Majadiliano ya Wikipedia:Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (Universal Code of Conduct)

Latest comment: miaka 4 iliyopita by Czeus25 Masele in topic Maswali ya Wikimedia Foundation

Karibu! Hapa ni mahala pa kutoa maoni yako kuhusu nia ya Shirika la Wikimedia Foundation kuanzisha Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Nidhamu.
(itasaidia kama unaweza kuweka kichwa juu ya mchango wako kwa kutumia alama za == KICHWA == ; ukijibu hoja lililotolewa weka nuktambili : kwenye nafasi ya kwanza ya mstari wako wa kwanza, hii inasaidia kupanda michango vizuri)

Maswali ya Wikimedia Foundation

hariri

Swali la Kwanza

hariri
Mambo gani ya unyanyasaji wa kitabia uliwahi kukumbana nayo katika utumiaji au uchangiaji katika miradi ya Wikimedia Foundation ambayo uliyaona kama ni changamoto kwako?(What are the major challenges that you ever faced with respect to behavioral issues in the projects?
  • andika hapa chini majibu/maoni yako kuhusu swali hilo
  • Tangu nilipoanza kushiriki shughuli mbalimbali za Wikimedia Foundation sijawahi kukumbana na unyanyasaji wa kitabia. MagoTech Tanzania 19:37, 6 Aprili 2020 (UTC)

Sijawahi kukutana na changamoto hiyo, labda kwavile ni mgeni kiasi hapa.

Swali la Pili

hariri
Una maoni gani juu ya kuanzishwa kwa MWONGOZO WA KIMATAIFA WA MWENENDO NA MAADILI/ Universal Code of Conduct [UCoC] utakaosaidia watu wote kujisikia huru katika kuchangia katika miradi ya Wikimedia Foundation?
  • andika hapa chini majibu/maoni yako kuhusu swali hilo
  • Sioni haja kwa upande wa swwiki. Tena kuna maswali nani ataamua ambayo hayakujibiwa. Tuko tofauti vile kati ya jumuiya za kilugha. Kla jumuiya iamue yenyewe.Kipala (majadiliano) 18:37, 12 Machi 2020 (UTC)Reply
  • 1.Ushauri uliopendekezwa wa ulimwengu wote unapaswa pia kwa njia ambayo inafaa katika tamaduni zote kwa sababu ikiwa sivyo kanuni za ulimwengu zote zitapendelea watu wengi kuliko vikundi vya wachache.
  • 2. Hapa misingi ya umri haijadiliwi mahali popote kwa sababu ya kuongezeka kwa utumiaji wa teknolojia lazima kuwe na sheria, kanuni ambazo zinalenga mwongozo wa watoto haswa kwa yaliyomo ambayo yamekadiriwa vurugu mfano, ngono, vita nk.Czeus25 Masele (majadiliano)
  • Kwa upande wangu naona kuna umuhimu sana juu ya kuwa na miongozi hii. Siku zote kuwa na miongozo inayomwongoza na kumlinda kila mtumiaja anapokuwa akishiriki shughuli flani na watu mbalimbali ni swala la muhimu sana, na humfanya mtu kujisikia huru na amani kushiriki, kwa maana anakuwa akijua kuwa kuna miongozo inayomlinda na kumwongoza.MagoTech Tanzania 19:42, 6 Aprili 2020 (UTC)

Swali la Tatu

hariri
Wewe binafsi unadhani vitu gani ungependa viwemo kwenye huo Mwongozo? (Things that you want to see in a Universal Code of Conduct [UCoC])

Swali la Nne

hariri
Vitu gani ambavyo kwa maoni yako unadhani VISIWEKWE kwenye huo Mwongozo? (Things that your community does not want to see in a UCoC.)
  • andika hapa chini majibu/maoni yako kuhusu swali hilo
  • Sipendi kuwa na mwongozo huo, tunao tayari ya kwetu (tunayoweza kuendeleza kama kuna haja..). Jambo muhimu tusiongeze ngazi za urasimu (bureaucracy) ndani ya wikimedia Kipala (majadiliano) 18:40, 12 Machi 2020 (UTC)Reply

