Mauaji ya kimbari ni maangamizi ya mpango ya kundi zima la watu au ya sehemu yake kwa msingi wa taifa, kabila, rangi au dini.

Kambi la Buchenwald walipouawa halaiki ya watu kwa amri ya Adolf Hitler.

Ufafanuzi

hariri

Ingawa ufafanuzi fasaha haujapatikana, kutokana na tofauti kati ya wataalamu wa mauaji ya kimbari, ufafanuzi wa kisheria hupatikana katika Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari (unaofupishwa "CPPCG" katika lugha ya Kiingereza) wa Umoja wa Mataifa wa mwaka wa 1948. Ibara ya 2 ya mkataba huo inayafafanua mauaji ya kimbari kama "Tendo lolote kati ya yale yafuatayo linalofanyika kwa nia ya kuharibu, kikamilifu au katika sehemu, kikundi cha kitaifa, kikabila, kirangi au cha kidini, kama vile: mauaji ya watu wa kikundi hicho; kusababisha athari kubwa upande wa mwili au wa akili kwa watu wa kikundi hicho; kutwika kwa makusudi juu ya kundi hali za maisha, zinazonuiwa kuleta uharibifu wa mwili mzima au sehemu ya mwili; kuchukua hatua zinazonuiwa kuzuia wanawake wasijifungue katika kikundi hicho; [na] kuhamisha watoto wa kikundi hicho hadi kikundi kingine kwa lazima.[1]

Utangulizi wa CPPCG unasema kuwa matukio ya mauaji ya kimbari yamefanyika tangu jadi,[1] lakini haikuwa hadi Raphael Lemkin alipoyatunga maneno hayo na wahusika wa Mauaji ya kimbari ya Wayahudi waliposhtakiwa katika kesi za Nuremberg; ndipo Umoja wa Mataifa ulipokubaliana na CPPCG ambayo iliufafanua uhalifu wa mauaji ya kimbari ya watu chini ya sheria ya kimataifa. Kulikuwa na zaidi ya miaka 40 kati ya CPPCG kukamilika na mashtaka ya kwanza chini ya masharti ya mkataba kufanywa.

Hadi leo mashtaka yote ya kimataifa ya mauaji ya kimbari, hasa ya Mauaji ya kimbari ya Rwanda, na Mauaji ya kimbari ya Srebrenica, yamefanywa kupitia mahakama ya dharura ya kimataifa.[2]

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai iliundwa mwaka wa 2002 ikiwa na mamlaka ya kuwahukumu watu kutoka nchi ambazo zimetia saini mkataba huo, lakini hadi sasa haijamhukumu yeyote.

Tangu CPPCG ianze kutumika mnamo Januari 1951, takriban nchi 80 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa zimepitisha sheria ambayo inayajumuisha masharti ya CPPCG ndani ya sheria za nchi yao, na baadhi ya wahusika wa mauaji ya kimbari wamepatikana na hatia chini ya sheria za namna hizo, kama vile Nikola Jorgic, ambaye alipatikana na hatia ya mauaji ya kimbari katika Bosnia na mahakama ya Ujerumani (Jorgic dhidi ya Ujerumani).

Wakosoaji wa CPPCG wameangazia uwepo wa ufafanuzi finyu wa makundi yanayolindwa chini ya mkataba, hasa ukosefu wa ulinzi kwa makundi ya kisiasa, jambo ambalo linajulikana kama Mauaji ya watu wa kundi fulani la kisiasa (Mauaji hayo yamejumuishwa na mauaji ya kimbari katika baadhi ya nchi).[3]

Tatizo moja ni kwamba hadi mkusanyiko wa kesi za sheria kutoka mashtaka upatikane, ufafanuzi fasaha wa kile ambacho mkataba ulimaanisha haukuwa umepimwa mahakamani, kwa mfano, ni nini hasa maana ya maneno "katika sehemu"? Kadiri wahalifu wanavyozidi kufikishwa mahakamani chini ya mfumo wa mahakama ya kimataifa na kesi za mahakama za nchi, ndivyo mkusanyo wa hoja za kisheria na tafsiri za kisheria unavyosaidia kuyashughulikia masuala haya.

Ukosoaji mwingine wa CPPCG ni kwamba wakati vifungu vyake vimetumiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, vimetumiwa tu kuwaadhibu wale ambao tayari wametenda mauaji ya kimbari na wamekuwa wapumbavu kiasi kwamba wameacha ishara fulani iliyoandikwa. Ilikuwa ukosoaji huo uliosababisha kuundwa kwa Sheria ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya 1674 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 28 Aprili 2006, ambayo inahimiza Baraza lichukue hatua ya kuwalinda raia katika vita na kulinda wakazi kutoka mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita, utakaso wa kikabila na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Wasomi wa mauaji ya kimbari, kama vile Gregory Stanton, wamedadisi kwamba masharti na vitendo ambavyo mara nyingi hutokea kabla, wakati na baada ya mauaji ya kimbari - kama vile vikundi vya wahasiriwa kunyimwa utu, upangaji kabambe katika makundi yanayofanya mauaji ya kimbari, na kukana kwa mauaji ya kimbari na wahusika wake - yanaweza kutambuliwa na hatua kuchukuliwa kukomesha mauaji ya kimbari kabla ya kutokea. Wakosoaji wa mbinu hii, kama vile Dirk Moses, wamedai kwamba haya hayafafani na mambo jinsi yalivyo na kwamba, kwa mfano, "Michafuko ya Darfur itakamilika kwa wakati utakaozifaa nguvu kubwa ambazo zina mambo yatakayozifaidi katika kanda hiyo".

Utunzi wa msamiati "Genocide"

hariri

Maneno "mauaji ya kimbari" yalianzishwa na Lemkin Raphael (mwanachuoni wa kisheria mwenye asili ya Kiyahudi aliyezaliwa Poland 1900-1959), mnamo mwaka wa 1944, kwanza kutoka Kilatini "gens, gentis," kumaanisha "kuzaliwa, kabila, ukoo, aina" au mzizi wa Kigiriki "génos" (γένος) (maana sawa); pili kutoka Kilatini -"cidium" (kukata, na kuua) kupitia Kifaransa -"cide".[4][5]

Mwaka wa 1933, Lemkin aliitayarisha insha yenye kichwa: Uhalifu wa Kinyama ambapo mauaji ya kimbari yalionyeshwa kuwa uhalifu dhidi ya sheria za kimataifa. Dhana ya uhalifu, ambayo baadaye ilibadilika na kuwa wazo la mauaji ya kimbari, ilitokana na mang'amuzi ya Waashuri [6] waliouawa kinyama nchini Iraq tarehe 11 Agosti 1933. Tukio la Iraq lilimpa Lemkin "kumbukumbu ya kuchinjwa kwa Waarmenia" kwa mikono ya Waturuki miaka 1915-1916, wakati wa Vita Vikuu Vya Kwanza Vya Dunia.[6] Aliliwakilisha pendekezo lake la kwanza la kuyafanya "matendo kama hayo ya kinyama" yawe hatia kwa Baraza la Sheria la Shirikisho la Mataifa mjini Madrid mwaka huohuo. Pendekezo lilishindikana, na kazi yake haikuifurahisha serikali ya Polandi, ambayo wakati huo ilikuwa ikiifuata sera ya upatanisho na Ujerumani wa Kinazi.[6]

Mwaka wa 1944, Taasisi ya Carnegie kwa Amani ya Kimataifa ilachapisha maandishi muhimu zaidi ya Lemkin, yaliyoitwa Utawala wa Kiaksisi Katika Ulaya Iliyokuwa si Huru, nchini Marekani. Kitabu hicho kilikuwa na uchambuzi wa kina wa kisheria wa utawala katika nchi zilizosimamiwa na Ujerumani wa Kinazi wakati wa Vita Vikuu Vya Pili Vya Dunia, pamoja na ufafanuzi wa maneno mauaji ya kimbari.[7]

