Majadiliano:Uvinza
Haya ni Majadiliano kwa ajili ya kuboresha makala ya Uvinza. | |||
---|---|---|---|
|
|
Hii ni makala ya Uvinza ipo katika eneo la Wikipedia:Mradi wa Tanzania, juhudi za pamoja katika kuboresha maeneo ya Tanzania kwenye Wikipedia. Iwapo utapenda kushiriki, tafadhali tembelea ukurasa wa mradi, ambapo unaweza kujiunga na majadiliano na utazame orodha ya kazi zilizo wazi. |
JE, NI WAPI PANGEFAA ZAIDI KUWA MAKAO MAKUU YA WILAYA MPYA UVINZA: LUGUFU AU KIBAONI UVINZA
haririKWANINI TUNATOA PINGAMIZI:
MAKAO MAKUU YA WILAYA YA UVINZA KUWA LUGUFU :
1. Utangulizi: Tofauti na maeneo mengine yaliyotengwa kuwekwa majengo ya utawala wa makambi ya wakimbizi katika mkoa wa Kigoma ( Kasulu mjini karibu na ofisi za halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, maofisi ya serikali pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya, Kibondo mjini: maeneo yaliyo mjini na karibu kabisa na shughuli zote za kiserikali na kibiashara Makere mjini kwa madhumuni hayohayo kwamba makambi yakawepo mbali na ofisi za kiutawala ili watakapoondoka wakimbizi majengo yangetumika kwa manufaa ya miji ya wilaya ambazo makambi yalikiwepo) UVINZA: Mambo yalikuwa tofauti MAJENGO YALIYORITHIWA yaliyokuwa ya mradi ulioshindikana wa ufugaji wa ng’ombe kwa kukosekana maji na eneo la kuaminika la kuchunguia (Lugufu Heifer Project) yaliyo katika sehemu isiokalika na binadamu yaliteuliwa na hata pale wana Uvinza na baadhi ya mashirika yaliyokuwa yakihudumia wakimbizi walipolalamika na kuteua sehemu ambayo inaitwa hivi sasa KIBAONI kiongozi aliyekuwepo wakati ule kwa sababu alizozijua mwenyewe alipinga na alilazimisha mahali hapo pasipo na tumaini la kukua na kuwa mji pawe na majengo ya utawala wa kambi ya wakimbizi.
Pamoja nakwamba infahamika bayana kuwa na ofisi za kiutawala kwenye makambi kuna madhara makubwa hasa pale makambi yanaposhambuliwa na au wakimbizi kugoma na kutaka kuwahujumu wanao wahudumia kuwaokoa( evacuation) huwa haiwezekani lakini ushawishi wa kiongozi huyo ulishinda ingawa baadhi matokeo hasi kama yatakavyoonyeshwa hapa chini yalitokea; • Kulitokea na machafuko kambini ilitumika gharama kubwa na hali kubwa ya wasiwasi na misukosuko kuwaokoa (evacuate) wahudumiaji wageni na wenyenji. Hata hivyo viongozi wageni wa UNHCR WALIKODISHA MAJENGO YA MGODI WA CHUMVI Uvinza na kuwa wakitumia magari kwenda na kurudi, walihamia huko miaka mingi baadaye. • Palikuwepo na gharama kubwa ya kuweka mfumo wa maji kwa wakimbizi na wanaohudumia. Pamoja na kuwa huo ulikuwa ni mradi unafadhiliwa 100% na UNHCR na wafadhili wengine wa kimataifa, gharama ilikuwa kubwa mno hata wakashindwa kabisa kumudu kuendelea na mradi wa maji safi kutoka mto Malagarasi wakalazimka kuchimba visima karibu na makambi ambavyo, hata hivyo gharama zake zikawa kubwa pia kwani ukiachilia mbali gharama za uwekaji miundo mbinu, ukarabati na ukarafaki wake, za mfumo huo wa maji mafuta ya kuendelesha mitambo ya mfumo huo ilikuwa ni takriban lita 10,000 kwa mwezi! • Hayo ni machache, yapo mengi; lakini gharama nyingine nyingi ziliambatana na umbali toka Lugufu kuelekea Uvinza kulikokuwa kunapatikana huduma kwa wahudumiaji. Lakini kikubwa ni mazingira ya kijamii-kisaikolojia • ( psycho-social environment) ilyopo ya wahumiaji ambao hawana uhakika wa kile cha usalama wao na wengi kama sio wote hawakua na familia zao wala mali zao. Hii ndiyo hali yakuhudumia wakimbizi.