Swali la Tano

hariri
Je, una swali, pendekezo, wazo, dukuduku, ushauri n.k kuhususiana na uanzishwaji wa Mwongozo huo ukizingatia ukizingatia hali ya mwenendo na maadili baina ya wachangiaji wa miradi ya Wikimedia Foundation? (Jisikie huru kusema chochote)
  • andika hapa chini majibu/maoni yako kuhusu swali hilo
  • ni vema kama kila mradi una kanuni zake zinazoeleweka na kutekelezwa. Kila mmoja anayeingia kutoka mradi tofauti aziangalie na kufuata. Kipala (majadiliano) 18:42, 12 Machi 2020 (UTC)Reply

Swali la Sita

hariri
Je wewe binafsi ulishawahi kukumbana/ au uliwahi shuhudia mtu mwingine akikumbana na jambo lolote la unyanyasaji wa kitabia lililokufanya ujisikie vibaya/ kuudhika wakati wa uchangiaji wa miradi ya Wikimedia? Kama NDIYO, ni lipi? (mf. mtumiaji/mhariri mwingine kukuambia kitu kwa lugha isiyofaa, kukuita jina lisilo faa, n.k)
  • andika hapa chini majibu/maoni yako kuhusu swali hilo
  • Tofauti na Swali la kwanza?? Ni lazima kila mmoja azoee kukusolewa bila kukasirika. Lakini hapa tuangalie mipaka inayoendana na tamaduni mbalimbaliKipala (majadiliano) 18:44, 12 Machi 2020 (UTC)Reply
  • Hapana sijawahi. MagoTech Tanzania 19:45, 6 Aprili 2020 (UTC)

Maoni ya nyongeza

hariri
  • Hapa unaruhusiwa kutoa maoni yako mengine ya nyongeza kuhusu kitu chochote kinachohusiana na miradi ya Wikimedia mfano: kuhusu Wikipedia ya Kiswahili

My general comment; is to have a guidelune wchich is short, simple inclusive with understandable language. Aristarik (majadiliano) 18:10, 22 Machi 2020 (UTC)Reply

Marejeo Mbalimbali Kuhusu Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili

hariri
  1. https://meta.wikimedia.org/wiki/Strategy/Wikimedia_movement/2018-20/Recommendations Mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na wanawikimedia kutoka jumuiya mbalimbali wakati wa majadiliano kuelekea kutimiza malengo ya mpango wa Wikimedia 2030
  2. https://meta.wikimedia.org/wiki/Wikimedia_Foundation_Board_noticeboard/February_2020_-_Board_of_Trustees_on_Movement_Strategy Maridhio ya bodi ya watendaji ya Wikimedia Foundation kuhusu kuanzishwa kwa Mwongozo wa kimataifa wa Mwenendo na Maadili
  3. https://meta.wikimedia.org/wiki/Universal_Code_of_Conduct Huu ni ukurasa katika meta unaoelezea kuhusu Universal Code of Conduct
  1. https://meta.wikimedia.org/wiki/Wikimedia_Community_User_Group_Tanzania/Universal_Code_of_Conduct Hapa utapata tafsiri ya Kiswahili kuhusu Universal Code of Conduct

Majadiliano kwenye orodha ya Whatsapp ya kundi la Dar es Salaam "Wikimedia Community User Group Tanzania"

hariri

(Kopi hii kutoka Whatsapp haionyeshi michango iliyorejelewa, hivyo utaangalia mantiki ya majibu)
[3/10, 15:54] AMtavangu (WMF) : Kingine kinachoendelea kwa sasa within Wikimedia Foundation movement ni "UNIVERSAL CODE OF CONDUCT". Sisi kama Jumuia ya wachangiaji wa Wikipedia ya Kiswahili na Kiingereza kutoka Tanzania, tunaombwa kutoa maoni yetu juu ya kuanzishwa kwa "Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Nidhamu" ="Universal Code of Conduct" a.k.a UCoC. Maelezo ya kwanini kuna wazo hilo yanapatikana hapa chini:-