Wazo la Lemkin la mauaji ya kimbari kama kosa dhidi ya sheria za kimataifa lilikubalika na jamii ya kimataifa na lilikuwa mojawapo kati ya sheria msingi za Mashitaka ya Nuremberg (mashitaka ya viongozi 24 wa Kinazi) iliyotilia mkazo katika sehemu ya 3 kuwa watuhumiwa "walifanya mauaji ya kimbari kwa makusudi na kwa utaratibu - yaani, kuviaangamiza vikundi vya rangi na vya kitaifa ..." [8])

Lemkin aliiwasilisha rasimu ya azimio la Mkataba wa mauaji ya kimbari kwa nchi kadhaa katika jitihada za kuzishawishi zilidhamini azimio hilo. Kupitia msaada wa Marekani, azimio liliwekwa mbele ya Mkuu wa Bunge lizingatiwe. Akiyafafanua mauaji ya kimbari mwaka wa 1943, Lemkin aliandika:

Kiujumla, mauaji ya kimbari si lazima yamaanishe uangamizaji wa taifa mara moja, isipokuwa yanapofuatwa na mauaji ya halaiki ya watu wote wa taifa hilo. Inanuiwa kuashiria mpango wa hatua mbalimbali zenye nia ya kuangamiza misingi muhimu ya maisha ya vikundi vya kimataifa, zikiwa na nia ya kuviangamiza vikundi hivi vyenyewe. Lengo la mpango kama huo utakuwa kubomoa miundo-msingi ya kisiasi na kijamii, ya tamaduni, lugha, hisia za kitaifa, dini na kuwepo kwa vikundi vya kitaifa kiuchumi, na uharibifu wa usalama wa kibinafsi, uhuru, afya, heshima na hata maisha ya watu binafsi katika vikundi hivyo.[9]


Mauaji ya kimbari kama uhalifu

hariri

Chini ya sheria ya kimataifa

hariri

Kufuatia mauaji ya kimbari ya Wayahudi, Lemkin alifanikiwa katika kampeni za kukubalika ulimwenguni kote kwa sheria za kimataifa zilizoyafafanua mauaji ya kimbari na kuyapinga. Mnamo mwaka wa 1946, kikao cha kwanza cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa]] kilipitisha azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Sheria 96 "lililosisitiza" kwamba mauaji ya kimbari yalikuwa hatia chini ya sheria ya kimataifa, lakini ambalo halikutoa ufafanuzi wa kisheria wa uhalifu huo. Mnamo mwaka 1948, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliukubali "Mkataba wa Kuzuia na Kuadhabu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari" ambao ulifafanua kisheria kwa mara ya kwanza mauaji ya kimbari.

"CPPCG" ilipitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 9 Desemba 1948 na ikawa rasmi mnamo 12 Januari 1951 (Sheria nambari 260 (III)). Inayo ufafanuzi unaotambulika kimataifa wa mauaji ya kimbari ambao uliingizwa kwenye sheria ya jinai ya kitaifa ya nchi nyingi, na ilikubalika na Katiba ya Roma ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, mkataba ambao ulianzisha Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC kwa lugha ya Kiingereza). Mkataba (katika ibara ya 2) unafafanua mauaji ya kimbari:

...tendo lolote kutoka ya yale yafuatayo linalofanyika na nia ya kuharibu, kikamilifu au katika sehemu, kikundi cha kitaifa, kikabila, kirangi au kundi la kidini, kama vile

(a) mauaji ya watu wa kikundi hicho;
(b) kusababisha athari kubwa ya kimwili au kiakili kwa watu wa kikundi hicho;
(c) kuzitwika kimakusudi juu ya kundi hali za maisha, zinazonuiwa kuleta uharibifu wa mwili mzima au sehemu ya mwili;
(d) kuchukua hatua zinazonuiwa kuzuia wanawake wasijifungue) katika kikundi hicho;
(e) kuhamisha watoto wa kikundi hicho hadi kundi lingine kwa lazima.

Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Hualifu wa Mauaji ya Kimbari, Ibara ya II

Rasimu ya kwanza ya Mkataba iliyajumuisha mauaji ya kisiasa, lakini Muungano wa Jamhuri za Kisosholisti za Kisovyeti [10] pamoja na baadhi ya mataifa mengine yalikataa hatua dhidi ya makundi yaliyotambuliwa kuwa na maoni sawa ya kisiasa au hali ya kijamii yatambulike kama mauaji ya kimbari,[11] kwa hivyo, masharti haya hatimaye yaliondolewa katika maelewano ya kisiasa na kidiplomasia.

Mkataba ulionekana kukubalika kwa minajili ya kuwasaidia watu katika taabani na raia. Malengo yake ni kulinda kuwepo kuwa vikundi fulani vya watu na kutilia mkazo na kusisitiza zile kanuni za kimsingi za utu na maadili. Kulingana na haki zilizopo, majukumu ya kisheria ya kujiepusha na mauaji ya kimbari yanafahamika kama erga omnes

Wakati mkataba uliporasimiwa kwa mara ya kwanza, tayari ilitarajiwa kuwa haungetumika tu kwa kwa aina ya mauaji ya kimbari ya wakati huo, bali ungetumika "kwa mbinu yoyote ambao huenda ingeundwa siku za usoni kwa madhumuni ya kuangamiza kikundi fulani".[12] Jinsi ilivyosisitizwa katika utangulizi wa Mkataba, mauaji ya kimbari yameadhiri enzi zote za kihistoria, na ni kwa kulifahamu swala hili la kusikitisha ambapo dhana hii inapewa hali yake ya kubadilika ya kihistoria.

Mkataba lazima utafsiriwe kwa nia nzuri, kulingana na maana ya kawaida ya maneno yake, katika muktadha wa maneno hayo, na kwa mujibu wa chombo na lengo lake. Isitoshe, nakala ya Mkataba inafaa itafsiriwe kwa namna itakayowezesha sababu na maana ipewe kwa kila neno. Hakuna neno au sehemu nyeti ambayo inafaa kupuuzwa au kufanywa kana kwamba imetumia maneno mengi bure, labda tu ikiwa kufanya hivi kunahitajika kutupea maana kwa maswala yatakaposomwa kikamilifu.[13]

Mauaji ya kimbari ni hatia chini ya sheria ya kimataifa bila kujali "ikiwa makosa yalitendwa katika kipindi cha amani au vita" (ratiba ya I). Kwa hivyo, muktadha ambapo jambo lilitokea haujalishi (kwa mfano, wakati wa amani, wakati wa migogoro ndani ya kitaifa, migoro ya kimataifa ya silaha au kiujumla yoyote yanayoendela) mauaji ya kimbari ni hatia ya kimataifa inayoadhibika. –

Kamati ya Wataalamu ya Umoja wa Mataifa iliyochunguza ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu katika eneo la Yugoslavia ya zamani.[14]

Nia ya kuharibu

hariri

Mnamo mwaka wa 2007 Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR kwa lugha ya Kiingereza), ilibainisha katika uamuzi wake wa kesi ya Jorgic dhidi ya Ujerumani kuwa mnamo mwaka wa 1992 wasomi wengi wa kisheria walikuwa na mtazamo finyu kwamba "nia ya kuharibu" katika CPPCG ilimaanisha uharibifu wa kimwili na kibaiolojia wa kundi lenye ulinzi na kwamba haya bado yalikuwa maoni ya wengi. Lakini ECHR pia ilibainisha kuwa wachache walikuwa na mtazamo mpana na hawakufikiri uharibifu wa kimwili na kibaiolojia ulikuwa muhimu kwani dhamira ya kuharibu kundi la kitaifa, kirangi, kidini au kikabila ilitosha kuhitimu kuwa mauaji ya kimbari.[15]

Katika hukumu iyo hiyo ECHR ilipitia uamuzi wa mahakama kadhaa ya kimataifa na ya kimanisipaa na Ilibainisha kuwa Mahakama ya Kimataifa la Jinai ya Yugoslavia ya Zamani na Mahakama ya Kimataifa ya Haki yalikuwa yamekubali kupitia ufafanuzi finyu, kwamba uharibifu wa kibaiolojia na kimwili ulikuwa muhimu kwa tendo kuhitimu kuwa mauaji ya kimbari.