Hayo ndiyo mazingira ambayo TUMEYARITHI kutoka kituo cha kuhudumia wakimbizi ambayo yanaonekana muafaka kutumia kituo hicho kuwa makao makuu ya wilaya mpya ya Uvinza?? Inaaminika kuwa hivi sasa hakuna mkono wa Yule kiongozi aliyelazimisha kuwepo kwa kituo cha kuhudumia wakimbizi kwenye mahame ya mradi wa ng’ombe lakini ni hisia kuwa ||legacy” yake inatumika kuaanzishia makao makuu ya wilaya kwenye eneo hatrishi lililowapa matatizo mengi ya waliokuwa wakiwahudumia wakimbizi.
Zama hizo palikuwepo na wakimbizi makambini hivi sasa hakuna watu wala makazi katika makambi ya wakimbizi. Mchakato mzima wa kuweka makao makuu Lugufu katika mazingira hakika yaliyotajwa unajiweka wenyewe katika kile waingereza wanachokiita “PANDORA’S BOX” na hivyo kutarajiwe kuanzishwa kwa mlolongo wa matatizo magumu yasiyo sababu wala ulazima wa kushughulikiwa kama yale yaliyoleta shida na adha kati ya makao makuu ya wilaya ya Igunga kuwa Nanga badala ya Igunga yenyewe. Yalihamia Igunga na yapo huko na maji yanatoka mMwanzugi!
2. UVINZA PANAFAA KUWA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA UVINZA.
Mazingira muafaka: Uvinza ni mji mkongwe ambao una historoa iliyoanzia KARNE YA SITA pakiwa na migodi kadhaa ya chumvi ya kienyeji. Panapo mwaka wa 1896 wajerumani walianzisha mgodi wa kisasa wa chumvi wa chumvi ambao upo mpaka leo (2011). Pia walianzisha makao makuu ya utawala yaliyoitwa “Rudschugi Posten”
Mamlaka zilizopita hazikuweka program thabiti ya kuuendeleza mji wa Uvinza na hivyo kuuweka kwenye chati. Lakini hiyo sio hadithi yapo ya msingi wilaya ya Kasulu ilianzishwa kutoka Uvinza mwaka 1910 na ile ya wajerumani iliyoitwa wilaya ya UDJIDJI sasa Kigoma mwaka 1896 cha ajabu inwezekana na iaminike kuwa sehemu zilipoanzishiwa wilaya hizo panaitwa “Rutschugi Posten” au “Urvinsa” au “Uwinsa” - Pwaga karibu sana na Kibaoni mahali ambapo Halmashauri ya wilaya ya Kigoma imejenga kituo cha Afya (Hospitali ya wilaya tarajiwa), kituo cha vijana na Ruchugi Sekondari. Maeneo ni makubwa mno na maji yapo karibu mita 30 tu. Pia wakazi zaidi ya 28,000 katika mazingira yanayozunguuka wapo wakazi zaidi ya 150,000 kwenye vijiji viavyouzunguuka ‘Mji mdogo’ wa Uvinza na kuwa na mkabala muafaka wa kitovu kichocheo cha maendeleo.
Zipo shule za msingi 6 moja katika yazo ikiwa ni shule ya msingi maalum. Zipo shule za Sekondari mbili na ipo High school inayojengwa na asasi isiyo ya kiserikali EHENA. Ukiachilia mbali kituo cha afya kilichotajwa zipo zahanati tatu na pia yapo maduka kadha ya madawa ya binadamu na mifugo pia soko kubwa lenye maduka ya vifaa vya ujenzi na nguo na vyakula. Ipo migodi takriban mitatu na kituo kinacho endelezeka cha utalii cha sokwe zipo nyumba za kulala wageni zaidi ya sita, nyumba za vinywaji, mahoteli na pia upo uwezekano wa kufanyika zaidi ya hayo na upo uwezekano wa nyingine nyingi kuanzishwa.Zipo nyumba za ibada makanisa na misikiti pia upo uwezekano wa kuanzishwa synagogue,
Ipo ofisi ya posta na minara ya simu zote, kiwanja cha ndege, kituo cha reli na ndiyo makutanio ya barabara itokayo Cape Town kwenda Cairo barabara ambazo zinaunganisha mikoa takriban yote ya Tanzania kitovu chake ni mji wa Uvinza.
