Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda


Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ing. International Criminal Tribunal for Rwanda, ICTR), au Tribunal pénal international pour le Rwanda (TPIR) kwa Kifaransa, ni mahakama ya kimataifa yaliyoanzishwa mnamo mwezi Novemba mwaka wa 1994 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuwahukumu watu walisababisha mauaji ya kimbari ya Rwanda na hatia zingine kuu za sheria ya kimataifa nchini Rwanda, au raia wa Kirwanda katika nchi jirani, kati ya tarehe mosi Januari na tarehe Desemba mwaka wa 1994

Mnamo mwaka wa 1995, mahakama hayo yalipata makao mjinui Arusha, Tanzania. Mahakama hayo yana mamlaka ya kisheria ya mauaji ya kimbari na hatia za kivita, ambazo zinafafanuliwa kama ukiukaji wa Ibara ya jumla ya tatu na Itifaki ya II ya Mkataba wa Geneva(unaohusu hatia za kivita zilizofanywa wakati wa migogoro ndfani ya nchi)

Kufikia wakati wa sasa, Mahakama hayo yamekamilisha kesi kumi na tisa na kuwahukumu washitakiwa ishirini na watano. Kesi za watu wengine ishirini na watano bado zinaendelea. Kumi na watisa wanasubiri kesi zao kizuizini. Kumi bado hawajakamatwa. Kesi ya kwanza, ya Jean-Paul Akayesu, ilianzishwa mnamo mwaka wa 1997. Jean Kambanda, Waziri Mkuu wa mpito, aliyakubali mashtaka.

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.