There was a harassment Survey in 2015 which was open for participation from all Wikimedia projects. Of the 3,845 Wikimedia users who participated, 38% of the respondents could confidently recognize that they had been harassed, while 15% were unsure and 47% were confident that they had not been harassed. Similarly, 51% witnessed others being harassed, while 17% were unsure and 32% did not witness harassment.

Following that challenge, some wikimedians from different communities gave their recommendations that there should be a ‘’Universal Code of Conduct (UCoC) that will lay down basic guidelines for all Wikimedia projects users and contributors to ensure availability of safe space for all people to get involved into Wikimedia projects without any fear.

Currently WMF is on a process of community consultation so as to obtain their opinions on what they think about the implementation of ‘‘UNIVERSAL CODE OF CONDUCT (UCoC)’’

Hence you can participate in providing your opinions by filling below form through this link: https://forms.gle/bh7msd8PyffyXQiy5


[3/10, 16:09] AMtavangu (WMF) : I am a Universal Code of Conduct Facilitator kwa upande wa Swahili speaking community. Kwa swali lolote kuhusu Universal Code of Conduct waweza uliza humu kwa faida ya wote au inbox. Kazi yangu kubwa ni kukusanya maoni yetu sote na kuyawasilisha kitengo cha (Trust & Safety team) ili wayafanyie kazi yale tunayopendekeza. Hivyo nitaomba ushiriki wenu ili kama jumuiya tuwe na kauli kuhusu mpango huo. NOTE: Wakati wa kushiriki survey hii unaweza chagua kuto jitambulisha jina, cha msingi ni maoni tu. Unaweza kutoa maoni yako hapa: https://forms . gle/bh7msd8PyffyXQiy5
[3/10, 16:15] +255 78xxxxx56: Nzuri sanaa iyoo Mr.Tonny .. Waiting for event so much.
[3/10, 18:28] Kipala : Swali langu kuu : je tuna tatizo la uchokozi au uonevu kwenye swwiki? Kama iko, tunaweza kupata mifano?
[3/10, 18:29] Kipala : Binafsi sina nia ya kushiriki katika majadiliano ya enwiki. Upande wa swwiki ningeomba kwanza majadiliano yapelekwe mahali pake, panapofaa ni ukurasa wa Jumuiya wa swwiki. Sina uhakika kama kuna jambo. Maana lugha jinsi inavyoonyeshwa kwenye Harrassment Survey 2025 uk. 27 sijawahi kuona swwiki. Kama nimesahau tafadhali mnikumbushe.
[3/10, 19:08] MuddyB : Muhtasari wa lugha zao???
[3/10, 19:43] Kipala : Ziko. Kiingereza iko hapa https://en.m.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Etiquette
[3/10, 19:45] Kipala : Sw hapa https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Mwongozo_(Kumbuka)
[3/10, 19:46] Kipala : Nauliza kwako, Muddy: je unakumbuka mifano ya uchokozi (harassment) kwetu swwiki?
[3/10, 19:45] Kipala : Sw hapa https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Mwongozo_(Kumbuka)
[3/10, 19:46] Kipala : Nauliza kwako, Muddy: je unakumbuka mifano ya uchokozi (harassment) kwetu swwiki?
[3/10, 19:49] MuddyB : Tunaweza kuwa nayo, lakini si sawa na ENWIKI. Unaweza kutukana matusi mazito moyoni, hata kujiuliza mama yake aliyemzaa user fulani—kwanini alienda leba kutuletea shida hizi duniani. Huwa siwaelewi kabisaa!
[3/10, 21:08] Kipala : Najaribu kukumbuka. Uliwaona kweli kwetu swwiki?
[3/10, 21:28] MuddyB : Hapana!
[3/10, 21:30] Kipala : Sioni faida ya zoezi hili kuwa na kanuni moja kwa lugha zote za wikipedia. Kila jumuiya inapaswa kuamua ni nini inayoweza kuvumiliwa, ni nini ambayo haivumiliki.
[3/10, 21:31] MuddyB : Kweli kabisa. Kwani kuna global discussion juu ya kitu kimoja???
[3/10, 21:37] Kipala : Nikifuata majadiliano upande wa Wanawiki Wajerumani, wanahofia jaribio la WMF kuingilia zaidi ndani ya madaraka ya jumuiya za wanawikimedia. Maana kulikuwa na mfano wa mtumiaji mmoja aliyepigana na mwingine kwa maneno makali. Kamati ya enwiki ilimwonya lakini WMF waliingilia kati na kumbana kwa kipindikirefu. Hapa wanawikipedia wengi walipinga wakisema eti hapa WMF wanajaribu kujipatia madaraka ambayo si yao. Sasa wako wanaohofia kuna hatua inayofuata.
[3/10, 23:37] AMtavangu (WMF) : Asanteni sana wote mliochangia mjadala huu na watu zaidi wanakaribishwa kuendelea kuchangia waonavyo wao.Cha kukumbuka hapa ni kwamba chochote anachochangia mtu yeyote humu ndani au mahali pengine popote ni mawazo yake yeye binafsi na si msimamo wa watu wote. Hivyo huu ni mjadala uliowazi kabisa kwetu sote na kutofautiana kimtizamo ni kitu cha kawaida na kinategemewa, si lazima tukubaliane jambo moja, na hivyo watu wajisikie huru kabisa kusema maoni yao.