ECHR pia ilibainisha kuwa wakati wa uamuzi wake, mbali na mahakama nchini Ujerumani ambayo yalikuwa na mtazamo mpana, kulikuwa na kesi chache za mauaji ya kimbari chini katika nchi zingine zilizokuwa miongoni mwa sheria manisipaa za nchi zilizokuwa zimetia sahini mkataba na kwamba "Hakuna kesi zilizoripotiwa ambapo mahakama ya nchi hizo yamefafanua aina ya uharibifu wa kikundi ambao lazima mhalifu awe amekusudia ili kupatikana na hatia ya mauaji ya kimbari".[16]

Katika sehemu

hariri

Maneno "kikamilifu au katika sehemu" yamejadaliwa kwa kina na wasomi wa sheria ya kibinadamu ya kimataifa.[17]

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Yugoslavia ya Zamani yalibainisha katika kesi la "Mwendesha mashitaka dhidi ya Radislav Krstic - Chumba cha Kesi I - uamuzi- IT-98-33 (2001) ICTY8 (2 Agosti 2001)" [18] kwamba mauaji ya kimbari yalikuwa yametendeka. Katika "Mwendesha dhidi ya Radislav Krstic - Chumba cha Rufaa - Uamuzi- IT-98-33 (2004) ICTY 7 (19 Aprili 2004) " [19] aya za 8, 9, 10, na 11 zilifumbua suala la "katika sehemu" na zilipata kuwa "sehemu lazima iwe sehemu muhimu ya kundi.

Lengo la Mkataba wa Mauaji ya Kimbari ni kuzuia uangamizaji wa kimakusudi wa makundi zima ya binadamu, na sehemu iliyolengwa lazima iwe muhimu kiasi cha kuadhirisha kundi zima." Mahakama ya Rufaa inapeana maelezo zaidi ya kesi zingine na maoni ya wachambuzi wa kuheshimika kuhusu Mkataba wa Mauaji ya kimbari kuelezea jinsi walivyolifikia hitimisho hili.

Waamuzi wanaendelea katika aya ya 12, “Uamuzi wa ikiwa wakati sehemu inayolengwa inatosha kukidhi mahitaji haya unabidi maswala mengi yazingatiwe. Ukubwa wa kiidadi wa sehemu ya kikundi inayolengwa ndiyo sehemu muhimu na inayofaa kuanzia, ingawa sio mwisho wa uchunguzi katika matukio yote. Idadi ya watu binafsi wanaolengwa lazima inakiliwe si tu kwa ujumla, lakini pia kwa uhusiano na ukubwa wa kijumla wa kundi zima. Bali na ukubwa wa kiidadi wa sehemu inayolengwa, umuhimu wake katika kundi unaweza kuwa wazo muhimu. Ikiwa sehemu maalum ya kikundi inaweza kuliwakilisha kundi lote kiujumla, au ni muhimu kwa uhai wake, hilo linaweza kuunga mkono wazo kuwa sehemu hiyo inahitimu kama muhimu kulingana na maana ya Ibara ya 4 [ya Katiba ya Mahakama].” [20][21]

Katika aya ya 13 ya waamuzi wanaangazia suala la wahalifu kuweza kuwafikia waathirika: “mifano ya kihistoria ya mauaji ya kimbari pia inaonyesha kwamba eneo la wahalifu, wanalojishughulisha nalo na kulidhibiti, na pia kiwango wanachoweza kufikia, yanafaa kutiliwa maanani... Dhamira ya kuharibu inayoundwa na mhalifu wa mauaji ya kimbari daima itakomeshwa na upungufu wa nafasi inayopatikana kwake. Ingawa sababu hii pekee haitaonyesha kama kundi linalolengwa ni la kutosha, inaweza - ikihusishwa pamoja na mambo mengine - kusaidia katika uchambuzi.” [19]

CPPCG kufanywa kuwa na nguvu za kisheria

hariri

Baada ya nchi chache 20 zilizohitajika kuupitisha Mkataba kutia sahihi, ulifanywa kuwa sheria ya kimataifa mnamo tarehe 12 Januari 1951. Hata hivyo wakati huo, wanachama wawili pekee kati ya wanachama tano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC kwa Kiingereza) walikuwa wametia sahini mkataba: Ufaransa na Jamhuri ya Uchina. Hatimaye Umoja wa Kisovyeti ulitia sahini mnamo mwaka wa 1954, Uingereza mnamo mwaka wa 1970, Jamhuri ya Watu wa Uchina mnamo mwaka wa 1983 (Ikiwa imeingia badala ya Jamhuri ya Uchina yenye makao Taiwan katika UNSC mnamo mwaka wa 1971), na Marekani mnamo mwaka wa 1988. Kukawia huku kurefu kuunga mkono Mkataba wa mauaji ya Kimbari na mataifa yenye nguvu duniani kulisababisha Mkataba kutotumika kwa zaidi ya miongo minne. Ni tu katika miaka ya 1990 ndipo sheria ya kimataifa ya uhalifu wa mauaji ya kimbari ilipoanza kutekelezwa.

Wajibu wa Baraza la Usalama kulinda

hariri

[[Sheria ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nambari 1674, iliyopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 28 Aprili 2006, "inatilia mkazo masharti ya aya za 138 na 139 za Nyaraka ya Matokeo ya Mkutano wa Dunia wa mwaka 2005 kuhusu wajibu wa kuwalinda wakazi kutoka mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita, utakaso wa kikabila na uhalifu dhidi ya ubinadamu".[22] azimio linapea Baraza jukumu la kuchukua hatua kuwalinda raia wakati wa vita.

Chini ya sheria ya nchi

hariri

Tangu Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari (CPPCG kwa Kiingereza) ulipofanywa kuwa sheria mnamo Januari mwaka wa 1951 zipatazo nchi 80 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa zimepitisha sheria ambayo inajumuisha masharti ya CPPCG katika sheria zao za kimanispaa.

Ukosoaji wa CPPCG na fafanuzi mbalimbali za mauaji ya kimbari

hariri

William Schabas amependekeza kuwa kuwepo kwa mwili wa kudumu kama ilivyopendekezwa katika Ripoti ya Whitaker kufuatilia utekelezaji wa Mkataba wa mauaji ya kimbari, na kuhitaji nchi kutoa ripoti kuhusu jinsi zinavyoufuata mkataba (kama zile zilizojumuishwa ndani ya Itifaki Isiyo ya Lazima ya Mkataba dhidi ya Mateso ya Umoja wa Mataifa) , kutaufanya mkataba uwe na ufanisi zaidi.[23]

Wakiandika mnamo mwaka wa 1998 Kurt Jonassohn na Karin Bjørnson walisema kuwa CPPCG ilikuwa chombo cha kisheria kilichotokana na maafikiano ya kidiplomasia. Kwa hivyo, maneno ya mkataba hayafai kuwa ufafanuzi ufaao kutumika kama zana ya utafiti, na ingawa inatumika kwa kusudi hili, kwani ina hadhi ya kisheria ya kimataifa ambayo nyingine hazina, ufanunuzi mbalimbali pia umedadisiwa. Jonassohn na Bjørnson wanazidi kusema kwamba hakuna fafanuzi mbadala kati ya hizi ambazo zilizopata msaada mwingi kwa sababu mbalimbali.[24]

Jonassohn na Bjørnson wanadadisi kuwa sababu kuu ya ukosefu wa ufafanuzi wa kiujumla wa mauaji ya kimbari kuibuka ni kuwa wasomi wameurekebisha mtazamo wao ili kuvisisitiza vipindi tofauti na wamepata kuwa ni afadhali kutumia fafanuzi zinazotofautiana kidogo ili kuwasaidia kuyatafsiri matukio. Kwa mfano Frank Chalk na Kurt Jonassohn waliichunguza historia yote ya binadamu, ilhali Leo Kuper na R.J. Rummel katika maandishi yao ya hivi karibuni waliupea uzito karne ya 20, na Helen Fein, Barbara Harff na Ted Gurr wameyaangalia matukio yaliyofuata Vita Vya Pili Vya Duniani. Jonassohn na Bjørnson wameyakosoa baadhi ya matokeo ya utafiti huu wakisema kuwa ni mapana sana na wanahitimisha kwamba nidhamu ya kielimu ya masomo ya mauaji ya kimbari ni changa mno kuwa na msingi ambapo dhana ya kitaaluma itaweza kujengwa.[24]

