kiitikio hicho na ndani yake anataja wale wote walioifikisha hip hop ya Tanzania hapa kwa kuwataja.

Katika wimbo wa Piga Makofi, kamtaja, Cool Moe Cee, Fresh XE, Ibony Moalim (yeye na Kim ndio hasa waliokuwa waratibu wakuu kabisa wa Yo Rap Bonanza), Rankim Ramadhani, Big Rawy, JD, Uncle Jay, Masoud Masoud, Master T (Taji Liundi), Saleh Jabri na wengine wengi. Mtindo huu wa kuthamini muziki ulipotoka katika albamu hii umekuwa kitu cha kawaida huku utunzi na namna ya kuenzi hali halisi ya hip hop ya Tanzania katika nyimbo umekuwa wa kipekee sana.

Jay amerudia tena kuwataja waasisi wa muziki wa aina mbalimbali (Ugly Faces, KU Crew, Mr. 2, Taff B., Mack D, John Dillinger]], Tough B) nchini Tanzania katika wimbo wa "Yataka Moyo". Katika wimbo huo, Jay anajaribu kutazama kazi ya sanaa na kipato wanachokipata wasanii katika kazi hiyo. Halkadhalika anataja wasanii walioisukuma gemu ya muziki wa Tanzania katika kiwango cha sasa.

Vilevile anawataja wadau mbalimbali wa sanaa mbalimbali ambao nao walihangaikia kusukuma sanaa na wasanii wa Bongo katika ramani iliyoisimama. Mwaka ambao albamu hii inatoka, kulitoka pia albamu nyingine kibao, albamu kama vile Nini Chanzo, Ni Saa Ya Kufa Kwangu, Bwege Mtozeni, Poa Tu - Volume 1, Tuko Pamoja?... Vol. 1 na nyinginezo kibao. Huu ulikuwa mwaka wa mapinduzi hasa ya muziki wa kizazi kipya. Ilikuwa lazima kila albamu ikitoka ifanyiwe uzinduzi.[4]


Orodha ya nyimbo hariri

Hii ni orodha ya nyimbo zinazopatikana katika albamu hii.

  1. A1 - Ndio Mzee akiwa na Lady Jay Dee na MC Babu Ayubu
  2. A2 - Jay Jr. Interlude
  3. A3 - Jina Langu
  4. A4 - Bongo Dar Interlude
  5. A5 - Bongo Dar es Salaam - akiwa na Lady Jay Dee
  6. A6 - Yataka Moyo
  7. A7 - Nawakilisha
  8. B1 - Intro
  9. B2 - Machozi Jasho Na Damu
  10. B3 - Piga Makofi
  11. B4 - Niamini
  12. B5 - Salamu Bibi Na Babu
  13. B5 - Tathimini Interlude
  14. B6 - Tathimini
  15. B7 - Na Bado
  16. B8 - Outro


Tazama pia hariri


Marejeo hariri

  1. Machozi Jasho na Damu katika Awesome Tapes from Africa
  2. Machozi Jasho na Damu katika Reverb Nation
  3. Machozi Jasho na Damu katika wavuti ya Last FM
  4. Machozi Jasho na Damu katika wavuti ya "Discogs".