Lakini kikubwa kupita yote, Uvinza ndiyo Babeli (Babylon) pekee ya nchi ya Tanzania : mji uliopo kati kati ya mito miwili Tigris ( Ruchugi) Euphrates (Malagarasi) ipo fursa ya kupatikana kwa maji ya ya kutega kutoka maporomoko ya mito hiyo .
Hapapasiki kupuuzwa Uvinza kwa vile ndiyo mahali pekee katika iliyokuwa ‘Western Province’ penye kiwanda kikongwe na kiwanda pekee kilicho hai mpaka hivi leo. Na kinachoweza kuendelezwa na kukuzwa kwa sekta ya madini ambayo si chuma.
3. HITIMISHO:
Maelezo ya kisayansi muafaka yaliotolewa katika pingamizi hili yamebainisha hasara kubwa ya kun’gan’gania kuweka makao makuu ya wilaya kwenye iliyokuwa kambi ya wakimbizi Lugufu . Matumaini makubbwa sana ni kwamba yameeleweka vema kwetu sote na kwa faida na mustakabali wan chi yetu inayoongozwa na chama cha mapinduzi kilichosikivu sana. Mheshimwa Kikwete mara nyingi hurejea usemi kwamba “Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni” Hakuna tija hata moja kwa umma wa watanzania kuweka makao makuu ya wilaya ya Uvinza hapo Lugufu bali ni kuleta adha kubwa na usumbufu usio wa lazima kwa wananchi wa wilaya hiyo maridhawa mpya ambayo hata hivyo imechelewa kuwepo hapo tangu karne ya 6 hadi hapo 1896 wajerumani walipoanzisha “Rudschugi Posten” kwenye mlima unaotazama mto wa Ruchugi. Wajerumani nao walihamisha makao makuu kuyapeleka ‘Udjidji’ 1896 na Kasulu 1910 (Sutton and Roberts 1964) walifanya hivyo kwa minajili ya kudhibiti nguvu kazi vibarua na pia biashara ya Utumwa wa kizamani misafara yake ilipitia Uvinza (Kalufya,A.M. UDSM 1982) soko kuu la watumwa lilikuwepo Ujiji na hivyo kuufanya mji mdogo wa Uvinza kuwa ni Kambi tu la kutunza vibarua waliouza nguvu kazi zao si mahali pengine zaidi ya mgodi wa chumvi pakapewa jina Kimalampamba (sehemu ambayo ukienda na posho utaimaliza kabla ya kukudhi lengo lililokupeleka!
Uvinza ilipewa hadhi ya mji mdogo tangu mwaka 1974 lakini hakuna kikubwa kilichochuliwa zaidi ya kuirudisha kuwa kijiji chini ya sheria ya Vijiji na vijiji vya ujamaa na baadaye kuelezwa tena kuwa mji mdogo kwa kupanua upimaji na ramani bila mpango wa ziada wa kuikuza. Uvinza ikuwe lini kama si kwa kupanuliwa na kuwa makao makuu ya wilaya na kukuzwa kwa sekta ya madini chumvi na mengine na ukuaji na hadhi ya mji mdogo wa Uvinza. Inawezekana. Wawekezaji wa kilimo waendelee huko Lugufu na mabaki ya makambi ya wakimbizi yaendelezwe kuwa makambi hata yakiwa ni makambi ya upanuzi wa Jeshi la Kujenga Taifa Bulombola likiungana na wawekezaji. Uvinza ipewe haki na hadhi yake ya kuwa makao makuu ya Wilaya. Yapo majengo ya kuanzia na mahali penye hadhi pa kuishi watanzania hapo Uvinza. Inaaminika sana serikali ya awamu ya nne haiyumkiniki kuonekana inakubaliana na viongozi wanaopenda kuendeleza ‘legacy’ ya ‘alienation’ iliyoanzishwa na wakoloni na kufikiriwa kundelezwa nyakati na zama hizi za utandawazi.