Kuondolewa kwa makundi ya kijamii na kisiasa kama malengo ya mauaji ya kimbari katika ufafanuzi wa kisheria wa CPPCG umekosolewa na baadhi ya wanahistoria na wataalamu wa kijamii, kwa mfano M. Hassan Kakar katika kitabu chake "Uvamizi wa Kisovyeti na Jibu la Kiafghani, 1979-1982" [25] anadokeza kuwa ufafanuzi wa kimataifa wa mauaji ya kimbari una vikwazo vingi sana,[26] na kwamba ni lazima ujumuishe makundi ya kisiasa au kikundi chochote kinachofafanuliwa hivyo na mhalifu na anawanukuu Chalk na Jonassohn: "Mauaji ya kimbari ni mauaji ya aina ya kihalaiki kwa upande mmoja ambapo nchi au wenye mamlaka wanakusudia kuangamiza kundi, kwani kundi na uanachama katika kundi hilo linafafanuliwa na mhalifu." [27]

Ingawa kuna ufafanuzi mbalimbali wa hayo maneno, Adam Jones anasema kwamba wasomi wengi wa mauaji ya kimbari hufikiria kuwa "nia ya kuharibu" ni sharti iwe kwa kitendo chochote kuitwa mauaji ya kimbari, na kwamba kuna makubaliano yanayozidi kuongezeka kuhusu kujumuisha swala la uharibifu wa kimwili.[28] Barbara Harff na Ted Gurr waliyafafanua mauaji ya kimbari kama "ukuzaji na utekelezaji wa sera na nchi au mawakala wake ambazo husababisha vifo vya sehemu muhimu ya kundi ... [wakati] makundi yanayoteswa yanafafanuliwa kimsingi kupitia sifa za jumuiya zao, yaani, kabila, dini au utaifa." [29] Harff na Gurr pia wanatofautisha mauaji ya kimbari na mauaji ya kundi la kisiasa kupitia sifa ambazo wanachama wa kundi hilo wanajitambulisha kwa serikali. Katika mauaji ya kimbari, makundi yanayodhulumiwa yanafafanuliwa kimsingi kupitia sifa za jumuiya zao, yaani, kabila, dini au utaifa. Katika mauaji ya kisiasa makundi ya wahasiriwa yanafafanuliwa kimsingi kupitia nafasi ya kihierarkia au upinzani wa kisiasa dhidi ya utawala au vikundi muhimu.[30][31]

Daniel D. Polsby na Don B. Kates, Jr. wanasema ya kuwa "... sisi tunafuata mbinu ya Harff inayotofautisha kati ya mauaji ya kimbari na mauaji ya wapinzani wa kisiasa ambayo anaelezea kuwa 'hasira ya halaiki isiyokawia kwa muda mrefu, ambayo, ingawa mara nyingi inaruhusiwa na wenye mamlaka, ni nadra kuendelea. ' Kama ghasia itaendelea kwa muda fulani, basi, anasema Harff, tofauti kati ya kuruhusu na kushiriki itaisha. "[32]

Kulingana na R.J. Rummel, mauaji ya kimbari yana maana tatu tofauti. Maana yake ya kawaida ni mauaji ya watu na serikali kutokana nao kuwa wanachama wa kundi fulani la kitaifa, kikabila, kirangi, au kidini. Maana ya kisheria ya mauaji ya kimbari inahusu mkataba wa kimataifa, Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari. Hii pia ni pamoja na kutoua ambao mwishowe kunaangamiza, kama vile kuzuia kuzaliwa au kuhamisha watoto kwenda kundi lingine kwa lazima. Maana ya kiujumla ya mauaji ya kimbari ni sawa na maana ya kawaida lakini pia inajumuisha mauaji ya kiserikali ya wapinzani wa kisiasa au vinginevyo mauaji ya kimakusudi. Ni kwa minajili ya kuepuka utata kuhusu maana inayolengwa ndio Rummel akayatunga maneno mauaji ya idadi ya wakazi kwa ile maana ya tatu.[33]

Ukosoaji mkuu wa jinsi jumuiya ya kimataifa ilivyokabiliana na Mauaji ya kimbari ya Rwanda ni kuwa ilikuwa tendaji, si makini. Jamii ya kimataifa imeanzisha mfumo kwa ajili ya kuendesha mashtaka dhidi ya wahalifu wa mauaji ya kimbari lakini bado haijaunda nia au mifumo ya kukomesha mauaji ya kimbari wakati yanapotokea. Wakosoaji wanaashiria mgogoro wa Darfur na kupendekeza kwamba ikiwa yeyote atapatikana na hatia ya mauaji ya kimbari baada ya mgogoro huo iwe kupitia mashtaka mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai au Mahakama ya kidharura ya Jinai, hili litauthibitisha mtazamo huu. Kigezo:Marejeo yanahitajika

Mashitaka ya kimataifa ya mauaji ya kimbari

hariri

Kupitia mahakama ya kidharura

hariri

Nchi zote zilizotia saini mkataba wa CPPCG zinafaa kuzuia na kuadhibu vitendo vya mauaji ya kimbari, katika wakati wa amani na vita, ingawa vizuizi kadhaa hufanya hili liwe jambo gumu kutekeleza. Hasa, baadhi ya watia sahini &mdash yaani, Bahrain, Bangladesh, Uhindi, Malaysia, Ufilipino, Singapore, Marekani, Vietnam, Yemen, na Yugoslavia &mdash zilitia saini na maafikiano kwamba hakuna madai ya mauaji ya kimbari yangeoweza kuletwa dhidi yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki bila idhini yao.[34]

Licha ya maandamano rasmi ya watia sahini wengine (hasa Kupro na Norway) kuhusu maadili na uaminifu wa kisheria wa kinga wanayojipa, kinga hiyo dhidi ya mashitaka imetumika mara kadhaa, kama wakati Marekani ilipokataa kuruhusu madai ya mauaji ya kimbari kufanywa dhidi yao na Yugoslavia kufuatia vita vya 1999 vya Kosovo.[35]

Kawaida imekubalika kwamba, angalau tangu Vita Vikuu Vya Pili vya Dunia, mauaji ya kimbari yamekuwa haramu chini ya sheria ya kimila ya kimataifa kama kinga na vilevile chini ya sheria ya kawaida ya kimataifa. Kwa ujumla, ni vigumu kuyaanzisha mashtaka dhidi ya matendo ya mauaji ya kimbari, kwa sababu mfululizo wa uwajibikaji lazima ufahamike. Mahakama ya Kimataifa ya Jinai hutumika haswa kwa sababu nchi husika haziwezi kuyashitaki au hazina nia ya kuushitaka uhalifu wenye ukubwa wa kiasi hiki zenyewe.

Kesi za Nuremberg

hariri
Makala kuu: Kesi za Nuremberg

Kwa sababu kukubalika kwa sheria za kimataifa ulimwenguni kote, zinazoyafafanua na kuyapinga mauaji ya kimbari kulitimika mnamo mwaka wa 1948, pamoja na kupitishwa kwa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu kwa Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari (CPPCG), wale wahalifu ambao walishitakiwa baada ya vita katika mahakama ya kimataifa, kwa ajili ya kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Wayahudi walipatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na hatia zingine maalum kama vile mauaji. Hata hivyo mauaji ya kimbari ya Wayahudi yanatambuliwa duniani kote kuwa mauaji ya kimbari, na maneno ambayo yalikuwa yameundwa mwaka wa awali na Raphael Lemkin,[36] yalionekana katika mashitaka ya viongozi 24 wa Kinaksi, shitaka la 3, lilisema kuwa watuhumiwa wote walikuwa "wameua kimakusudi na kwa utaratibu - yaani, uangamizaji wa vikundi vya kirangi na vya kitaifa ... " [37]

Rwanda

hariri
 
Vifuvu vya waadhiriwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda katika makavazi ya makumbusho

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR kwa lugha ya Kiingereza) ni mahakama chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kushitaki makosa yaliyotokea nchini Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari yaliyotokea pale katika kipindi cha Aprili 1994, kilichoanza tarehe 6 Aprili. ICTR iliundwa tarehe 8 Novemba 1994 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuhukumu wale watu waliofanya vitendo vya mauaji ya kimbari na ukiukaji mwingine mbaya wa sheria za kimataifa nchini Rwanda, au kwa raia wa Rwanda katika majimbo jirani , kati ya tarehe 1 Januari na tarehe 31 Desemba 1994.