Kesho nitatolea maelezo zaidi kwa kila hoja iliyotolewa ili kujenga uelewa zaidi kwa kila mmoja wetu ili kutokea hapo mtu aweze kupata cha kuchangia kuhusu mjadala huu.
[3/10, 23:59] Kipala : Antoni, asante sana kwa kazi yako na jitihada kubwa za kutafsiri. Kama unatafuta pekee maoni ya kundi la Dar es Salaam, hii ni sawa. Kama unatafuta maoni yajumuiya ya Wikipedia ya Kiswahili, mahali pake si hapa tu, hasa na zaidi kwenye ukurasa wa jumuiya ya swwiki.
[3/11, 07:32] AMtavangu (WMF) : Asante sana Ingo kwa ushauri huo (ninalifanyia kazi na Nitakuja huko pia (katika ukurasa wa Jumuiya ya swwiki). Lengo ni kuwafikia watu wengi zaidi popote ambapo wapo active kutoa maoni yao.
[3/11, 11:24] AMtavangu (WMF) : Mara nyingi si rahisi kujua kama mtu ana tatizo flani hadi pale atakapopewa nafasi ya kujieleza, na chanagamoto anayopitia mtu A inaweza kuwa siyo ile anayoipata mtu B.Hivyo hivyo hii ndiyo sababu WMF wanatoa nafasi kwa watu kutoa maoni yao.
[3/11, 11:26] AMtavangu (WMF) : Asante kwa msimamo wako binafsi kuhusu enwiki. Sawa, kwa upande wa swwiki tutapeleka mjadala kule pia kujua watu wana maoni gani. Masahihisho kidogo kwenye sentensi yako hapa ‘’Harrassment Survey 2015 uk. 27’’ ni kwamba survey ilifanyika 2015. Kila mtu anayetaka anaweza ipitia pdf report ya survey hiyo hapa:(https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/5/52/Harassment_Survey_2015_-_Results_Report.pdf)
[3/11, 11:28] AMtavangu (WMF) : Ukusanyaji wa maoni haya haulengi swwiki na enwiki tu, bali miradi yote ya Wikimedia Foundation. Wanataka kujua ni namna gani watu wanajisikia wapo huru kuchangia katika miradi hiyo na namna wanavyojisikia wanaposhirikiana na wahariri wengine kutoka maeneo yote duniani.
[3/11, 11:30] AMtavangu (WMF) : Asante kwa kutushirikisha link hiyo. Ndiyo hii ni kwa english Wikipedia, na vivyo hivyo Wikipedia zingine zina sera zao za nini kinachukuliwa kuwa ni sawa na kipi kinachukuliwa kuwa si sawa kwa mujibu wa utamaduni wao. Swali ni je Waswahili tuna sera yetu tuliyotunga wenyewe kama wanawikipedia ya kiswahili? na kama ipo, watu wanafahamu hata uwepo wa hiyo sera?
[3/11, 11:32] AMtavangu (WMF) : Kwa upande wa Wikipedia ya Kiswahili sidhani kama tuna sera inayotuongoza (iliyotungwa na Wanawikipedia ya Kiswahili wenyewe) kutusimamia, kwa upande flani tumechukua baadhi ya miongozo na kuitafsiri kutoka Wikipedia ya Kiingereza na muda mwingine tunaonyana/kuelekezana tu kwa maandishi ndani na nje ya swwiki au kwa mdomo.(kama ipo hiyo sera kamili ya Waswahili wenyewe @Ingo na @Muddy mtanisahihisha hapa)