Kwa heshima na taadhima kubwa ombi la pingamizi la makao makuu ya wilaya ya Uvinza kuwa Lugufu linaletwa mbele yako na mapendekezo ya Kibaoni- Uvinza kuwa makao makuu ya wilaya ya Uvinza yanawakilishwa..
Ni sisi hapa chini tumeweka majina sahihi na namba zeu za simu.
Kutokana na hari halisi makao ya wilaya ya uviza yapelekwe nguruka kutokana na kubwa wa mji,population ya kutosha iliyoko nguruka kigezo cha mjengo ya kambi ya lugufu sicho kwa sababu kweni wilaya zote zinazo anzishwa zina mjengo ya wakimbizi?kitengo huwa kinawekwa na selekari kwa kuanzisha wilaya hivyo kigezo hicho ni uswahili mtupu,wilaya ibaki ya kigoma vijijini na mpya uvinza makao makuu nguruka vijiji vya mgambo,sunuka,ilagara na vingine vyote vibaki wilaya ya kigoma vijini kupunguza usumbufu wa wananchi
Asalamu alyekum ndungu zangu
Aammm mimi kwa upande wangu naona bilashaka kabisa hakuna haja wala hoja ya msingi kwanini makao makuu ya wilaya mpya ya uvinza kupelekwa lUGUFU nafikili walio kubali kuipeleka huko hawakuwahi kujua maisha halisi ya lugufu yalivyo magumu kwa walio wahi kufanya kazi lugufu ya kuhudumia wakimbizi jambo ambalo hata leo hii ukiwatafuta hupati taabu kuwaona kwamana walitoka pande zote ya Tanzania labda tuangalie mambo muhimu
LUGUFU
hii nikweli kabisa iliwahi kuwa sehemu ya ufugaji n'gombe miaka ya nyuma lakini mladi ulikufa kutokana na mazingira magumu kwa maisha ya binadamu na mifungo yenyewe hasa ukizingatia upatikanaji wa maji ilikuwa tatizo kubwa sana kwa wafanya kazi serekali ilitumia pesa nyingi kuandaa mradi ila mwishoni ilishindikana kumudu ghalama za uendeshaji na kuacha majengo na miundo mbinu yote kufa bila mafanikio hili sio tatizo kwa mbunifu wa mradi hapana kwani katika uchumi miladi kama hii huitwa (Tembo Mweupe)
kwani namini mbunifu alijali ukubwa wa eneo tu,linalo izunguka ligufu ila hakujali wafanya kazi watapata wapi huduma za msingi kwa mwanadamu hali iliyo kuwa changamoto kwa wakati ule kwani usafili hasa ulio tegemewa ulikuwa wa njia ya reli hivyo wali lazimika kusafili kufuata huduma mbali na kuludi kazini kwa muda wa uhai wa mradi
Kwa mara ya pili jambo lile lile lilijitokeza pale walipo letwa wakimbizi kwasababu lilikuwa jambo linalo hitaji msaada wa haraka hivyo kwa kufuata kigezo chu ukubwa wa eneo linalo izunguka Lugufu pia ikaoneka wapewe hifadhi pale kwasababu wakimbizi sio wakazi wa kudumu pia hawakuwa wakimbizi wa muda mrefu hivyo ikapitishwa waishi mahali hapo sababu walikuwa ni watu wanao hitaji msada hawakuwa na chaguo wao popote paliwafa kwa ni (Mgonjwa hlii kunoga) tuliofika Lugufu ya wakimbizi mwanzoni tuliyaona maisha yao sipendi kueleza maisha yao ila siwezi kusahau mateso ya wadudu aina ya inzi waitwao ndorobo walivyo kuwa wakisubua
swala la maji lilikuwa tatizo sugu kwa wafanyakazi walio jitolea kuwasaidi kutoa huduma za kijamii kwa nduguzetu toka Kongo sababu ilikuwa ni swala la umoja wa mataifa walijitahi kadili walivyo weza ila mara nyingi wakimbizi walipata taabu sana ya maji ila hawakuwa na chaguo isipokuwa kuvumilia maisha na mara ya mwisho walichimbiwa visima amabavyo havikuweza kukidhi haja ya maisha yao