Kufikia wakati wa sasa, ICTR imekamilisha kesi kumi na tisa na kuwahukumu washitakiwa ishirini na watano. Kesi za watu wengine ishirini na watano bado zinaendelea. Kumi na watisa wanasubiri kesi zao kizuizini. Kumi bado hawajakamatwa. Kesi ya kwanza, ya Jean-Paul Akayesu, ilianzishwa mnamo mwaka wa 1997. Jean Kambanda, Waziri Mkuu wa mpito, aliyakubali mashtaka.[38]

Yugoslavia ya Zamani

hariri

Maneno Mauaji ya kimbari ya Bosnia hutumika kurejelea mauaji ya kimbari yaliyofanywa na vikosi vya Kisabi pale Srebrenica mnamo mwaka wa 1995,[39] au kwa utakaso wa kikabila ambao ulifanyika wakati wa Vita vya Kibosnia vya mwaka 1992 hadi 1995 (mtazamo unaokataliwa na wasomi wengi).[40]

Mnamo mwaka wa 2001 Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Yugoslavia ya Zamani (ICTY kwa Kiingereza) yaliamua kuwa mauaji ya Srebrenica yaliyotendeka mwaka wa 1995 yalikuwa kitendo cha mauaji ya kimbari.[41]

Mnamo tarehe 26 Februari mwaka wa 2007 Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), katika kesi ya Mauaji ya Kimbari ya Kibosnia yaliuunga mkono uamuzi wa awali wa ICTY kwamba mauaji ya Srebrenica yalikuwa mauaji ya kimbari, lakini yalipata kuwa serikali ya Kisabia haikuwa imeshiriki katika mauaji ya kimbari mapana zaidi katika eneo la Bosnia na Herzegovina wakati wa vita, jinsi serikali ya Kibosnia ilivyokuwa ikidai.[42]

Mnamo tarehe 12 Julai 2007, Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR kwa lugha ya Kiingereza) ikiikataa rufaa ya Nikola Jorgic dhidi ya kushitakiwa kwake kwa mauaji ya kimbari na mahakama ya Kijerumani (Kesi ya Jorgic dhidi ya Ujerumani) ilibainisha kuwa tafsiri pana ya mahakama ya Kijerumani kuhusu mauaji ya kimbari imekataliwa na mahakama ya kimataifa yanapozingatia kesi sawa.[43][44][45]

ECHR pia ilibainisha kuwa katika karne ya 21 "Miongoni mwa wasomi, wengi wana maoni kwamba utakaso wa kikabila, haswa jinsi ulivyotendwa na vikosi vya Kisabi katika Bosnia na Herzegovina ili kuwafukuza Waislamu na Wakroati kutoka makazi yao , haukuwa mauaji ya kimbari. Hata hivyo, kuna idadi kubwa ya wasomi pia ambao wamependekeza kuwa matendo haya yalikuwa mauaji ya kimbari"[46]

Watu wapatao 30 wameshitakiwa kwa mauaji ya kimbari au kushiriki katika mauaji ya kimbari wakati wa miaka ya mapema ya 1990 nchini Bosnia. Hadi wa leo baada ya maombi mengi maalum mbele ya koti na hukumu chache ambazo zilifanikiwa kutupiliwa mbali baada ya rufaa Radislav Krstic tu ndiye aliyekuwa amepatikana na hatia ya kushiriki katika mauaji ya kimbari katika mahakama ya kimataifa. Kigezo:Marejeo yanahitajika Wengine watatu wamepatikana na hatia ya kushiriki katika mauaji ya kimbari nchini Bosnia na mahakama ya Kijerumani, mmoja wao akiwa Nikola Jorgic ambaye alishindwa katika rufaa dhidi ya hukumu yake katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu. Kesi za mashtaka zinaendelea nchini Bosnia na Herzegovina dhidi ya wanachama wengi wa zamani wa vikosi vya usalama vya Kibosnia na Kisabi kwa mashitaka mengi yakiwemo mauaji ya kimbari.

Slobodan Milosevic, alikuwa Rais wa zamani wa Serbia na Yugoslavia na alikuwa mtu mwenye ushawishi mkuu zaidi wa kisiasa kuwahi kufikishwa mbele ya ICTY. Alifariki tarehe 11 Machi 2006 wakati kesi yake ambapo alituhumiwa kwa mauaji ya kimbari au kushiriki katika mauaji ya kimbari katika maeneo ndani ya Bosnia na Herzegovina ilipokuwa ikiendelea, kwa hivyo hakuna uamuzi uliorudishwa. Mnamo mwaka wa 1995 ICTY ilitoa kibali kwa ajili ya kukamatwa kwa Wasabia wa Kibosnia Radovan Karadzic na Ratko Mladic kwa mashitaka kadhaa ikiwemo mauaji ya kimbari. Mnamo tarehe 21 Julai 2008 Karadzic alikamatwa Belgrade, na kwa sasa yuko katika gereza la Hague akisubiri kesi yake. Ratko Mladic bado hajakamatwa.

Kupitia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai

hariri

Hadi wa leo mashitaka yote ya kimataifa ya mauaji ya kimbari yamefanywa katika mahakama maalum ya kimataifa. Tangu mwaka 2002, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai yamepewa uwezo wa kushitaki kwa mujibu wa mamlaka yake ikiwa mahakama ya kitaifa hayana nia au hayawezi kuchunguza au kushitaka wahalifu wa mauaji ya kimbari, hivyo kufanywa kuwa "mahakama ya mwisho," na kuliachia mchi binafsi jukumu la kimsingi la kushtaki kwa mujibu wa mamlaka yake wanaodaiwa kuwa wahalifu. Kutokana na wasiwasi wa Marekani kuihusu ICC, Marekani inaonelea heri kuendelea kutumia mahakama ya kimataifa maalum kwa uchunguzi wa namna hiyo na mashitaka yatakayoibuka.[47]

Darfur, Sudan

hariri

Mgogoro unaoendelea katika eneo la Darfur, Sudan, ambao ulianza mwaka wa 2003, ulitangazwa kuwa "mauaji ya kimbari" na Katibu wa Nchi ya Marekani Colin Powell tarehe 9 Septemba, mnamo mwaka wa 2004 katika ushahidi mbele ya Kamati ya Seneti ya Uhusiano wa Nje.[48] Hata hivyo tangu wakati huo, hakuna mwanachama mwingine wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambaye ameufuata mfano huo. Kwa kweli, mnamo Januari mwaka wa 2005, Tume ya Kimataifa ya Uchunguzi wa Darfur, iliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Kimataifa Sheria nambari 1564 ya 2004, ilitoa taarifa kwa Katibu Mkuu ikisema kwamba "Serikali ya Sudan haijafuata sera ya mauaji ya kimbari." [49]

Hata hivyo, tume hiyo ilionya kwamba "hitimisho kwamba hakuna sera za uangamizaji zilizofuatwa na kutekelezwa katika eneo la Darfur na wenye mamlaka serikalini, moja kwa moja au kupitia wanamgambo chini ya udhibiti wake, haipaswi kueleweka kwa njia yoyote ile kama kutoashiria ukubwa wa hatia zilizofanywa katika kanda hiyo. Hatia za kimataifa kama vile hatia dhidi ya ubinadamu na hatia za kivita zilizofanywa katika eneo la Darfur zinaweza kuwa na uzito sawa na mauaji ya kimbari." [49]

