Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing they themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Translation request

hariri

Hello! May I ask you for a translation of the phrase Automatic refresh into Kiswahili? Thanks -XQV- (majadiliano) 21:31, 20 Juni 2018 (UTC)Reply

Habari! The translation of the phrase Automatic refresh is Onesha upya moja kwa moja Shukrani sana! Makangabila Clement (majadiliano) 17:17, 21 Juni 2018 (UTC)Reply

Mtumiaji:ChriKo

hariri

habari naona umesahihisha matini katika ukrasa wa ChriKo. Masahihisho haya ni sahihi. Lakini ka jumla hatuingii katika kurasa za watumiaji. Kila mmoja anajitambulisha jinsi anavyoona (na anavyoweza). Hii ni tofauti na makala anazotunga. Kipala (majadiliano) 05:39, 26 Novemba 2018 (UTC)Reply

Samahani sikua najua

hariri

Samahani mzee Kipala sikujua utaratibu huu. Czeus25 Masele (majadiliano)

Ngw'anamalundi (Mwanamalundi)

hariri

Naona tumehariri wakati mmoja, naomba uangalie tena kile ulichohariri mwishoni, inawezekana nimeiharibu kwa bahati mbaya. Niliingiza vyanzo vinavyopatikana google books na OUT. Kipala (majadiliano) 14:16, 4 Desemba 2018 (UTC)Reply

Sawa mzee nitaangalia Czeus25 Masele (majadiliano)

Samaki

hariri
 
Pezi
 
Mashavu ya jodari

Unaamini kweli samaki inavuta oksijeni kupitia mapezi?? Hii ingekuwa kazi ngumu mno, heri tumwachie mashavu!
ona Kamusi sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia (TUKI 20123)
gill arch n taoshavu kigegedu,kiungo maalum katika shavu la samaki kinachofanana na upinde, na ambacho hutegemeza vijishavu ambapo kubadilishana kwa oksijeni na dioksidi kaboni hutokea.
fin n pezi: kiungo katika wanyama wa inajini kama vile samaki ambacho hutokana na mkunjo wa ngozi na musuli uliotengenezwa na mifupa
TUKI English-Swahili dictionary gill n yavuyavu: shavu la samaki. Vt toa/tumbua mashavu (ya samaki) Kama ChriKo (PhD biolojia) ameshiriki katika makala, sijaona bado makosa mengi. Kipala (majadiliano) 18:29, 1 Machi 2020 (UTC)Reply

Tangazo

hariri

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 17:18, 5 Aprili 2020 (UTC)Reply

Kigezo: Picha ya wiki

hariri

 

Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. Spishi ya ng'ombe ina nususpishi au aina nyingi lakini ni spishi moja tu.

Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili. Asili yake ni aina za ng'ombe wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi nyingi anatumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.

Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga nas kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.

Picha

hariri

Asante kwa kuweka kumbukumbu hiyo ya warsha ya astronomia. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:30, 9 Aprili 2020 (UTC)Reply
Karibu. Czeus25 Masele (majadiliano) 09:48, 9 Aprili 2020 (UTC)Reply

Masanja

hariri

Kuna sababu ya kufuta picha ya V Masanja?Kipala (majadiliano) 19:24, 10 Aprili 2020 (UTC)Reply

Lugha za makabila ya Tanzania

hariri

Ndugu, hakuna haja ya kuanzisha jamii hiyo, inatosha ile ya lugha za Tanzania. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:05, 13 Aprili 2020 (UTC)Reply
Sawa Ndungu. Ahsante Czeus25 Masele (majadiliano) 07:26, 13 Aprili 2020 (UTC)Reply

Kukaribisha wageni

hariri

Asante kwa kushiriki katika kukaribisha wageni. Nashukuru ukiendelea. Ila tu usisahau kutia sahihi kwa kuingiza yafuatayo: {{karibu}}~~~~ . Sahihi yako ambayo ni sehemu ~~~~ inakuja pamoja na tarehe. Hii inatusaidia kujua baadaye ni lini kwamba mchangiaji amekaribishwa na kuelezwa kanuni zeti; ni msaada hasa tukilazimishwa kuchukua hatua dhidi ya mchangiaji: je aliweza kujua utaratibu kwa sababu amekaribishwa tayari au bado? Kipala (majadiliano) 23:27, 31 Julai 2020 (UTC)Reply