UVINZA
Nimji wa siku nyingi ulio na sifa nyingi naulio kuwa ukivutia wafanya biashara toka sehemu mbalimbali ya tanzania watu wengi walifika uvinza kwa minajiri ya kufanya biashara au kufanya kazi kwenye mgodi wa chunvi maisha ya wanauvinza yalikuwa mazuri na yenye kuvutia kwa miaka mingi watu wa mataifa mbalimbali walifanya maisha yao uvinza toka miaka hiyo ya MAMDARI hadi mwishoni ya miaka ya tisini ndipo maisha ya uvinza yalianza kubadilika kuwa magumu nakufanya wahindi na warabu walioishi uvinza kukimbilia sehemu nyingine zikiwemo Rukwa na Kigoma mjini
hivyo wana uvinza walipo ambiwa sasa umechaguliwa kupewa hadhi ya wilaya waliami huu ni wakati muafaka kwa ukombozi wao na ninakumbuka iliwahi kuwa moja ya ahadi iliyo wahi kutolewa na Mbunge aliye dumu ka mda mrefu sana alituambi sasa naongea na Raisi wa awamu ya Tatu aweze kuipa uvinza hadhi ya milaya yulimwami na tulitumaini mengi endapo uvinza itakapopewa rasimi hazi yake iliyo isubili kwa miaka mingi kuwa wilaya
WILAYA
Nihadhi inayo pewa sehemu wanapo ishi wana damu kulingana na kufikisha idadi furani ya wakazi na kufikia chanzo kikubwa cha pato la serekali kwa sehemu husika hivyo serekali hubolesha huduma kwa watu husuka wa sehemu hiyo hivyo uvinza ilionekana inahaja ya kupewa pongezi hizi toka serekali ya awamu ya tatu ndio maana hata Mbunge wa wakati ule ilikuwa moja ya ahadizake kwa wana uvinza sasa uboleshaji wa huduma hufaniwa wakazi wa sehemu husika na sio aridhi iliyo ukiwa cha kujiuliza walio kubaliana kupeleka MAKAO MAKUU YA WILAYA MPYA YA UVINZA LUGUFU je nawao walifuata mazingatio yaleyale ya bwana n'gomge kufuata ukubwa wa eneo linalo izunguka LUGUFU na mradi kuishia patupu? au walifuata nini huko kusiko na haja
kama kanuni na misingi ni ilele ya kupeleka au kuboresha huduma kwa ngazi ya wilaya sasa aliye boleshewa ni nani majengo yaliyo achwa na wkimbizi, eneo linalo izunguka Lugufu au wna UVINZA? kama ni kwawana uvina basi wapewe haki yao tuonomba WILWYA ikae uvinza kwani wotu tuna fahamu mkuu wa ulizi katika wilaya husuka ni MKUU WA WILAYA sasa inakuwaje akawekewa ofisi kilometa 30 kotoka uvinza hivi msada wake utakuwa nini kwa wana uvinza kwa bila kuwepo wakazi yeye asinge letwa basi nivizuri akishi hata kilometa 5 kutoka uvinza Hivyo swala la aridhi isiwe kisingizio kwambwa uvinza haina maeneo ya kutosha kujenga ofisi za taasisi ya wilwya sio kweli kwani kutokana na sheria ya Aridhi Tazania aridhi ni mali ya serekali hivyo endapo serekali itahihaji aridhi yake haiwezi kukosa kwa kufuata taratibu zilizo wekwa na serekali jamani MAKAO MAKUU YA WILAYA YAWE UVINZA NA SIO LUGUFU abdallah said msahala abdalla.said@hotmail.com 0764 15 18 29
Ushauli
haririMIMI NAFIKIRIA MAKAO MAKUU YA WILAYA HII IWE LUGUFU