Mnamo mwezi Machi mwaka wa 2005, Baraza la Usalama lilipeleka kirasmi swala la Darfur kwa mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, huku likiizingatia ripoti ya Tume lakini bila kuutaja uhalifu wowote maalum.[50] Wanachama wawili wa kudumu wa Baraza la Usalama, Umoja wa Marekani na Uchina, hawakupiga kura kuhusu azimio la sheria ya kushtaki.[51] Kwa mujibu wa ripoti yake ya nne kwa Baraza la Usalama, Mwendesha mashitaka amepata "uwezekano wa kuweko na misingi ya kuamini kwamba watu waliotambulishwa katika Sheria ya Baraza la Usalama la Umoja wa Kimataifa nambari 1593] wamefanya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita," lakini hakupata ushahidi wa kutosha kuwashitaki kwa mauaji ya kimbari.[52]

Mnamo Aprili mwaka wa 2007, Waamuzi wa ICC walitoa vibali vya kukamatwa kwa ya aliyekuwa Waziri wa Nchi kwa ajili ya Mambo ya Ndani, Ahmad Harun, na kiongozi wa wanamigambo wa Janjaweed, Ali Kushayb, kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.[53] Mnamo tarehe 14 Julai mwaka 2008, waendesha mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), waliyaandikisha mashtaka kumi ya uhalifu wa kivita dhidi ya Rais wa Sudan Omar al-Bashir: matatu ya makosa ya mauaji ya kimbari, matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na mawili ya mauaji. Waendesha mashitaka wa ICC wamedai kwamba al-Bashir "aliongoza upangaji na utekelezaji wa mpango wa kuharibu sehemu kuu" ya makundi tatu ya kikabila katika eneo la Darfur kwa sababu ya makabila yao.

Mnamo tarehe 4 Machi mwaka wa 2009 ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa Omar Al Bashir, Rais wa Sudan kadri Chumba cha utangulizi cha I cha ICC kilipohitimisha kuwa cheo chake kama mkuu wa nchi yake si kinga dhidi ya mashitaka mbele ya ICC. Hati ya kukamatwa ilikuwa kwa sababu ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Haikujumuisha uhalifu wa mauaji ya kimbari kwa sababu idadi kubwa ya waliokuwa katika Chumba cha utangulizi cha ICC hawakuona kama waendesha mashitaka walikuwa wametoa ushahidi wa kutosha kulijumuisha kosa hilo.[54]

Mauaji ya kimbari katika historia

hariri

Utangulizi wa CPPCG hausemi tu kuwa "mauaji ya kimbari ni kosa chini ya sheria za kimataifa, kinyume na roho na malengo ya Umoja wa Mataifa na linalokashifiwa na dunia iliyostaarabika", bali kwamba "katika vipindi vyote vya kihistoria mauaji ya kimbari yameleta hasara kuu kwa ubinadamu ".

Kuamua matukio ya kihistoria ambayo ni mauaji ya kimbari na ambayo ni tabia za kiuhalifu au unyama tu si jambo rahisi na wazi. Isitoshe, katika kesi zote ambapo shutuma za mauaji ya kimbari zimesambazwa, wanaotoka katika pande mbalimbali wanakana vikali tafsiri na maelezo ya tukio hilo, na hata mara nyingi huwa na maoni mbalimbali kuhusu ukweli. Mashitaka ya mauaji ya kimbari hayachukuliwi kimzaha na mara nyingi huzua utata. Majaribio ya wanaoangalia historia upya kuyakana mauaji ya kimbari (hasa mauaji ya kimbari ya Wayahudi) ni, katika nchi chache, kinyume na sheria.

Hatua za mauaji ya kimbari na juhudi za kuyazuia

hariri

Ili mauaji ya kimbari yatokee, mambo fulani yanafaa kuwepo. Kwanza kabisa ni utamaduni wa kitaifa ambao hauheshimu maisha ya kibinadamu inavyotakiwa. Jamii yenye uongozi wa kiimla, na itikadi zake zinazodaiwa kuwa bora kuliko zingine, ni jambo lingine linalofaa kuwepo kwa matendo ya mauaji ya kimbari kufanyika.[55]

Isitoshe, watu wa kundi linaloonekana kuwa na umuhimu mwingi lazima liwaangalie watu ambao huenda wakawa waathiriwa wa ukatili wao kama wao si binadamu kamili: kama “makafiri,” “watenda-unyama,” “watu ambayo hawajastaarabika,” “wasiomchamungu,” “waliokosa nidhamu,” “waliopingwa na miko,” “walio duni kirangi,” “watu wanaonuia kuharibu mpangilio wa kijamii,” “wanaopinga-mapinduzi,” na kadhalika.[56]

Hali hii pekee haitoshi kwa wahusika kufanya mauaji ya kimbari. Kufanya hivyo — yaani, kufanya mauaji ya kimbari — wahalifu wanahitaji wenye mamlaka wawe na nguvu na muungano na mpango wa ukiritimba na pia kuwe na watu wenye maradhi ya kiakili na wahalifu. Pia kampeni za wahusika za kuwawekea shutuma na kuwakosea utu waathiriwa zinahitajika, ambazo kwa kawaida huwa majimbo au serikali mpya zinazojaribu kulazimisha watu kuzifuata itikadi mpya na mipango yao ya kijamii.[57]

M. Hassan Kakar[58]

Mnamo mwaka wa 1996 Gregory Stanton rais wa shirika la kulinda dhidi ya mauaji ya kimbari aliwasilisha jarida kwa jina "Hatua 8 za mauaji ya kimbari" katika Idara ya Jimbo nchini Marekani.[59] Katika jarida hilo alipendekeza kuwa mauaji ya kimbari hufanyika katika hatua nane ambazo ni za "kutabiriwa lakini ambazo haziwezi kuepukika kikamilifu".[59][60]

Jarida la Stanton liliwasilishwa katika Idara ya Jimbo, muda mfupi baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda na uchambuzi mwingi umejikita katika sababu iliyoyafanya mauaji hayo ya kimbari kufanyika. Hatua ya kinga alizozipendekeza, kulingana na shabaha ya awali ya watu ambao utafiti huo ulilenga, zilikuwa zile ambazo Marekani ingeweza kutekeleza moja kwa moja au ingeweza, kwa kutumia ushawishi, wake kufanya serikali nyingine kutekeleza.

Hatua Sifa Hatua Zuilifu
1.
Uainishaji
Watu hugawanywa katika makundi ya "sisi na wao". "Hatua kuu zuilifu wakati huu wa mapema ni kuendeleza taasisi zitakazowafikia wote na ambazo zitapunguza ...utengano."
2.
Kufanya Mifano
"Ikijumuishwa na chuki, mifano inaweza kusukumwa kwa lazimi kwa wanachama wa vikundi vilivyotengwa ..." "Ili kukabiliana na kufanywa kwa mifano, mifano ya chuki inaweza kufanywa kuwa haramu kisheria hasa hotuba za chuki."
3.
Kunyima watu Utu
"Kundi moja linakana ubinadamu wa kundi lingine. Wanachama wa kundi hilo wanafananishwa na wanyama, viumbe viharibifu, wadudu au magonjwa. " "Viongozi wa nchi na wa kimataifa wanapaswa kushutumu matumizi ya hotuba za chuki na kufanya hotuba hizo zisikubalike kitamaduni. Viongozi wanaochochea mauaji ya kimbari wanafaa kupigwa marufuku wasisafiri kimataifa na wanafaa kunyimwa fedha walizohifadhi katika nchi geni."
4.
Mipangilio
"Mauaji ya kimbari daima hupangwa ...Vikundi maalum vya kijeshi au wanamgambo mara nyingi hupewa mafunzo na silaha ..." "Umoja wa Mataifa unapaswa kuanzisha vikwazo vya kisilaha dhidi ya serikali na raia wa nchi zinazoshiriki katika michafuko ya mauaji ya kimbari, na kuunda tume ili kuchunguza ukiukaji wa sheria"
5.
Ubaguzi
"Vikundi vya kueneza chuki hueneza matangazo ya kipropaganda yenye ubaguzi..." "Kuzuia kunaweza kumaanisha viongozi wa wastani kupewa ulinzi wa kisalama au msaada kwa vikundi vya haki za binadamu ...Upinduzi wa serikali na makundi haramu lazima yashutumiwe kupitia vikwazo vya kimataifa."
6.
Maandalizi
"Wahasiriwa hutambuliwa na kutengwa nje kwa sababu ya kabila au dini wanayojitambulisha nao..." "Katika hatua hii, ni lazima Hali ya Dharura dhidi ya Mauaji ya Kimbari itangazwe..."
7.
Uangamizaji
"Ni "uangamizaji" katika fikira za wauaji kwani hawaamini waathirika kuwa binadamu kamili." "Katika hatua hii, ni hatua ya dharura pekee yenye kutumia nguvu na silaha inayoweza kuyakomesha mauaji ya kimbari. Maeneo bayana ya salama au maeneo ya kuwawezesha wakimbizi kutorokea lazima yaundwe na yawe na ulinzi imara wa kimataifa wenye silaha."
8.
Kukana mauaji ya kimbari
"Wahalifu ... hukana kwamba walifanya uhalifu wowote ..." "Jibu la kukana ni adhabu kupitia mahakama ya kimataifa"