Ahsante sana Kipala, niliweza kujua utaratibu baada ya kufatilia mabadiliko ya karibuni hivyo niliona jinsi ya kukaribisha watu.Czeus25 Masele (majadiliano) 06:16, 7 Agosti 2020 (UTC)Reply

Salamu za "Karibu"

hariri

Uliweka salamu kwenye ukurasa wa Mtumiaji:Oparanya_harvey badala ya ukurasa wa majadiliano. Naomba uhakikishe unapoweka. Kipala (majadiliano) 22:54, 8 Septemba 2020 (UTC)Reply

Sawa, ahsante. Czeus25 Masele (majadiliano) 23:14, 8 Septemba 2020 (UTC)Reply

Hongera ya kazi

hariri

Naona jisi unavyopiga mbio siku hizi, hongera sana. Ila kwenye namna ya kutafsiri usifuate mfano wa Kiingereza neno-kwa-neno. Mfano hijabu ulichukua sehemu hii yote ya alama za kifonetiki kuhusu matamshi kwa Kiingereza, ambayo ni bure kidogo maana anayetaka kuona haya aangalie upande wa enwiki, si kwetu (isipokuwa labda kama matamshi ya Kiingereza isizo kawaida, inaweza kuwa na maana mara chache). Vilevile kwa karani umetafsiri "white collar" ambayo inaleta maana tofauti. Nani anavaa "kola" kwa Kiswahili? Hata kwa Kiingereza si maana asilia tena (kola kama sehemu ya vazi inayofungwa kwenye shati yako, jinsi ilivyo kwa wachungaji hadi leo, lakini nje ya magauni kadhaa ya wanawake "collar" yenyewe haipo tena) lakini inaeleweka kwa watu wanaofanya kazi ofisini kutokana na desturi ya zamani kubadilisha ile "kola nyeupe" iwe safi ilhali hujaosha shati kila siku. Kutafsiri kamwe ni neno kwa neno lakini kuonyesha maana. Sina wasiwasi, utapata uzoefu! Kipala (majadiliano) 05:25, 10 Septemba 2020 (UTC)Reply

Kwa Marejeo usisahau kuweka chini yake msimbo wa <references/> , itahakikisha tanbihi zinaonekana mahali panapotakiwa. Kipala (majadiliano) 05:29, 10 Septemba 2020 (UTC)Reply
Ahsante sana Kipala, nitazidi kujifunza kuboresha zaidi. Czeus25 Masele (majadiliano) 19:26, 10 Septemba 2020 (UTC)Reply

Uteuzi kuwa mkabidhi

hariri

Salaam! Ulipendekezwa na kukubaliwa kupata haki za mkabidhi. Je, uko tayari kupokea uteuzi huu na kushiriki katika kazi mara kwa mara kama jinsi ilivyoelezwa katika ukurasa wa wakabidhi? Tunaomba jibu lako kwa baruapepe katika wiki hii. Tumia zana za Wikipedia kutuma barua pepe. --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 07:43, 13 Septemba 2020 (UTC)Reply

Majadiliano ya ufutaji

hariri

Ukichangia kuhusu ufutaji wa makala, usiandike pekee kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala, usisahau kuipeleka pia kwenye ukurasa wa ufutaji, maana maazimio yanafanywa pale. Kipala (majadiliano) 21:43, 14 Septemba 2020 (UTC)Reply

Sawa, nitafanya hivyo. Czeus25 Masele (majadiliano) 21:47, 14 Septemba 2020 (UTC)Reply

Jamii Forums

hariri

JamiiForums ni mtandao wa kijamii maarufu zaidi nchini Tanzania ulioanzishwa rasmi mwaka 2006 mwezi Machi ikiwa na waanzilishi wawili, Maxence Melo na Mike Mushi ambao walijuana kupitia mtandao wakati ambao mtandao ukiwa dubwana geni si tu Tanzania lakini sehemu kubwa ya dunia, wakati huo ikijulikana kama Jambo Forums na jina hilo lilidumu kwa miaka miwili pekee.

Historia

hariri

Uanzilishi

hariri

JamboForums ilikuja baada ya kuwa na majukwaa mbalimbali kama Tanzania Economic Forum, Habari Tanzania, Jambo Network, Jambo Radio na Jambo Videos.