[3/11, 11:35] AMtavangu (WMF) : Hiki ndicho tunachokiongelea, watu wanajisikia huru kiasi gani kuchangia katika miradi bila woga au kinyongo kuwa huyu asije akasema hivi, asije akanitukana, asije sema mimi sijui, au akaniambia kitu fulani kitakachonifanya nijisikie vibaya sababu tu mimi ni A,B,C n.k
[3/11, 11:36] AMtavangu (WMF) : Kama hawapo itakuwa inapendeza, lakini bado kwa uhakika zaidi ni vema tukapeleka mjadala kule washirika wengine pia wakatoa maoni yao.Yawezekana kuna namna nyingine tofauti wanazopitia tofauti na ‘’harassment’’ za swwiki moja kwa moja kweli hakuna kabisa mambo kama hayo.
[3/11, 11:38] AMtavangu (WMF) : Asante kwa maoni binafsi. Kimsingi Universal Code of Conduct haina lengo la kufuta sera zilizopo za jumuia husika, bali kuunganisha maudhui yaliyomo kwenye hizo sera na kupata sera moja yenye hadhi ya kutumika na wanawikimedia wote. Moja ya faida zake ni kurahisisha namna ya kujiheshimu pale mwanawikipedia wa kutoka jumuia A anaposhirikiana na mwanajumuia B. Mfano, Waswahili ni kitu cha kawaida kusema ‘’Aisee sasa hivi umenenepa’’ na akafurahi akaendelea kula zaidi anenepe vizuri zaidi, lakini kitu hichohicho ukimwambia mwingine kutoka ufilipino anaweza chukulia maana tofauti na akasema ‘’umemtukana’’ nakadhalika. Nitatoa mifano hapo chini baadhi ya maneno watu walioshiriki katika hiyo survey ya 2015 ambayo walisema walijisikia kuwa wamefanyiwa ‘’harassmment’’
[3/11, 11:40] AMtavangu (WMF) : NDIYO. Kuhusu Universal Conduct kwa kiingereza unaweza soma hapa :https://meta.wikimedia.org/wiki/Universal_Code_of_Conduct na majadiliano yake mapana na maeefu kutoka kwa wanawikimedia mbalimbali yapo hapa: https://meta.wikimedia.org/wiki/Talk:Universal_Code_of_Conduct
[3/11, 11:42] AMtavangu (WMF) : Ni kweli mjadala ni mpana na kila mmoja ana maoni yake. Kwa kifupi ni kwamba baadhi ya watu wanataka kuwe na uhuru usio na mipaka wa ‘’freedom of expression” kwamba chochote wanaweza sema kwa mtu yeyote na kwa kutumia lugha ya aina yoyote iwe ni sawa tu na asitokee mtu wa kuwaambia waache kufanya hivyo. Hilo ndilo tatizo linalofanya wanawikimedia wengine kuacha kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia Foundation kwa kukwazwa na watu wengine. Tatizo hili pengine linaweza lisiwepo kwenye swahiliwiki, kakini ‘’mwenzio akinyolewa ,zako tia maji’’ na ikumbukwe kundi hili hatuchangii swwiki pekeyake. Ndiyo maana baadhi ya watu wakapendekeza kuwe na mwongozo wa kutusimamia kimataifa kuhusu namna tunavyoshirikiana na wengine.
