Majadiliano:Vudee

Latest comment: miaka 6 iliyopita by Nelson Japhet Mtoru in topic Tutunze Mazingira Yatutunze

Tutunze Mazingira Yatutunze hariri

Ndugu zangu wana Same wenzangu kutoka kwenye kata yoyote kati ya kata 32 zilizopo kwenye wilaya yetu ya same ningependa kuwaomba tuwa sisitize viongozi wetu pamoja na nduguzetu swala la uoteshaji wa miti na utunzwaji wa vyanzo vya maji. Hata ikiwezekana miti mitano mitano kwa kila kaya kwani niwajibu wetu sisi kwapamoja kuyatunza mazingira yetu. Swala la mabadiliko ya tabia ya nchi niswala ambalo tunalishuhudia kwani hali ya hewa ya mazingira yetu tunayoishi imebadilika sio kama zamani na hii imesababishwa na ongezeko la watu, uvunaji wa miti bila kuotesha mingine, uchomaji wa misitu pamoja na uharibifu wa vyanzo vya maji. Hivyo basi niwajibu wangu mimi na wewe kupaza sauti katika hili ndani ya wilaya yetu nanje ya wilaya kwamanufaa yetu na taifa kwa ujumla.naomba ushirikiano waku punde usomapo ujumbe huu. Nelson Japhet Mtoru (majadiliano) 14:05, 17 Agosti 2017 (UTC)Reply

Return to "Vudee" page.