Majadiliano:Mpui

Latest comment: miaka 9 iliyopita by Baba Tabita in topic habari kuhusu kijiji cha Ilembo

habari kuhusu kijiji cha Ilembo

hariri

Tarehe 5 Septemba 2015, mtumiaji asiyejisajili aliongeza habari zifuatazo:

1.KIJIJI CHA ILEMBO. Ilembo ni kijiji kilichopo kata ya Mpui wilaya Sumbawanga Vijijini. shughuli kubwa au uchumi wa kijiji cha Ilembo hutegemea KILIMO na UFUGAJI. wakazi wa kijiji hiki ni WAFIPA na baadhi ya wakazi wa makabila tofauti wanaokwenda Ilembo hasa kwa shughuli za kiuchumi na kilimo pia. wakazi wa kijiji hiki wakarimu. wakazi hawa wamezungukwa na vivutio vingi ambavyo ni vyanzo vya uchumi pia Baadhi ya vivutio vya kijiji cha ILEMBO ni bwawa la MASOLA linalotumiwa kwa shughuli za Uvuvi na kilimo cha bustani, vilima na misitu asili ya YUNGA, mto NYINARUZI ambao wananchi hunufaika nao hasa kwa kilimo cha kiangazi kwa umwagiliaji 'MANTAKIA' na MISITU ya KUPANDWA inayovutia na kuzidi kuwapa neema wananchi wa Ilembo. Mazao yapatikanayo ILEMBO ni mahindi,maharage,ulezi,karanga pia miwa hulimwa katika bonde la nyinaruzi. mbali na kuwa na vyanzo vizuri lakini wakazi wa ilembo wanakabiliwa na kero mbalimbali kama ifuatavyo . Ukosefu wa miundombinu bora ya kukidhi shughuli zao,Afya,na kero nyingine nyingi.

Hali ilivyo haifai kuingizwa, tena alifuta habari nyingine za kata ya Mpui. Nimehifadhi habari zake humo kwa sasa. --Baba Tabita (majadiliano) 08:00, 6 Septemba 2015 (UTC)Reply

Rudi kwenye ukurasa wa " Mpui ".