Kila tovuti ilikuwa na malengo tofauti lakini yote yakilenga kuwahudumia watu wa nyanja husika kuweza kupata sehemu ya kusemea au kubadilishana mawazo.

Lengo kuu la JF likiwa ni kuanzisha Jamvi moja ambapo wadau watakutana na kubadilishana mawazo huku wakikubali kutokubaliana (utofauti wa mawazo) na kujenga mijadala endelevu. Katika Jambo Network (jambonetwork.com) au JamboRadio.com mijadala ilikuwa kwa mtindo wa chat ambapo hakukuwa na kumbukumbu baada ya mjadala, hii ilipelekea mijadala mingi kuwa inarudiwa na kusababisha kukosa mwelekeo kabisa.

Katika uanzilishi lengo kubwa lilikuwa kuwafikia wazungumzaji wa kiswahili wa eneo la Maziwa Makuu na hata watumiaji wengi wa Kiingereza lakini wenye kupenda kujua habari za ukanda huu.

Mkusanyiko wa majukwaa haya ulipelekea kuwa na kusanyiko moja ambalo kwa wakati huo (2006) liliitwa JamboForums.com, jina ambalo lilitumika hadi mwezi Mei 2008

Mabadiliko ya jina

hariri

Mwaka 2008 yalifanyika maamuzi ya haraka na ya lazima kwa wakati huo kwa kubadili jina kutoka Jambo Forums kwenda JamiiForums. Jina la JamiiForums lilichagizwa na kubakia na kifupi cha JF kutoka kuwakilisha neno JamboForums na sasa kuwakilisha neno JamiiForums.

Jina lililazimika kubadilishwa kutokana na mgongano wa matumizi ya jina la JamboForums ambapo lilikuwa halijachukuliwa haki miliki (copyrights) za jina ingawa baadaye walifanikiwa kulimiliki kihalali.

Uongozi haukutaka kusimamisha moja kwa moja matumizi ya JF hivyo wakafikiria jina mbadala la JamboForums na kubaini kuwa tayari hili kusanyiko la wadau ni kusanyiko la Jamii, na bado Jamii ilikuwa ikiendelea kutunza JF kama wengi wanavyopenda kufupisha.

Madhumuni ya kuanzisha JF

hariri

Lengo kubwa la uanzishwaji wa JF likiwa ni kuwafikia wazungumzaji wa Kiswahili wa eneo la Maziwa Makuu na hata watumiaji wengi wa Kiingereza lakini wenye kupenda kujua habari za ukanda huu kwa kutoa uwanja huru wa kujadili kwa wanachama wake ambao sio shuruti kutumia majina yao halisi.

Mafanikio

hariri

Kwa miaka yote iliyodumu, Jamiiforums imekuwa msaada katika nyanja nyingi ikiwemo siasa, michezo, afya, habari na hasa habari mtambuka. Mtandao wa JamiiForums unatoa fursa ya kipekee ya kujadili habari na hoja mbalimbali badala ya habari kulishwa kwa upande mmoja.

JamiiForums imetoa fursa kwa wananchi wa kawaida kujadiliana na viongozi wa juu katika serikali na taasisi mbalimbali pia watu maarufu katika jamii ambao kwa namna moja au nyingine ingekuwa ngumu kwao kuwapata. Mfano watu maarufu ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania ambae alipata kuwa katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani Tanzania na kuwania urais mwaka 2010, Dr. Wilbrod Peter Slaa, Mwigulu Nchemba ambae aliwahi kuwa naibu wizara ya fedha na mgombea aliekuwa anawania kupewa tiketi ya Urais kwa niaba ya chama tawala, chama cha Mapinduzi, aliekuwa naibu katibu mkuu chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Kabwe Zuberi Zitto pia baadhi ya taasisi kubwa nchini kama TCRA ambao ni wadhibiti wa mawasiliano Tanzania.

JamiiForums kutokana kuwa na wanachama wa aina mbalimbali ina wataalam waliobobea katika fani mbalimbali ambao wanaweza kutoa majibu ya kitaalamu kulingana na fani zao ambapo si ajabu muhusika angelipia kama wangekutana ofisini ama kuibiwa. Mifano inajumuisha ujenzi, afya, teknologia pia inajumuisha uchambuzi makini katika siasa na chaguzi za miaka nenda rudi kwa kutoa mawazo mbadala na kufikisha sauti za watu wasioweza kusikika.