[3/11, 11:47] AMtavangu (WMF) : Baadhi ya maneno watu waliyo ripoti kama ni harassment kutoka hapa (https://commons.wikimedia.org/w/index.php?title=File:Harassment_Survey_2015_-_Results_Report.pdf&page=2): ni “Your Writings are shit ! “, “Halt die Fresse, du Arschloch” (Shut up, you asshole) , “son of a bitch” , "I am going to kill your grandchildren" (How can you be such dishonorable and at the same time seem like a good and stupid person?), “You are a bigot who should be banned from Wikipedia” “With Jews you win”, “What entitles a feminized nebbish like you to delete a book that you haven't even read", “You're an old fart and so is your friend”
[3/11, 11:48] AMtavangu (WMF) : Nimejaribu kuelezea zaidi kwa kila hoja, mnakaribishwa kwa maoni zaidi
[3/11, 11:49] Kipala : Samahani lakini hapa unalenga mbali kidogo. Nikifuatilia majadaliano sijakuta mtu anataka kila aseme chochote. Kinyume chake kwenye miradi yote watu wanaotukana wanaonywa na wanabanwa. Swali linalojadiliwa ni: kwa nini isiendelee jinsi ilivyo? WMF ina kazi hapa? Ni dhahiri kwamba matatizo lazima kushughulikuwa ndani ya jumuiya, si katika ofisi pale Kalifornia. Wanajuaje kama kuna lugha isiyofaa inatumika kwa Kiswahili, Kikorea, Kitigrinya, Kisomali, Kitelugu?
[3/11, 11:50] Kipala : Sijaelewa bado kwa sababu gani mfumo uliopo unahitaji mabadiliko.
[3/11, 12:02] Kipala : Je yupo anayetetea lugha hii?
[3/11, 12:05] Kipala : Kama majadiliano yanalenga jumuiya ya Wikipedia ya Kiswahili, tafadhali yapelekwe huko yaani kurasa za swwiki. Nimeweka tangazo ukurasa wa jumuiya na kuandaa ukurasa wa pekee https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Mwongozo_wa_Kimataifa_wa_Mwenendo_na_Maadili_(Universal_Code_of_Conduct) Karibuni.
[3/11, 12:17] Kipala : Tunayo. Unaonaje hiyo iliyopo ndani ya Mwongozo imetokea wapi? Mwongozo tulio nao ulitungwa miaka kadhaa iliyopita. Kila mwanawikipedia mpya anashauriwa kuiangalia katika sanduku la "Karibu" linaloonekana kwenye ukurasa wake baada kujiandikisha.
[3/11, 12:49] AMtavangu (WMF) : Samahani lakini hapa unalenga mbali kidogo. ‘’Nikifuatilia majadaliano sijakuta mtu anataka kila aseme chochote. ‘’* _(Asante kwa marekebisho kuhusu ‘kusema chochote’. Nilitaka kumaanisha kuna changamoto ya tafsiri ya kipi kinatafsiriwa kuwa kinakubalika/ hakikubaliki kumwambia mwingine. Na kuna changamoto ya kuwa japokuwa watu wanaonywa wengine wanakuwa wabishi wanapoonywa (anaona kama yule anaye muonya admin au mtu mwingine yeyote hana mamlaka ya kumwambia vile na muda mwingine baadhi ya admins wa wiki husika hutumia vibaya haki zao za u admin kuwafanyia fujo wachangiaji wengine wasio na u admin._