Katika jarida la Baraza la Utafiti wa Sayansi ya Jamii Dirk Moses anazikosoa mbinu za Stanton akihitimisha:

Kutokana na mazoea haya yasiyoridhisha katika kuyakomesha mauaji ya kimbari, swali linalofaa kuulizwani mbona dhana ya "masomo ya mauaji ya kimbari" ishindwe kutazamia na kukomesha mauaji ya kimbari kwa ufasaha wa kutegemewa. Dhana ya "masomo ya mauaji ya kimbari," hasa jinsi yanavyoendeshwa katika eneo la Marekani ya Kaskazini, yana nguvu na udhaifu. Ingawa ujasiri wa kimadili na mikakati ya umma inafaa kupongezwa, dhana yenyewe inaonekana pofu kimaana katika miradi ya kiimpiriali ambayo ni sehemu ya shida na pia sehemu ya suluhisho. Serikali ya Marekani iliita Darfur mauaji ya kimbari ili kuyafurahisha mashirika ya kindani yanayotetea haki, na kwa sababu matamshi hao hayana umuhimu wowote. Machafuko ya Darfur yatakamilika kwa wakati utakaozifaa nguvu kubwa ambazo zina mambo yatakayozifaidi katika kanda hiyo.

Dirk Moses[61]

Tume ya Utenda Kazi ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari

hariri

Mnamo Tarehe 8 Desemba mwaka wa 2008, tume ya utenda kazi ya kuzuia mauaji ya kimbari, iliyosimamiwa na Madeline Albright, Katibu Mkuu wa zamani wa Marekani kama wenyekiti msimamizi, na William Cohen, Katibu Mkuu wa zamani wa Ulinzi wa Marekani, ilitoa ripoti yake ya mwisho ambayo ilihitimisha kwamba serikali ya Marekani inaweza kuyazuia mauaji ya kimbari na ukatili mkubwa dhidi ya binadamu katika siku usoni.[62]

Katika mujibu wa maneno ya Bw. Kohen, “Ripoti hii inatoa mwongozo ambao unaweza kuiwezesha Marekani kuichukua hatua ya kuzuia, ikifanya kazi pamoja na washirika wa kimataifa, ili kuchelewesha mazingaombwe ya kesi za mauaji ya kimbari na visa vikubwa vya ukatili katika siku za usoni.”[63]

Kati ya mapendekezo ni:

  • jukumu la utendaji kwake rais wa Marekani ambalo litaonyesha Marekani na Dunia yote kwamba kuzuia mauaji ya kimbari na visa vikubwa vya ukatili ni kipaumbele cha taifa kitaifa
  • kuujenga mwili ndani ya Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani kuchambua vitisho na kuwaza juu ya hatua za kinga
  • kuanzisha mfuko wa dola milioni 250 wa kuizuia migogoro kuzuia na kukabiliana na machafuko
  • kusaidia kujenga mtandao wa kimataifa kwa ajili ya kubadilishana habari na uratibu wa hatua za kinga[64]

