Majadiliano ya kigezo:Afrika

Nimegundua kwamba nchi ya Ginekweta (ilivyoandikwa kwenye ukurasa huu) imeingizwa kama Guinea ya Ikweta (tena ni makala nzuri). Sasa sina uhakika, tubadilishe jina la nchi hapa, au weka #REDIRECT, au tufanye nini? Oliver Stegen 08:53, 3 May 2006 (UTC)

Tena ni mimi - kwa sababu vilevile kwa Sao Tome na Principe kuna makala chini ya São Tomé e Príncipe, na kwa Kameruni kuna makala chini ya Kamerun. (Na labda kuna mengine ambayo sijayagundua.) Je, kuna orodha ya majina ya nchi kwa lugha ya Kiswahili ambayo tuifuate? Oliver Stegen 08:58, 3 May 2006 (UTC)
Unauliza swali nzuri. Kuna tatizo. Nimetengeneza templeti kwa kutumia orodha ya nchi iliyotengenezwa na sijui nani. Kati yetu sisi wachache kuna wengine wanopendelea kuandika majina jinsi wanavyotamka wenyewe. Tumeshajadiliana tayari matatizo ya tahijia tuemona tufuate kamusi za TUKI kwa kawaida. (Kwa mfano: majina ya sayari hata TUKI wanakosa ninayvoona mimi). Mimi naweza kurejea kamusi mbalimbali za TUKI.
Kuhusu majina ya jiografia nina tatizo ya kwamba TUKI hawana majina mengi ya kijiografia (vilevile kihistoria) katika kamusi zao. Tufanye nini? Nasikia kuna orodha ya TUKI lakini sijaipata kama kijitabu.
Mapendekezo yafuatayo: Kwa sasa twende ama na majina ya Kiswahili sahihi (kama yapo: Shelisheli n.k.) au majina ya wenyewe. Au kama ni rahisi kwa kuchanganya, kwa mfano Guinea ya Ikweta. Halafu tuunde "REDIRECT" za kutosha. (Kodivaa RED Cote d'Ivoire; Swaziland RED Uswazi n.k.). Watumiaji wengi wa wikipedia yetu hawajui umbo lipi la neno litakuwa sawa.
Swali la herufi zisizopatikana kwa Kiswahili: Sipendi kuzitumia katika jina la makala, Matt anazipenda. Si kitu, tunaweza kuweka Redirect kwa njia yoyote.
Je, uko wewe TZ mwenyewe wakati huu? Kama unaweza kupata vitabu vinyoonyesha ramani (atlasi) uwe mhariri wetu. Ingawa ningesema uwe na vitabu angalau viwili tofauti kwa sababu imani yangu katika ubora wa uhariri wa vitabyu vya shule TZ si kubwa sana.
Nimebadilisha sasa templeti. --Kipala 09:33, 3 May 2006 (UTC)
Sasa hivi nipo Chuo Kikuu cha Edinburgh. Nitakapokuwa nimerudi Tanzania wiki ijayo bahati mbaya sitakuwa na nafasi ya kutumia mtandao mara kwa mara. Lakini nitahamia Ujerumani mwezi wa Julai. Baada ya hapo nitakuwa 'active' tena. Oliver Stegen 10:01, 3 May 2006 (UTC)
Return to "Afrika" page.