Mfano wa mijadala JamiiForums

hariri

ELIMUTIBA: Jinsi ya kujieleza kwa Daktari

Yaliyojiri Bungeni: Ijumaa, 28 Novemba 2014 (Hatma ya Sakata la Tegeta Escrow Account)

WALIMU: Kwa wale wanaotaka kubadilishana vituo vya kazi

Kitabu gani ambacho kimewahi kubadilisha maisha yako na unatamani wengine tukisome?

Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma, kuiba jina

Mahojiano ya moja kwa moja na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe katika JamiiForums

Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Chanzo/uthibitishaji habari JamiiForums

hariri

Hili kwa muda mrefu limekuwa swali kwa watu wengi kwa jinsi gani JamiiForums wanadhibiti habari za uongo na nini chanzo cha habari zao. JamiiForums ni mtandao wa kijamii na si gazeti wala redio lakini utofauti wake wenyewe wameweka wahariri ambao kazi yao kubwa ni kusimamia sheria za majadiliano walizojiwekea lakini pia ikiwekwa habari na wanachama wake inayotiliwa shaka basi hufatilia na kuthibisha au kubatilisha.

FikraPevu

hariri

Kuongeza ufanisi na uhakika wa habari zake, kilianzishwa kitengo maalum kinachohusika na habari ambapo huaririwa na waandishi na kuchapishwa kwenye mtandao wa www.FikraPevu.com ambapo ni gazeti mahsusi la mtandaoni kwani kuwazuia watu kuweka habari mpaka uthibitisho kwenye JamiiForums ilionekana ni ukirikitimba na ungeelekea kwenye mkwamo. Wanachama wa JF wamekuwa waungwana na pale ambapo mwanachama mwenzao akipotosha basi kuna nafasi ya kuripoti ili usawa uwekwe.

Takwimu

hariri

Kwa mwaka 2012 JamiiForums ilikuwa na wanachama zaidi ya 100,000 na kupata watembeleaji 50,000 kila siku. Kulingana na mtandao wa statscrop.com ambao hupima tovuti mbalimbali, JamiiForums ina thamani ya $3,182,721.

Wanachama wakongwe

hariri
Faili:JamboForums.jpg

Pamoja na JF kuwa na wanachama wengi lakini wapo wanachama walioanza tangu JamboForums inaanza mwaka 2006 na wangine wamekuwa nayo kwa takriban miaka kumi sasa. Mafano wa wanachama hao ni Mzee Mwanakijiji, Rev. Kishoka, Augustine Moshi, Kyoma, Mwawado, Mkandara, Kibunango, Steve Dii Mwafrika wa Kike, Kichuguu Choveki Masatu Masanja Quemu Mlalahoi Mtanzania Bibi Ntilie Game Theory jmushi1 Zakumi Moelex23 na wengineo wengi.

JamiiForums kwenye mitandao ya kijamii

hariri

Pamoja na kuwa mtandao wa kijamii maarufu zaidi ukanda wa Afrika Mashariki wenye asili ya Tanzania, JamiiForums inazo kurasa kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook ikiwa na wafuatiliaji wengi zaidi Afrika Mashariki takribani 3,200,000 mpaka September 2019 pia JamiiForums ina kurasa yake katika mtandao wa Twitter na Instagram..

Kuna Pendekezo la ufutaji wa Makala uliyoanzisha, hivyo unaweza kuiboresha zaidi ili kuepushwa kufutwa.

Majadiliano:Jihadi

hariri

Nimerudisha matini ya mtumiaji:JJOSY2000, maana si vizuri tukijaribu kuficha ukosoaji. Akikosoa (bila matusi, bila fujo) ni haki yake, hata kama sababu anazoleta ni dhaifu na mabadiliko aliyoleta hayawezi kubaki maana anaanza kugusa uwanja wa mahubiri. Sitashughulika usiku huu. Kipala (majadiliano) 21:15, 18 Januari 2021 (UTC)Reply

Sawa, ahsante kwa taarifa. Czeus25 Masele (majadiliano) 19:12, 19 Januari 2021 (UTC)Reply

Boot Camps article

hariri

This is my first try and you guys attack me instant. I know is some kind robotic but Im working on it plus to add more sources. Just give me a chance. I will proof read it until tommorow and add more citations.