Angalia pia

hariri
 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 Office of the High Commissioner for Human Rights. Convention on the Prevention and Punishment of the Crime of Genocide
  2. Verdirame, Guglielmo "The Genocide Definition in the Jurisprudence of the Ad Hoc Tribunals", International & Comparative Law Quarterly (2000), 49 : 578-598 Cambridge University Press, doi:10.1017/S002058930006437X. Abstract Archived 4 Juni 2011 at the Wayback Machine.
  3. Naomi Klein. The Shock Doctrine: The Rise of Disaster Capitalism, Macmillan, 2007 ISBN 0-8050-7983-1, 9780805079838. p. 101, see footnote
  4. Oxford English Dictionary, second edition draft entry 2004. "genocide".
  5. Raphael Lemkin Axis Rule in Occupied Europe: Laws of Occupation - Analysis of Government - Proposals for Redress Chapter IX: Genocide a new term and new conception for destruction of nations, (Washington, D.C.: Carnegie Endowment for International Peace, 1944), pages 79 - 95
  6. 6.0 6.1 6.2 Raphael Lemkin - EuropeWorld, 22/6/2001
  7. "By 'genocide', we mean the destruction of a nation or of an ethnic group." Axis Rule in Occupied Europe, ix. 79. As quoted in the 3rd Oxford English Dictionary.
  8. Oxford English Dictionary "Genocide" citing Sunday Times 21 Oktoba 1945.
  9. Raphael Lemkin, Axis Rule in Occupied Europe (Wash., D.C.: Carnegie Endowment for International Peace, 1944), p. 79.
  10. Robert Gellately & Ben Kiernan (2003). The Specter of Genocide: Mass Murder in Historical Perspective. Cambridge, UK: Cambridge University Press. uk. 267. ISBN 0521527503.
  11. Staub, Ervin. The Roots of Evil: The Origins of Genocide and Other Group Violence. Cambridge, UK: Cambridge University Press. uk. 8. ISBN 0-521-42214-0.
  12. From a statement made by Mr. Morozov, representative of the Union of Soviet Socialist Republics, on 19 Aprili 1948 during the debate in the Ad Hoc Committee on Genocide (E/AC.25/SR.12).
  13. See Vienna Convention on the Law of Treaties, opened for signature on 23 Mei 1969, United Nations Treaty Series, vol. 1155, No. I-18232.
  14. Mandate, structure and methods of work: Genocide I Archived 21 Juni 2007 at the Wayback Machine. of the UN Commission of Experts Archived 13 Novemba 2007 at the Wayback Machine. to examine violations of international humanitarian law committed in the territory of the former Yugoslavia, created by Security Council resolution 780 (1992) of 6 Oktoba 1992.
  15. European Court of Human Rights Judgement in Jorgic v. Germany (Application no. 74613/01) paragraphs 18, 36,74
  16. European Court of Human Rights Judgement in Jorgic v. Germany (Application no. 74613/01) paragraphs 43-46
  17. What is Genocide? Archived 5 Mei 2007 at the Wayback Machine. McGill Faculty of Law (McGill University)
  18. Prosecutor v. Radislav Krstic - Trial Chamber I - Judgment - IT-98-33 (2001) ICTY8 (2 August 2001)
  19. 19.0 19.1 Prosecutor v. Radislav Krstic - Appeals Chamber - Judgment - IT-98-33 (2004) ICTY 7 (19 April 2004)
  20. Prosecutor v. Radislav Krstic - Appeals Chamber - Judgment - IT-98-33 (2004) ICTY 7 (19 April 2004) See Paragraph 6: "Article 4 of the Tribunal's Statute, like the Genocide Convention, covers certain acts done with "intent to destroy, in whole or in part, a national, ethnical, racial or religious group, as such."
  21. Statute of the International Tribunal for the Prosecution of Persons Responsible for Serious Violations of International Humanitarian Law Committed in the Territory of the Former Yugoslavia since 1991, U.N. Doc. S/25704 at 36, annex (1993) and S/25704/Add.1 (1993), adopted by Security Council on 25 Mei 1993, U.N. Doc. S/RES/827 (1993).
  22. "Resolution 1674 (2006)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-23. Iliwekwa mnamo 2009-12-26.
  23. William Schabas War crimes and human rights: essays on the death penalty, justice and accountability, Cameron May, 2008 ISBN 1-905017-63-4, 9781905017638. p. 791
  24. 24.0 24.1 Kurt Jonassohn & Karin Solveig Björnson, Genocide and Gross Human Rights Violations in Comparative Perspective: In Comparative Perspective, Transaction Publishers, 1998, ISBN 0-7658-0417-4, 9780765804174. pp. 133-135
  25. M. Hassan Kakar Afghanistan: The Soviet Invasion and the Afghan Response, 1979-1982 University of California press © 1995 The Regents of the University of California.
  26. M. Hassan Kakar 4. The Story of Genocide in Afghanistan: 13. Genocide Throughout the Country
  27. Frank Chalk, Kurt Jonassohn The History and Sociology of Genocide: Analyses and Case Studies, Yale University Press, 1990, ISBN 0-300-04446-1
  28. Jones, Adam. Genocide: A Comprehensive Introduction, Routledge/Taylor & Francis Publishers, 2006. ISBN 0-415-35385-8. Chapter 1: The Origins of Genocide Archived 10 Oktoba 2017 at the Wayback Machine. pp.20-21
  29. What is Genocide? Archived 5 Mei 2007 at the Wayback Machine. McGill Faculty of Law (McGill University) source cites Barbara Harff and Ted Gurr Toward empirical theory of genocides and politicides, International Studies Quarterly, 37:3, 1988
  30. Origins and Evolution of the Concept in the Science Encyclopedia by Net Industries. states "Politicide, as [Barbara] Harff and [Ted R.] Gurr define it, refers to the killing of groups of people who are targeted not because of shared ethnic or communal traits, but because of 'their hierarchical position or political opposition to the regime and dominant groups' (p. 360)". But does not give the book title to go with the page number.
  31. Staff. There are NO Statutes of Limitations on the Crimes of Genocide! Archived 28 Julai 2015 at the Wayback Machine. On the website of the American Patriot Friends Network. Cites Barbara Harff and Ted Gurr "Toward empirical theory of genocides and politicides," International Studies Quarterly 37, 3 [1988].
  32. Daniel D. Polsby and Don B. Kates, Jr. of Holocaust and gun control Archived 15 Januari 2008 at the Wayback Machine., Washington University Law Quarterly 1997, (Cite as 75 Wash. U. L.Q. 1237). Article cites Citing Barbara Harff, Recognizing Genocides and Politicides, in GENOCIDE WATCH 27 (Helen Fein ed., 1992) pp.37,38
  33. Domocide versus genocide; which is what?
  34. United Nations Treaty Collection (As of 9 October 2001): Convention on the Prevention and Punishment of the Crime of Genocide on the web site of the Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights
  35. (See for example the submission by Agent of the United States, Mr. David Andrews to the ICJ Public Sitting, 11 May 1999 Archived 17 Agosti 2007 at the Wayback Machine.)
  36. Oxford English Dictionary: 1944 R. Lemkin Axis Rule in Occupied Europe ix. 79 "By 'genocide' we mean the destruction of a nation or of an ethnic group."
  37. Oxford English Dictionary "Genocide" citing Sunday Times 21 Oktoba 1945
  38. These figures need revising they are from the ICTR page which says see www.ictr.org
  39. Staff. Bosnian genocide suspect extradited, BBC, 2 Aprili 2002
  40. European Court of Human Rights - Jorgic v. Germany Judgment, 12 Julai 2007. § 47
  41. The International Criminal Tribunal for the Former Yugoslavia found in Prosecutor v. Radislav Krstic - Trial Chamber I - Judgment - IT-98-33 (2001) ICTY8 (2 August 2001) that genocide had been committed. (see paragraph 560 for name of group in English on whom the genocide was committed). It was upheld in Prosecutor v. Radislav Krstic - Appeals Chamber - Judgment - IT-98-33 (2004) ICTY 7 (19 April 2004)
  42. "Courte: Serbia failed to prevent genocide, UN court rules". Associated Press. 2007-02-26. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-08-10. Iliwekwa mnamo 2021-01-17.
  43. ECHR Jorgic v. Germany. § 42 citing Prosecutor v. Krstic, IT-98-33-T, judgment of 2 Agosti 2001, §§ 580
  44. ECHR Jorgic v. Germany Judgment, 12 Julai 2007. § 44 citing Prosecutor v. Kupreskic and Others (IT-95-16-T, judgment of 14 Januari 2000), § 751. In 14 Januari 2000 the ICTY ruled in the Prosecutor v. Kupreskic and Others case that the killing of 116 Muslims in order to expel the Muslim population from a village, was persecution, not of genocide.
  45. ICJ press release 2007/8 Archived 13 Februari 2010 at the Wayback Machine. 26 Februari 2007
  46. ECHR Jorgic v. Germany Judgment, 12 Julai 2007. § 47
  47. Statement by Carolyn Willson, Minister Counselor for International Legal Affairs, on the Report of the ICC, in the UN General AssemblyPDF (123 KB) 23 Novemba 2005
  48. POWELL DECLARES KILLING IN DARFUR 'GENOCIDE' Archived 11 Septemba 2004 at the Wayback Machine., The NewsHour with Jim Lehrer, 9 Septemba 2004
  49. 49.0 49.1 Report of the International Commission of Inquiry on Darfur to the United Nations Secretary-GeneralPDF (1.14 MB), 25 Januari 2005, at 4
  50. Security Council Resolution 1593 (2005)PDF (24.8 KB)
  51. SECURITY COUNCIL REFERS SITUATION IN DARFUR, SUDAN, TO PROSECUTOR OF INTERNATIONAL CRIMINAL COURT, UN Press Release SC/8351, 31 Machi 2005
  52. Fourth Report of the Prosecutor of the International Criminal Court, to the Security Council pursuant to UNSC 1593 (2005)PDF (597 KB), Office of the Prosecutor of the International Criminal Court, 14 Desemba 2006.
  53. Statement by Mr. Luis Moreno Ocampo, Prosecutor of the International Criminal Court, to the United Nations Security Council pursuant to UNSCR 1593 (2005), International Criminal Court, 5 Juni 2008
  54. ICC issues a warrant of arrest for Omar Al Bashir, President of Sudan (ICC-CPI-20090304-PR394), ICC press release, 4 Machi 2009
  55. M. Hassan Kakar References Chapter 4. The Story of Genocide in Afghanistan Footnote 9. Citing Horowitz, quoted in Chalk and Jonassohn, Genocide, 14.
  56. M. Hassan Kakar References Chapter 4. The Story of Genocide in Afghanistan Footnote 10. Citing For details, see Carlton, War and Ideology.
  57. M. Hassan Kakar References Chapter 4. The Story of Genocide in Afghanistan Footnote 11. Citing Horowitz, quoted in Chalk and Jonassohn, Genocide, 13.
  58. M. Hassan Kakar , ,Afghanistan: The Soviet Invasion and the Afghan Response, 1979–1982, University of California Press, 1995.
  59. 59.0 59.1 Gregory Stanton. The 8 Stages of Genocide, Genocide Watch, 1996
  60. The FBI has found somewhat similar stages for hate groups.
  61. Dirk Moses Why the Discipline of "Genocide Studies" Has Trouble Explaining How Genocides End? Archived 18 Oktoba 2017 at the Wayback Machine., Social Science Research Council, 22 Desemba 2006
  62. Christian Science Monitor 9 December 2008
  63. "PGTF press release". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-09. Iliwekwa mnamo 2009-12-26.
  64. Report of the Prevention of Genocide Task Force Archived 9 Mei 2009 at the Wayback Machine. pp. 111-114

Marejeo

hariri

Marejeleo zaidi

hariri
Books
Muhtasari
Rasilimali
Mipango ya Utafiti