  • ‘’Kinyume chake kwenye miradi yote watu wanaotukana wanaonywa na wanabanwa.’’*

_Hapa napo changamoto ipo kwenye kutukana. Ni rahisi kujua mtu ametukana unapokuwa mwenyeji wa jumuia husika. Tabu hutokea pale kunapokuwa na ‘’interaction’’ baina ya jumuiya mbili. Ni tabu sana kutafsiri kipi kinakubalika na kipi hakikubaliki (kimataifa). Jambo moja la kukumbuka hapa mwongozo huu haulengi kutatua tatizo la ‘’onwiki activities tu’’ bali hata ‘’off-wiki activities’’ baina ya wanawikimedia.mfano mikutano ya kikanda na kimataifa (regional na international conferences) ambapo wanawikipedia kutoka tamaduni tofauti wanakutana._

  • ‘’Swali linalojadiliwa ni: kwa nini isiendelee jinsi ilivyo? WMF ina kazi hapa?’’*

_Hapa hakuna ubaya wa kuendelea jinsi ilivyo ( na natumaini sera za jumuia husika zitaendelea kama kawaida
[nitawauliza]), isipokuwa kuna upungufu unaoonekana kwamba hakuna SERA JUMUISHI baina ya sera za jumuia zote itakayoweza kusaidia watu kuingiliana ‘’interact’’ katika nyanja ya kimataifa na si tu kama jumuia husika tu._

  • ‘’Ni dhahiri kwamba matatizo lazima kushughulikuwa ndani ya jumuiya, si katika ofisi pale Kalifornia.’’*

_Ni kweli, lakini pia ni dhahiri kuwa WMF kama shirika mama linalosimamia/Kuongoza miradi hiyo (jumuiya hizo) wana wajibu wa kuwezesha jumuiya hizo kwa kushirikiana na wao kutafuta suluhu ya matatizo yanayoripotiwa katika jumuiya na miradi mbalimbali ya WMF. Na ndio maana wazo hili la kuwa na Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Nidhamu haujaanzishwa na WMF bali na wikimedians wakati wa Wikimedia 2030: Community consultations, WMF board of Trustees wamefanya kuridhia tu na wazo hilo, na ndiyo maana kwa sasa mchakato uliopo ni kulipa wazo hilo nafasi ya kujadiliwa kwa kina na Jumuiya mbalimbali (ikiwemo ya kwetu) ili kupata mawazo yao zaidi._

  • Wanajuaje kama kuna lugha isiyofaa inatumika kwa Kiswahili, Kikorea, Kitigrinya, Kisomali, Kitelugu?*

_Watajua kwa kupitia maoni yanayotolewa na ‘’Waswahili, Wakorea. Wakitigrinya,Kisomali Kitelugu n.k’’ Kazi yao ni kutenengeneza tu mazingira ya jumuiya hizo mbalimbali zijadili kuhusu kipi wanakubaliana na kipi hawakubaliani kuwa nacho kama kitu cha pamoja kimataifa._


[3/11, 12:51] Kipala : Asante kwa majibu, pole na kazi nyingi. Ila si afadhali tuipeleke swwiki? Hapa tuko kwenye uwanja wa kundi tu.