You seems passionate user:Crapalan‬ and thats a good start. But we can't keep such article not knowing when you gonna improve it. Next time try to pe patient and perfect the article before publishing. You may have as more practices into your sandbox as many times as you can. Peaceful!! Czeus25 Masele (majadiliano) 17:28, 1 Juni 2021 (UTC)Reply

Kituo cha reli Luebeck Travemuende Strand

hariri

Hello Bro, I d like to ask you if you could check the grammar of this article please? I am in a starters level in Kiswahili yet and for sure I wrote some typos. Thank you! Alex. 87.153.174.166 20:42, 24 Agosti 2021 (UTC)Reply

Okay I will check Czeus25 Masele (majadiliano) 21:14, 24 Agosti 2021 (UTC)Reply

We can finish up the article together if you want, I know the station and the district. You know the Kiswahili language. 87.153.174.166 11:44, 25 Agosti 2021 (UTC)Reply

Okay, please login or share username so as I can contact you easily to help you with the translation. Thanks Czeus25 Masele (majadiliano) 20:45, 25 Agosti 2021 (UTC)Reply

You can email me directly to denjakvienna@gmail.com please. What informations do you want to addict into this article? 87.153.174.166 11:35, 26 Agosti 2021 (UTC) Bro could you help me to translate some words because google translate gives stuff only, how would you call:Reply

  • timetable
  • network map
  • ticket validators
  • equipment

In Kiswahili? Regards, Alex 87.153.174.166 22:01, 27 Agosti 2021 (UTC)Reply

  • timetable ( Ratiba)
  • network map (Mchoro wa ramani ya mtandao)
  • ticket validators (Wakatisha tiketi/Wakaguzi wa tiketi))
  • equipment (Kifaa)

Czeus25 Masele (majadiliano) 22:16, 27 Agosti 2021 (UTC)Reply

How we will see unregistered users

hariri

Hi!

You get this message because you are an admin on a Wikimedia wiki.

When someone edits a Wikimedia wiki without being logged in today, we show their IP address. As you may already know, we will not be able to do this in the future. This is a decision by the Wikimedia Foundation Legal department, because norms and regulations for privacy online have changed.

Instead of the IP we will show a masked identity. You as an admin will still be able to access the IP. There will also be a new user right for those who need to see the full IPs of unregistered users to fight vandalism, harassment and spam without being admins. Patrollers will also see part of the IP even without this user right. We are also working on better tools to help.

If you have not seen it before, you can read more on Meta. If you want to make sure you don’t miss technical changes on the Wikimedia wikis, you can subscribe to the weekly technical newsletter.

We have two suggested ways this identity could work. We would appreciate your feedback on which way you think would work best for you and your wiki, now and in the future. You can let us know on the talk page. You can write in your language. The suggestions were posted in October and we will decide after 17 January.

Thank you. /Johan (WMF)

18:19, 4 Januari 2022 (UTC)

Thanks Czeus25 Masele (majadiliano) 05:59, 5 Januari 2022 (UTC)Reply

Have you voted in the UCoC enforcement guidelines ratification?

hariri

Hi! @Czeus25 Masele:

The ratification voting process for the revised enforcement guidelines of the Universal Code of Conduct (UCoC) is now open! Voting commenced on SecurePoll on 7 March 2022 and will conclude on 21 March 2022. Please read more on the voter information and eligibility details.

Please vote and encourage other editors of Swahili Wikipedia to also vote.

Regards, Zuz (WMF) (majadiliano) 12:23, 11 Machi 2022 (UTC)Reply

Thanks Czeus25 Masele (majadiliano) 16:12, 14 Machi 2022 (UTC)Reply

King Kikii

hariri

Original state of "King Kikii" contains nothing but misspellings of it as Kiki with SINGLE "i". Kokamamie (majadiliano) 09:56, 23 Novemba 2024 (UTC)Reply

Thanks Mtumiaji:Kokamamie; please refer below:
Tanzanian rumba maestro King Kikii passes away at 77 | The Citizen ~2024-18927 (talk) 13:01, 25 Novemba 2024 (UTC)Reply