[3/11, 12:52] AMtavangu (WMF) : kutokana na majibu ya utafiti hadi wakayataja maana yake yapo na yanafanyika, kuhusu uwepo wa wanaotetea ni swala lingine nitahitaji muda kidogo kufuatilia


[3/11, 12:54] AMtavangu (WMF) : ndiyo. Asante kwa kuanzisha ukurasa. Lakini hapa pia ni mojawapo ya uwanja ambao walengwa wapo. Ila kwa wanaoweza kutoa maoni yao moja kwa moja https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Mwongozo_wa_Kimataifa_wa_Mwenendo_na_Maadili_(Universal_Code_of_Conduct) ni vema pia.


[3/11, 12:56] Kipala : Bila shaka kundi hili kwa sasa ni sehemu ya jumuiya iliyo hai zaidi na kuwa na uwezo wa kuchangia mengi! Ila ni sehemu tu ya jumuiya, wengine wako nje.


[3/11, 12:56] AMtavangu (WMF) : Ni sahihi kabisa, Asante.


[3/11, 13:20] AMtavangu (WMF) : Asante, nafurahi kusikia tunayo na ilitungwa. Samahani, napenda tu kujua ilitungwa na Wanawikipedia ya Kiswahili wenyewe (yaani mawazo ya sera hiyo yalitoka vichwani mwao) au kama sivyo ilitungwa na nani, au baadhi tu ya ya sera kutoka Wikipedia nyingine(mf.enwiki) zilitafsiriwa kwenda kwenye Kiswahili na tuka adopt kuitumia, au ni mchanganyiko wa sera za kutohoa na za kwetu ?


[3/11, 20:27] Kipala : Ukiisoma utaona haikutafsiriwa ni hitimisho fupi ya mambo yanayoandikwa enwiki, pamoja na kurejelea ukurasa wa enwiki. Nikisoma majadiliano kwenye ukurasa wa Meta, nahisi kwamba msingi wa zoezi ni matatizo kwenye enwiki. Nimesoma mmoja aliyeandika pale dewiki mfumo upo lakini enwiki hakuna utaratibu mzuri unaofuatwa kama mtu anabanwa na kupinga, namna ya kuondoa ugomvi huu. Sijui kama ni vile au la. Ila tu kuna imani upande wa "Waingereza" hao wenyewe ni dunia yote ( na Waingereza na Wamarekani ni dhaifu kujua lugha zingine). Kumbe kama wana tatizo upande wao wanataka kutibu dunia yote.
[3/11, 21:41] AMtavangu (WMF) : Ni kweli, inaonesha hali ni mbaya zaidi kwa enwiki nadhani kinga ni bora kuliko tiba. hata Corona ilianzia Wuhan China lakini sasa ni global threat. Kwa vyovyote anachofanyiwa mmarekani katika Wiki platforms ni rahisi pia kufanyiwa Mtanzania kupitia platforms hizohizo. ndiyo maana wanajaribu kutafuta suluhu ya pamoja (angalau kwa vitu vichache tunavyofanana, maana itakuwa ngumu kuwa na mfumo utakaotibu kila aina ya mapungufu kwa kwa kila jumuiya) '

Swali la mifano

hariri

Nimeuliza juu kama kuna mifano ya uchokozi hapa sw. Kama imetajwa moja kwa moja kwa antoni, naomba tuone mifano (si lazima kitaja majina). Menginevyo sijaelewa bado haja ya "Global Code" kwa mawasiliano ya wanawikipedia kutoka makundi tofauti. Kama mtu kutoka enwiki anafika hapa, anatakiwa kufuata kawaida za hapa. Nikiingia enwiki, natakiwa kufuata mashariti na kawaida zao. Ukienda Commons, utawasiliana na maadmins wa Commons. Hii ni kawaida sijaelewa tatizo. Hapa naomba ufafanuzi kwa kutaja mifano halisi. Kipala (majadiliano) 22:33, 11 Machi 2020 (UTC)Reply

Rudi kwenye ukurasa wa mradi " Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (Universal Code of Conduct) ".